CUF yapinga bara kupewa ardhi Z’bar

CUF yapinga bara kupewa ardhi Z’bar

Lazima Tuwe wakweli. Hivi wakija Watu millioni 2 tu kutoka Bara wakataka ardhi kweli tunayo ardhi hiyo. WaZanzibari wapo 1.2 million kuna matatizo ya kugombea ardhi
Mkuu hapa swala ni utanzania,kama sheria ni kwamba ardhi siyo mali ya muungano mbona wazanzibar wanamiliki ardhi huku bara?
kama issue ni ukubwa wa ardhi kwa nini wanyarwanda wamarudishwa kwao kama waamihaji haramu?
 
yaaani mimi toka nijue cuf...wamekuwa wakipigania......
1.uhuru wa wapemba........
2.sera zao zilijikita katika dini
3.muungano wa uvunjikee.....

Lakini wenzao chadema...muda mwingi wa wanaoutmiaa

1.katika kujenga hoja nzito bungeni......
2.kujenga chama chao....

3.kuunesha nia ya kwenda ikuluuu

Mkuu utakuwa umezaliwa juzi tu basi. Kwa sababu mi tangu nizaliwe Cuf nimegundua kuwa CUF ya zanzibar ipo kutetea maslahi ya WAZANZIBARI, sera zake zimejikita zaid katika UZANZIBARI, na pia haina sera ya kuvunja muungano bali serikali 3!!! Chadema tangu nzaliwe naona wao wapo katika ukanda tu, ukabila, udini, kutafuta umaarufu kupitia matukio, kutafuta sympathy ya wananchi, kufuja mali za chama kwa kukopeshana, kuzuia demokrasia na kumfukuza kila anaitishia kuchukua madaraka ya bamkwe na padre, kikubwa Zaidi, CHADEMA hakina nia nzuri na zanzibar, wala zanzibar hawana time nayo. Nikuweke wazi kidogo, fikra inayokufanya uone kuwa CUF ni cha cha waislam ambayo ni fikra batil, tambua kuwa Cuf ni waasi wa Ccm, na zanzibar tangu kipindi icho waislam ni 99% sasa sijui ingetosha vipi 1% wakristo kuonekana katika chama icho na hasa ukizingatia wakristo wao ni CCM kwa zanzibar, mngelikuwa cdm mpo zenjy mngeliwachukua wakristo weni
 
Chama Cha Wananchi(CUF) kimepinga wazo na rai ya kupunguza masharti ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ili kulegeza nguvu zake kisheria na kuwapa fursa Watanzania Bara kumiliki ardhi Visiwani Zanzibar.

Msimamo huo umetolewa na Mkurugenzi wa Habari na Mwasiliano ya Umma wa CUF Salum Bimani katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana visiwani humo, siku chache baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(Muungano) Samia Suluhu Hassan, kushauri Katiba ya Zanzibar kuangaliwa upya na kuwapa nafasi Watanzania Bara kumiliki ardhi Zanzibar.

Bimani alisema kuwa suala la ardhi siyo la Muungano tangu mkataba wa awali wenye orodha ya mambo ya Muungano na siyo sahihi kufanyika marekebisho ili kuwapa nafasi Watanzania Bara kumiliki ardhi Zanzibar kwani ni ndogo na ndiyo sababu hata waasisi wa Muumgano waliamua ardhi hiyo imilikiwe na wazanzibari pekee. Chanzo mwananchi

Ikija kwenye masuala ya kibaguzi kama haya wanasema "waasisi wa muungano" na yakija mambo serious "wanasema ulikuwa muungano wa Karume na Nyerere"
 
Hapa nilipo kuna jirani yangu ambaye ni mzanzibar pure na anamiliki ardhi ya kutosha. Sasa huu uzi umenifungua macho kuwa kumbe ile ardhi inaweza kuwa yangu muda wowote,ni suala la muda tuuuu. Huyu jirani yangu alishawahi kumkatalia mtoto wangu wa mwanaume alipoenda kuchumbia kwake kwa kigezo cha kwamba suala la kuoleana si la muungano!!!!, kumbe hata ardhi nayo cyo suala la muungano!! Huyu jamaa atanikoma kwenye hili suala la ardhi lazima alikimbie jiji la sivyo akubali kijana wangu amuoe binti yake.

hahahahahahaa! Kaaaaazi kwelikweli. Ndio hivyo mkuu. Mshauri tu mkubaliane ili umteteeee kuwa ni mtanga wakati wa msako wa wazanzibar wanaoshi bara utakapoanza. Huku songea wapo lkn hawataki kusikia habari za muungano, wanasema wao ni watz.Mungu apishe mbali.
 
Chama Cha Wananchi(CUF) kimepinga wazo na rai ya kupunguza masharti ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ili kulegeza nguvu zake kisheria na kuwapa fursa Watanzania Bara kumiliki ardhi Visiwani Zanzibar. Msimamo huo umetolewa na Mkurugenzi wa Habari na Mwasiliano ya Umma wa CUF Salum Bimani katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana visiwani humo, siku chache baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(Muungano) Samia Suluhu Hassan, kushauri Katiba ya Zanzibar kuangaliwa upya na kuwapa nafasi Watanzania Bara kumiliki ardhi Zanzibar. Bimani alisema kuwa suala la ardhi siyo la Muungano tangu mkataba wa awali wenye orodha ya mambo ya Muungano na siyo sahihi kufanyika marekebisho ili kuwapa nafasi Watanzania Bara kumiliki ardhi Zanzibar kwani ni ndogo na ndiyo sababu hata waasisi wa Muumgano waliamua ardhi hiyo imilikiwe na wazanzibari pekee. Chanzo mwananchi
ukiwa mchoyo usiwe mroho!
 
Jalood,
Kwani hata Tanganyika kila mtu ana ardhi? Kinachotakiwa hapa ni kwamba Mtanganyika awe na haki sawa ya kumiliki ardhi Zanzibar kama ambavyo Mzanzibari ana haki ya kumiliki ardhi Tanganyika.

Kwa mfano kama kuna mtu anauza kiwanja Zanzibar, basi mtu mwenye asili ya Tanganytika asinyimwe haki ya kununua kwasababu tu anatoka Tanganyika. Mgawanyo wa ardhi utategemea supply and demand.

Kwa asilimia kubwa ya watu hakuna kitakachobadilika. Ila kwa asilimia ndogo ya Watanganyika wanaoishi Zanzibar, hii sheria ya kibaguzi ikiondoka watakuwa na haki sawa ya kumiliki mashamba na kujenga nyumba zao.

Kama Wazanzibari hamtaki hili ni wazi mtapata madhara zaidi kwani na huku bara itabidi sheria kama hiyo hiyo ya Zanzibar itungwe na maelfu ya watu wa Zanzibar ambao wana mashamba na nyumba huku TZ itabidi wanyang'anywe.
Lazima Tuwe wakweli. Hivi wakija Watu millioni 2 tu kutoka Bara wakataka ardhi kweli tunayo ardhi hiyo. WaZanzibari wapo 1.2 million kuna matatizo ya kugombea ardhi
 
Wazanzibar wanatamani mambo ya zanzibar yawe ya kwao, wakati wanataka ya tanganyika iwe ya wote! Huu muungano ni wa kihuni kwelikweli!

tunataka wabunge wa zanzibar katika bunge la jamhuri warudishe posho zote walizopokea wakati bunge linajadili mambo yasiyo ya muungano na wapige hesabu kuanzia mwaka 1964, unakuta mzanzibari povu linamtoka kujadili bajeti ya wizara ya mifugo au ustawi wa jamii wakati halimhusu
 
Naunga mkono cuf.
Haya maneno ya huyu bini ni kujikomba.mungejua hawa ccm walivo wanafiki msinge isema cuf.
Hakuna watu walio kua hawana mwelekeo kama ccm znz.
Hivi mnajua kuwa wazanzibar walioko bara hawaruhusiwi kumuliki ardhi huko kwao znz?
Basi kwanza wangebadili katiba kuwaruhusu wa znz waishio bara kuwa na haki hio.
Ni ujinga tu kujipendekeza kwa bara ili walindwe hata kwa gharama ya kuuza nchi yao
 
Hapa nilipo kuna jirani yangu ambaye ni mzanzibar pure na anamiliki ardhi ya kutosha. Sasa huu uzi umenifungua macho kuwa kumbe ile ardhi inaweza kuwa yangu muda wowote,ni suala la muda tuuuu. Huyu jirani yangu alishawahi kumkatalia mtoto wangu wa mwanaume alipoenda kuchumbia kwake kwa kigezo cha kwamba suala la kuoleana si la muungano!!!!, kumbe hata ardhi nayo cyo suala la muungano!! Huyu jamaa atanikoma kwenye hili suala la ardhi lazima alikimbie jiji la sivyo akubali kijana wangu amuoe binti yake.

hahahahhaha! eti kuoleana haipo kwenye muungano.
naona mate yashakutoka kwa ardhi ya mpemba!
 
Lazima Tuwe wakweli. Hivi wakija Watu millioni 2 tu kutoka Bara wakataka ardhi kweli tunayo ardhi hiyo. WaZanzibari wapo 1.2 million kuna matatizo ya kugombea ardhi[/
QUOTE]
ndio mana naamini wazanzibar wengi wajinga...........sasa kwa nini munalilia tugawane pato la taifa wakati hiki kitongoji munachokiita nchi Temaake tu hamujai!!!!!!!!
 
Hapa nilipo kuna jirani yangu ambaye ni mzanzibar pure na anamiliki ardhi ya kutosha. Sasa huu uzi umenifungua macho kuwa kumbe ile ardhi inaweza kuwa yangu muda wowote,ni suala la muda tuuuu. Huyu jirani yangu alishawahi kumkatalia mtoto wangu wa mwanaume alipoenda kuchumbia kwake kwa kigezo cha kwamba suala la kuoleana si la muungano!!!!, kumbe hata ardhi nayo cyo suala la muungano!! Huyu jamaa atanikoma kwenye hili suala la ardhi lazima alikimbie jiji la sivyo akubali kijana wangu amuoe binti yake.
 
ninavyojua mimi ni kwamba wako Watanzania bara wengi tu wenye
kumiliki ardhi huko visiwani pamoja na makanisa ambayo ni ya bara;
au vp? Kiongozi anaemiliki hecta 500 Morogoro, 300 Bagamoyo, 250
Mbeya na bado anatamaa ya hect 400 Zanzibar ili azihodhi tu haiewzekani.
Kihistoria Zanzibar imekuwa nchi huru baada ya kanisa kuwepo zanzibar,mkuu usipotoshe umma.
 
Hata kama ardhi ni ndogo si automatically tutaikosa sasa hadi muifanye rasmi /kisheria? Suala hapo sio udogo wa ardhi bali ubaguzi. Hata huku bara ardhi haitutoshi.
 
Back
Top Bottom