CUF yapinga bara kupewa ardhi Z’bar

CUF yapinga bara kupewa ardhi Z’bar

Ikija kwenye masuala ya kibaguzi kama haya wanasema "waasisi wa muungano" na yakija mambo serious "wanasema ulikuwa muungano wa Karume na Nyerere"
Waingereza wanaita "double standards"
 
  • Thanks
Reactions: bdo
undugu wetu "wewe ukiishiwa chumvi rukra kuja kuniomba ila mi nikiishiwa siruhusiwi kabisa kuja kuomba chumvi kwako"
hapa lazima kuna ulakini ktk undugu wetu
 
Kweli hii imesema mengi. Bila shaka ni mmoja wa wanaotaka Sultani arudi Zanzibar. Hajali maslahi ta wapemba wenye ardhi na vitega uchumi/biashara Tanganyika

Kwan Sultan anakushulisha nn wwe mtu Pori, hata kama akirudi Wazanzibar ndio wenye mamlaka ya kumpokea, sio nyie Watu Pori!!
 
Kusema ukweli, muungano hauna faida yoyote kwa Tanganyika. Tanganyika ina shida, badala ya kushughulikia shida zake inakwenda kumbeba mtu asiyejua anachotaka. Inatosha sasa. Ama zenji wanachagia ipasavyo kwenye muungano au hakuna muungano.
 
Ni vizuri wanasiasa na Wazanzibari wote wakaelewa na kujipanga, kuwaandalia Mazingira au maeneo ya kuhamia Wazanzibar kwa walioko huku Bara kwa sasa.
Maana kama hawatakuwa tayari kufungua milango kwenye zoezi la Uhuru wa kumiliki ardhi kwa pande zote za Muungano. Uwepeo wa Tanganyika baada ya Katiba hii hautawacha salama Wazanzibar wote walioko Tanganyika na hii haitaishia hapo itakwenda mbali (Unguja VS Pemba).

Wengine mtakumbuka Maneno ya Hayati JK-Nyerere.

NB.Ni vigumu Wazanzibar wakafurahia Ardhi Bara na wabara wawe wakuja wakiwa Kule zanzibar wacha tu subiri!
Wachaga vs Wamasai -Umesahau kina lowasa.
Wanyamwezi vs wakurya
Wapare vs Warangi.

Ukimbukwe kuwa Tanganyika kuna mababila zaidi ya 20 sijui nanyi mutaishi vipi, kutagawana mikoa,

P.S
Kama wazanzibari watatengena na wapemba sio vibaya hilo ni jukumu la wazanzibari na sio kuwasemea, hivyo basi bado sisi tutaishi kwa salama zaidi kwa kutengena baina ya Pemba na unguja.

Hata hivyo hizo siasa za unguja na Upemba hazina nafasi tena kwetu, ni nyimbo za wafuasi wa nyerere katika kuwatawala wananchi kisaikolojia kama unavyo tawaliwa wewe na ccm kwa upumbavu wako.
 
Ukimbukwe kuwa Tanganyika kuna mababila zaidi ya 20 sijui nanyi mutaishi vipi, kutagawana mikoa,
Tanaganyika ina makablila zaidi ya 120. Unapotaka kuandika jambo jiridhishe kwanza kwamba unalifahamu vinginevyo unatueleza habari kuhusu wewe na uwezo wako bila sisi kuomba

Wanyamwezi na Wakurya wana tatizo gani? Jiografia haionyeshi kuwa wapo karibu
Wapare wanatoka Kilimanjaro, Warangi Singida, mikoa hiyo haina mpaka

Tatizo la znz ni kusikia hadithi na ni mafundi wa kueneza hadithi za kusimuliwa. Muda wa kwenda library ni kidogo sana.
Wznz tatizo lenu si muungano, ni zaidi ya hapo
 
kwa ubaguzi huu zanzibar iachwe iende salama! Umejaa ubaguzi mpaka kwenye kope.!

Nasikia kule Zenj kama huitwi Adamu, Hasani nk au hujui kula wali kwa mkono unaweza tengwa na jamii! nijulisheni wadau!
 
undugu wetu "wewe
ukiishiwa chumvi rukra kuja kuniomba ila mi nikiishiwa siruhusiwi kabisa
kuja kuomba chumvi kwako"
hapa lazima kuna ulakini ktk undugu wetu

Unavyo wewe! halafu ni tegemezi kwako. inakubidi umwache tu ili kupunguza malumbano yasiyo ya msingi!
 

Attachments

  • Adamuphoto.JPG
    Adamuphoto.JPG
    11.2 KB · Views: 60
Hapa nilipo kuna jirani yangu ambaye ni mzanzibar pure na anamiliki ardhi ya kutosha. Sasa huu uzi umenifungua macho kuwa kumbe ile ardhi inaweza kuwa yangu muda wowote,ni suala la muda tuuuu. Huyu jirani yangu alishawahi kumkatalia mtoto wangu wa mwanaume alipoenda kuchumbia kwake kwa kigezo cha kwamba suala la kuoleana si la muungano!!!!, kumbe hata ardhi nayo cyo suala la muungano!! Huyu jamaa atanikoma kwenye hili suala la ardhi lazima alikimbie jiji la sivyo akubali kijana wangu amuoe binti yake.

Teh teh teh!
 
Kama Wanzibar ruksa kupewa ardhi bara, Zanzibar ikijaa si watakuja bara na kuishi mahali popote wanapopataka? Hata hivyo ni uchoyo unaowasumbua nani aliwaambia wabara wanahitaji sana kuishi Zanzibar. Kuruhusu haina maana wabara wote watataka kwenda Pemba.Unaweza ukaruhusu wanafunzi wote kwenda kuangalia Disco lakini sio wote wataenda wengine ni wakristo au waislamu safi. Kuna watu hawataki kuhama kwao hata ungewajengea nyumba bure Pemba
Lazima Tuwe wakweli. Hivi wakija Watu millioni 2 tu kutoka Bara wakataka ardhi kweli tunayo ardhi hiyo. WaZanzibari wapo 1.2 million kuna matatizo ya kugombea ardhi
 
wasiotambua uwepo wa Tanganyika ni wa bara (ccm)wasiotaka wabara wamiliki ardhi znz ni wabara (ccm) sisi wa bara ndo tunaweza kuamua huu muungano uweje ( kwa vile tuko wengi na ardhi kubwa basi sisi ndo waamuuzi ila sisi hatutaki) tusiwalaumu waznz kwa msimamo wao wenzetu wanajitambua.
 
pole sana mkuu, naomba uhangaike na uitafute katiba ya zanzibar utaiona inasemaje kuhusu haki ya kumiliki ardhi ipo kwa nani! Huu ubaguzi hauvumiliki hata kidogo mkuu!

Inasema Mtanganyika hana haki?
 
huo uzushi usiulete hapa mkuu!

Nyie Watanganyika mnapenda kukurupuka kama ni uzushi basi si ungetaka uthibitisho? Nakwambia tena Mtanganyika anaweza kumiliki ardhi akifuata utaratibu na hili la utaratibu si kwa Mtanganyika tu bali hata Wazanzibari wenyewe.
 
Mkuu hilo ni jema sana na ndivyo inavyotakiwa kuwa.kuna aliyeandika kwamba wabara milioni 2 wakija huko watapata wapi ardhi nilikuwa napingana na hilo,kama inaruhusiwa kumiliki ardhi ni vyema.

Kwani unafikiri sio kweli kuwa Watanganyika millioni 2 wakija watakosa ardhi? Hiyo inabaki ukweli.
 
Kama Wanzibar ruksa kupewa ardhi bara, Zanzibar ikijaa si watakuja bara na kuishi mahali popote wanapopataka? Hata hivyo ni uchoyo unaowasumbua nani aliwaambia wabara wanahitaji sana kuishi Zanzibar. Kuruhusu haina maana wabara wote watataka kwenda Pemba.Unaweza ukaruhusu wanafunzi wote kwenda kuangalia Disco lakini sio wote wataenda wengine ni wakristo au waislamu safi. Kuna watu hawataki kuhama kwao hata ungewajengea nyumba bure Pemba

Unajuwa mimi huwa nakushangaeni nyie na wengine ni viongozi wakubwa tu serikalini wakilizungumza hili la ardhi ya Zanzibar kama ni tofauti na ardhi ya Tanganyika. Hivyo wapi kusiko na utaratibu wa kumiliki ardhi?
Jee pale wafugaji na wakulima wanapozuiliwa kutumia ardhi watakavyo inakuwa nini ni ubaguzi au ni utaratibu. Utaratibu wa makazi uko duniani kote na taratibu huwekwa kwa sababu maalum. Inakuwaje tabu kwa Zanzibar kuweka taratibu za makazi na umiliki wa ardhi na kwanini iwe nongwa kwa wanaotaka kuhamia wasifuate taratibu za kupata ardhi hiyo?

Makelele yanayopigwa ni ya bure kwani hakuna kipengele hata kimoja cha katiba kilichomzuia Mtanganyika kumiliki ardhi lakini tatizo ni kuwa taratibu zilizowekwa hawataki kuzifuata na wachache walioelewa mbona wanamiliki ardhi Zanzibar!
 
duh...mkuu hesabu na reaction zako zinatisha...hiyo decimation unayomfanyia uyo mzenji ingekuwa kwenye battle field ange surrended within few minutes

Siyo ange "surrended" bali ange surrender. Kuna shida gani ukiandika Kiswahili Mkuu?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Lazima Tuwe wakweli. Hivi wakija Watu millioni 2 tu kutoka Bara wakataka ardhi kweli tunayo ardhi hiyo. WaZanzibari wapo 1.2 million kuna matatizo ya kugombea ardhi

Kwa hiyo wote wakae kwao sio? Natamani wazenji wasimiliki ardhi bara pia maana wataja jazana huku pia! Watu wenyewe wazaa kama nzige!
 
Back
Top Bottom