wabara
JF-Expert Member
- Sep 30, 2013
- 1,500
- 706
Wazenji wana Tabia za Uchoyo sana yaani chao ni chao Ardhi ya Wazenji ni ya wazenji tu lakini Ardhi ya watanganyika ni Ardhi ya wote Tambueni Kuwa wapemba wengi sana wanamiliki Ardhi huku Tanganyika na hawapati Vikwazo wakati wa kununua viwanja mashamba nk Lakini Mtu wa Bara akitaka kumiliki Ardhi Zenji inakuwa issue ! Watu wa Bara wanabaguliwa Zenji eti wamewabatiza majina wanawaita Vichogo au Chogo yaani Utazani wao wamesahau Kuwa pale walipelekwa Enzi ya Utumwa asili Yao ni huku huku Bara kwa kweli Wazenji wana Vituko sana Siku muungano Ukiwa marehemu watawakumbuka sana watanganyika Maana Mkoloni Mwarabu wanayetaka kumrejesha hataki vuvuzela atawanyoosha hadi wanyooke
Mie ni mbaara kabisaa, lakini nina miliki nyumba huko Zanzibar, hayo maneno mangine nani kakunywesha..?
Na hakuna Mzanzibar wala Mpemba ang'ang'aniaye ati Tanganyikwa, bali Wazanzibar wana madai yao ya muhimu na tatizo kubwa kabisa laanzia pale katika ule ati Muungano.
Ina maana jambo hilo hulifahamu ama watumia uburu wa jirani yako kutafakari mambo..?
Wakati mwangine jaribu kuketi pekeako na utafakari kwamba, hivi wanachodai Wazanzibar kina maana au ni wameamua tu..? Kisha picha hiyo ijenge upande wako kuwa weye ndo Mzanzibar na viongozi wako wamekutenda kiasi hicho, je, utapata muda wa kuleta maropoko kama hayo...?!!
Choyo wanacho wahodhio madaraka na wenye tamaa kama waliopo SIASANI.
Hapo namaanisha wale waililiao ati kukamata madaraka ilhaali uadilifu waishaanza uvunja hata kabla hawajapewa nchi.
Na weye jigeiye muda ili kutafakari mambo kwa faida ya kuonesha uendeaji wa mambo na si kufuata fuata kiushabiki.