CUF yazindua Kongamano la kudai Katiba mpya, yataka maoni ya wananchi kuheshimiwa

Bado sijakuelewa vizuri unamaana gani. Embu dadavua vizuri bwana deeppond
Katika kusoma Kuna mambo mawili ya muhimu

1. Kuna kusoma ili Elimu IKUKOMBOE

2. Kuna kusoma ili UIKOMBOE Elimu.

Sasa uyu mzee wetu, Miaka yote kasota vyuoni kuihangaikia hoja namba 2 Apo juu.
 
Maneno ya Mhe.Rais ni kweli tupu, amesema hatoongeza hata siku moja madarakani.

Miradi mikubwa aliyoanzisha haitakuwa imekamilika; kwa vyovyote vile SGR na mradi wa Kufua umeme Rufiji haitakuwa imekamilika, hivyo wapambe wake wa kutoka kanda ya ziwa watalazimisha aendelee sio kwa maslahi ya nchi bali kwa maslahi yao!!! Na yeye atakubali kwa kisingizio cha kwamba chama kimemlazimisha na Ndugai ndio atakuwa mstari wa mbele kushabikia!!!!

Usimsikilize anaposema kuwa hataongeza muda, mbona kuongopa ni jadi yake; kumbuka alivyodanganya kuwa angetoa STIMULUS ya 50million kwa kila kijiji!!!
 
Chama cha CUF jana kimezindua Kongamano la kudai Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi, ikiwa ni siku 53 baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika.

Akifungua Kongamano hilo, Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba ametoa rai kwa Rais John Magufuli kuheshimu maoni ya wananchi kwa kuwapatia Katiba mpya na Tume Huru.

Vilevile, amesema Rais anatakiwa kuheshimu ukomo wa Uongozi uliopo kwa mujibu wa Katiba na kuepuka majaribio yoyote ya kumuwezesha kukaa madarakani kwa muda mrefu.

Amesema Rais anapaswa kufufua mchakato ya kuandika Katiba mpya kuwapatia Watanzania Tume huru ya Uchaguzi itakayoubganisha Taifa na kufuta machungu yaliyotokana na Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Ameongezaa kuwa, rasimu ya Katiba mpya iliyo chini ya Jaji Mstaafu Joseph Warioba imekidhi matakwa ya wananchi walio wengi na jukumu alilobaki nalo Rais ni kuhitimisha mchakato huo.

======

The opposition Civic United Front (CUF) on Sunday, December 20, 2020 organized a congress gathering national leaders, members of the national congress and members to discuss on the demand for the new constitution and an independent electoral commission.

The conference was organized 53 days after the conclusion of this year’s General Election that saw President John Magufuli re-elected and the ruling CCM increasing domination in the Parliament and local councils.

Opening the conference, the party’s chairman Prof Ibrahim Lipumba asked Dr Magufuli to respect citizen’s opinion by providing them with the new constitution and the independent electoral commission.

“Dr Magufuli should revive the new Katiba writing process now in order to provide citizens with an independent electoral commission in order to unify the country and cure it from wounds resulting from the 2020 General Election,” he said.

The economics professor who turned politician said President Magufuli should also respect the leadership term limit provided by the constitution and ignore any attempts of making him a life president.

He said since the draft constitution from the defunct Constitution Review Commission (CRC) under Judge (rtd) Joseph Warioba has accommodated most citizens’ opinions; the president’s remained with the task to finalize the process.

Former Bukoba Urban MP Wilfred Lwakatare said the two demands should bring together all Tanzanians, political parties, academia, Civil Society Organizations (CSOs), clerics etc.

However, the new constitution is not in the ruling party’s manifesto.
 
Hizi ndo harakati pekee zenye maana za kufanywa na vyama vya upinzani kwa sasa. Ukweli ni kwamba wapinzani hawajawahi kuvalia njuga kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi vitu ambavyo ni vya msingi katika kuhakikisha usawa kwenye masuala ya kidemokrasia. Vyama vingine navyo vianze vuguvugu hili.
 
Binafsi sioni umuhimu wa kudai katiba mpya wakati hata hii iliyopo tumeshindwa kuisimamia ,mfn hii katiba iliyopo inasema mbunge akifukuzwa uwanachama ubunge wake utakoma muda huo huo ,sasa juzi kuna wabunge wamefukuzwa uanachama lakini sipika anasema bado ni wabunge ina maana ameikanyaga katiba wazi wazi.

Katiba inasema mikutano ya vyama vya siasa ni haki ya kila chama na maandamano ya amani ruksa lakini bado kuna mbabe mmoja amesema mikutano na maandamano ni jinai 🤔 ,wazo lao ni zuri lakini wangepambana kwanza kukemea ukiukwaji wa katiba maana hata ikiletwa mpya kama hatujajenga misingi ya kuheshimu katiba tutakwama.
 
Wanakumbuka shuka asubuhi!

Tanzania hii ya maccm hawawezi kukubali hiyo katiba mpya na hawawezi kuwapatieni hiyo katiba mpya.

Tumieni njia nyingine ya kupata katiba mpya.
 
Back
Top Bottom