CUF wataka Waziri Masha na IGP Mwema wajiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF wataka Waziri Masha na IGP Mwema wajiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jul 30, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,654
  Trophy Points: 280
  CUF wataka Waziri Masha na IGP Mwema wajiuzuluNa Salim Said

  CHAMA cha Wananchi (CUF) kimewataka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Laurence Masha na Mkuu Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema kujiuzulu mara moja kwa kushindwa kudhibiti matukio ya ajali nchini.

  Mwenyekiti wa CUF Taifa Profesa Ibrahim Lipumba jana alisema ajali zinazotokea nchini zinatokana na utendaji mbovu wa wakuu hao pamoja na uzembe wa madereva.

  Alisema ajali hizo zimekuwa zikisababisha upotevu wa nguvu kazi na rasilimali za taifa na kuongeza idadi kubwa ya watu wenye ulemavu.

  Profesa Lipumba alisema Waziri Masha na IGP Mwema, wamezidiwa nguvu na wauaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) pamoja na madereva wazembe.

  “Kwa hivyo tunawataka waziri Masha na IGP Mwema wawajibike kwa kujiuzulu nyadhifa zao mara moja, ili kunusuru nchi na kuwapisha wengine watakaomudu na kulinda usalama wa raia na mali zao.

  “Pia serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inapaswa kuchukua hatua mahsusi za kubaini vyanzo vya ajali, zinazotokea mara kwa mara nchini, ili kuweza kuzidhibiti pamoja na kuangalia upya adhabu kwa wanaosababisha ajali,” alisema Profesa Lipumba.

  Wakati huohuo, CUF imetoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa, familia na marafiki watu 27, waliokufa katika ajali ya Basi la Mohamed Trans, iliyotokea juzi baada ya basi hilo kugongana na lori la mizigo wilayani Korogwe mkoani Tanga.

  Basi hilo, lililikuwa njiani kutoka Nairobi Kenya kuja Dar es Salaam Tanzania, liligongana uso kwa uso na lori la mizigo lililokuwa limebeba bia katika eneo hilo.
  Profesa Lipumba alisema kwamba, “tumepokea habari za msiba huo kwa masikitiko makubwa na tunatoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na familia za marehemu wote,” alisema kwa masikitiko.
  Tuma maoni kwa
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  badala ya kumtaka spika ajiuzulu wanawavamia wasio husika

  kwani ajali tatizo ni jeshi la polisi au SUMATRA?

  mbona hawakutoa rambi rambi kwa waliofariki ajali ya meli ya Pemba?
   
Loading...