CV ya Dr Slaa From Certificate to PhD

CV ya Dr Slaa From Certificate to PhD

Status
Not open for further replies.
Dr mi nakukubali hasa ukinzingatia nimepitia seminari pia nimekua mlei mwema.

Nilishangaa walipo kuletea nape eti ujadiliane nae topic.
 
KWA UMRI WENU MNAJADILI ELIMU MTU?
KWELI FB fungulia mbwaa!.
 
Niliwaandikia siku moja. Kuwa mtendajimkuu wa baraza la maaskofu wa kikatoliki lazima uwe na kichwa si kichwa, cha kufuga vywele! Unawaongoza mabingwa wa elimu wa kikatoliki!
 
KWA UMRI WENU MNAJADILI ELIMU YA MTU?
KWELI FB fungulia mbwaa!.
 
Sasa DR. Slaa elimu yake anaitetea ya nini wakati kashafikisha umri wa kustaafu?
Mkuu eti ile costa inayokuwaga kwenye msafara wa kipenzi chenu na wazee kibao ndani huwa wanasghulika na nani? Samahani lkn
 
Dr mi nakukubali hasa ukinzingatia nimepitia seminari pia nimekua mlei mwema.

Mie nilikuwa Katekista, bado Mulugo nae aje atoe ufafanuzi, heri yangu nilieishia Form IV science lakini halali kuliko wale wenye elimu za juu ila zina maswali mengi kama ya Mulugo, anyway Slaa ni jembe kwenye elimu
 
Katika watu ninaowaheshimu kwa michango yao humu ndani ni Zemarcopolo, HARMY D, CHAMA, Utakuwa umewakosea heshima mkuu.

hawa huwa wanajadili watu tuu hakuna lolote. bora hata ritz huwa kwenye hoja anajadili hoja.
 
tatizo la ccm kuwapa vijana vijisent kupiga propaganda mitandaon tunaanza kuliona..wengi wao wanaandika puuzuri na ushabiki wa kitaarabu taarabu
 
bora cv ya ungumbaru inayojieleza kuliko ya phd ya kutokea kwenye certificate, ukiacha slaa tutajie msomi mwingine aliepata phd akitokea kwenye Certificate
Sheikh Simba ana masters ya Islamic studies toka chuo kikuu cha Misri baada ya kuhitimu darasa la nne!
 
Njaa zinawafanya vijana wa Lumumba wawehuke kwa kutafuta visa vya kutunga na kukebehi ili kushusha hadhi ya mtu.Hiyo siyo siasa ila ni utumwa wa kifikra japokuwa inawezekana mnafaidika kiuchumi kwa hoja dhaifu kama hizi.
 
Kwa vile kasoma mambo ya dini sana ; mi naona mambo ya dunia ajui lolote. Namshauri rudi kundini ueneze neno ; huku tuachie kaisari. Sijaona kasoma shule za kata wa la serikali kwa hiyo hajui machungu ya maisha hawezi kutetea lolote; usilolijua ni kama usku wa giza et slaa
 
EDITED
Wabongo msiwe mnaenda enda tu tu jamani ndo mana mnasaini mikataba ya iliyoandikwa KICHINA .
 
EDITED
Wabongo msiwe mnaenda enda tu tu jamani ndo mana mnasaini mikataba iliyoandikwa KICHINA .
 
Slaa ajitetea kuhusu elimu yake. Jionee mwenyewe
By Dr.W.Slaa :
Ndahani,
Ni haki Yao kujadili. Msiwapuuze
wala kuwakatisha tamaa kujadili.
Inawezekana kweli wapo ambao
kwa nia njema hawajui mfumo wa
Elimu wa Kanisa Katoliki ambao tok
a Seminary Ndogo ( Form 1-V1)
nimepitia Dungunyi Seminary and
Itaga Seminary of which am very
proud na ninatoa shukrani za dhati
kabisa kwa waalimu wangu wote si
tu kwa kunipa elimu bora, Bali pia
kwa kunipa misingi imara ya malezi
( formation) kwani elimu bora ni
zaidi ya vyeti.
Aidha si wengi wanaojua
Philosophia hasa wanafundisha nini.
Kwa bahati mbaya kuna watu
wanadhani wameelimika na kuwa
mavuvuzela kumbe hawajui kitu,
ndio maana ya msemo " nusu elimu
ni hatari sana". Kuna watu Leo
ukiwaambia kuwa masomo ya
philosophia( falsafa) yanahusu
subjects muhimu Kama 1) Ethics 2)
Logic 3)Epistemology 4) Cosmology
5) Metaphysics 6) Psychology na
philosophy yenyewe yaani misingi
ya philosophy hawaelewi
unazungumzia nini na si kosa lao.
Kuhoji is not an issue, issue ni je
anayehoji anahitaji kujifunza au
anahoji kwa ushabiki tu! This is the
issue at stake!
Wako watu wanafikiria Seminary
Kuu unajifunza Theolojia ( Tauhidi).
Hawajui kabisa kuwa miaka 5 ya
masomo ya Theolojia ni pamoja na
complete course on Sociology,
Anthropology, Oratory,miezi Sita ya
mwisho nilipata complete course ya
ukunga kwa kuwa ukiwaambia
Padre vijijini wewe pia ni
ambalance, hivyo lazima ujue
basics za kumhudumia mama
mjamzito unayemkimbiza hospital
ini na kadhalika. Msomi yeyote,
kabla ya kuhukumu anaanza kwa
kutafuta ukweli juu ya jambo na
kufanya utafiti. Prospectus ya
Seminary Kuu ambazo ziko affiliated
kwa vyuo vikuu mbalimbali duniani
zinapatikana, hivyo hakuna msingi
wa mtu kufanya guess work, labda
awe tu na sababu zake na au
agenda yake ambayo nintofauti na
lengo la elimu ambayo ni kutafuta
"full truth" ambayo nayo ni msingi
wa Somo la Epistemology katika
masomo ya Philosophy(Fals-afa).
Katika Vyuo vikuu, ikiwa ni pamoja
na Chuo Kikuu cha Urbaniana
( Roma) nilikosoma Mimi, pamoja na
miaka 7 ya Seminary Kuu
nilizosoma (Kibosho Major
Seminary/ Moshi na Kipalapala
Major Seminary ambazo zilikuwa
affiliated kwa Kwa Makerere
University na Ndiyo maana vyetu
vyangu ni vya Makerere University
na Urbaniana Pontifical University
Rome, 1) Nilianza na Bacclaureate
( equivalent ya BA) na kuandika
Paper baada ya Course Work, na
Licentiate ( Masters) nayo
nikaiandikia Paper na kufaulu, ndipo
nikaruhusiwa kuendelea na JCD).
2) Napennda pia kuwafahamisha
kuwa wengi kwa kutokuelewa
wanafikiria kuwa JCD inafundisha tu
Canon Law. Pamoja na Canon Law
masomo mengine ni 1) Civic Law
( ambayo ni msingi wa sheria zote
inayotokana na Roman Law), 2)
Family Law( ikumbukwe Kanisa
Katoliki ina mfumo kamili wa ki
mahakama kuanzia Courts of First
Instance hadi court of Appeal
( Sacred Rota) na Supreme Court
( signature Apostolica). Huu ni
mfumo kamili wa ki mahakama,
kwa kawaida ukijishughulish-a na
maswala yote ya ndoa,na
Patrimony. 3) Jurisprudence 4)
comparative Law French,
Commonwealth, American, Russian
kwa maana nyingine all major Legal
Systems worldwide. 5) International
Law na branches zake zote. 6)
Principles of criminal Law
( elements ambazo haiku kwenye
Comparative Law na Civic Law.
Ili kufanya Desertation yangu,
nilipaswa kujifunza Lugha 5 ( nje ya
Kiingereza ambayo kwa wanafunzi
wa English Speaking Countries
inahesabiwa kuwa Mother Tongue,
Latin ambayo kwa aliyetoka
Seminary Kama nilivyopitia Mimi
inahesabiwa Kama original
language, na Hebrew ambayo pia
kwa mtu aliyepitia Seminary it was
taken as on Original language, japo
Mimi sikuwahi kujifunza Hebrew
Seminarini). Hivyo nikachagua a)Ki
Italiano ambayo pia ndiyo ilikuwa
Mwdium of Instruction yaani lugha
ya kufundishia,b) Kijerumani
c)French d) Spanish na e)
Portuguese. Hata hivyo focus yangu
ilikuwa kwa Italian na German na
mengine matte nilijifunza kuweza
kufanya research yangu, na
kuniwezesha kusoma lakini Siko
fluent katika kuzungumza.Hii pia ni
kutokana na muda mfupi. Nilipata
course ya Wiki 3 tu ya kujifunza
Lugha kabla sijaingia darasani kwa
masomo proper.
Nimeyaweka kwa uwazi, na
ninadhani wako wanaofahamu
mfumo wa masomo katika vyuo vya
Kanisa Katoliki wanaweza kujazia.
Wako ambao tumesoma nao was
mapadre katika Pontifical
Universities za Rome, Leo
wanashika nafasi kubwa katika
Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania au nafasi zinging
mbalimbali kwenye Taasisi
mbalimbali. Kwa kuwa nilienda
Roma nikiwa tayari Mkurugenzi wa
Maendeleo Jimbo Katoliki la Mbulu,
nikawa Nina shuttle Kati ya
Pontifical University ya Urbaniana
na Pontifical University ya St.
Thomas Aquinas, Rome ambako
nilisomea Advance Diploma ya Rural
Development.
Nadhani sasa mnaweza kupima
kwa vigezo hivi hoja za mleta
thread hii. Mnaweza kupima nini ni
puma na nini ni mchele. Mnaweza
pia objectively kuangalia depth ya
masomo kwa kulinganisha na
propaganda nyingi zinazopigwa kwa
malengo tu ya upotoshwaji na au
Propaganda. Vyuo vikuu Biko
kwenye mitandao, mleta thread na
wengine wa aina yake wakijisumbua
kidogo tu kuingia kwenye Google
watapata ukweli bila kutafuniwa na
mtu. Tuweke uvivu wa kufikiri
pembeni tunapojadili mambo
makubwa na mazito. Nafasi ya kila
mmoja kujipatia Elimu bora ipo
Kama watu tutakubali kujisumbua na
kuacha uvivu wa kufikiri. Nchi
haitaendelea kwa propaganda na
otoshwaji, Taifa halitaendelea kwa
wivu....shika Kitabu. Soma.
Jichimbie utavuna lakini Kama
utakesha kwenye mitandao kufanya
Propaganda badala ya kuchota
elimu bora tena ya bure kwenye
mitandao utaachwa unajiozea!
Nawahimiza wote wenye kupenda
Taifa lao kujichimbia. Innovation ni
msingi wa maendelo na Innovation
haipatikani kwa majungu na umbeya
inapatikana kwa wanaochimbia
vichwa vyao kwenye utafiti,
kujisomea na kujiendeleza. Tupende
Taifa letu, uzalendo uwe kwa
matendo na sio Maneno matupu.
Mzee slaa umezungumza vitu vingi sana ktk elimu yako na hongera ulipofika lakini kanisa katoliki linafundisha pia nidhamu na uadilifu sasa wewe uadilifu wa kikatoliki uliuacha wapi hadi ukawa ulivyo mtu wa historia na matukio mabaya kabisa.
 
Dah ! Kweli nimeamini Slaa ni balaa aisee ! Hebu tuichambue na elimu ya Katibu Mkuu wa CCM na yule wa CUF , huyu SAM LUHUZA wa NCCR- MAGEUZI tuachane naye , nina hakika kuna watu watabadili ID'S zao kesho asubuhi.
Do not waste your time and resources. Elimu ya Dr Slaa haitofautiani sana na ya Pope Francis. Umewahi kujiuliza kwa nini rais wa Marekani (Super power) anakaogopa sana haka ka taifa (Vatican state) kasiko hata na jeshi kuliko, China au Russia? Think twice. Mbumbumbu wa chini kabisa kwenye taifa la Vaticano ana elimu ya kiwango cha shahada ya uzamili. Unakumbuka Bush alivyokwenda kujikomba kwa John Paul ii na vinishani mshenzi baada ya ku mess mambo huko Iraq? The Vatican is no Mecca my bro!
 
Ninaamini sio Dr Slaa ameandika haya maneno...sio yeye kabisa japo elimu yake ndo hii na wote ni ukweli...ila hii ni mtu kaifraft
 
Nami naomba kuuliza juu ya taaluma ya Mheshimiwa Slaa. Inaonekana alidahiliwa kusoma PhD kwa miaka 4 (1977-1981). Hiyo inakubalika kimataifa. Lakini msingi wangu wa swali ni pale ndani ya hiyo miaka 4 kusoma taaluma 2 tofauti kwa vyuo tofauti lakini shahada and stashahada zote kutolewa mwaka huo huo (1981)! Je PhD ilisomwa miaka miwili tu (1977-1970)? Je inakubalika popote?
 
Mzee slaa umevunja amri nyingi sana za kanisa katoliki miongoni mwa hizo ni kutamani mke asiye mke wako,usiibe,usizini,usiibe,shika sheria katoliki za ndoa,usiseme uongo sheria hizina zingine nyingi hakika umezivunja.
 
Theology(tauhidi) dr kanifundisha kitu hapa yaani kumbe kanisani wanafundishwa tauhidi?
Tauhidi=upwekeshaji=mungu mmoja=kuacha kumuabudu mungu pamoja na wengine kama masanamu. Sijui ndio maana yake pia huko kwenye christian theological studies? Someone to help me please.
Msomi tauhidi/theology huwa heshima na maadili yake yanakuwa ya juu sana na ikiwa kinyume chake atakuwa course ameikimbia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom