Mimi naona kwa hili kuwa kama Zanzibar vyama viwili ndio vimeungana serikari ya Kitaifa kwa nini wasihusishe na vyama vingine huko zenji?
Hivi tatizo la CUF ni nini?Mkuu tukiangalia hivyo na tukienda down that road utaanza kuona kwamba wote wana makosa. Maana CUF wanaonekana ni Waislamu na Chadema Wakatoliki/Wachaga. Udini upo na ukabila upo sikatai. Hata katika hali ya kawaida mtu ukiwa na nafasi uka kutana na mtu wa kabila lako au dini yako una kuta ni rahisi zaidi kuwasaidia ila haimaanishi wewe ni mkabila au mdini.
Ila mkuu hamna haja ya mimi na wewe kubishana. Unaweza kuwa sahihi kusema udini umechangia nami nasema muafaka nao kwa kiasi kikubwa umechangia. Mbona wakati CUF ndiyo wameunda baraza kivuli bunge lililo pita wali washirikisha Chadema? Wakati huo udini haukuepo? Kwa mantiki hilo swala la kwanza linalo kuja kichwani mwangu ni kwamba it's not a matter of "udini" per se bali inferiority complex inayo izuia CUF kuwa chini ya Chadema kwenye baraza kivuli ndani ya Bunge.
Hivi na CHADEMA Walipokuwa wanakampeni kama wakipewa ridhaa kuongoza wataunda serikali ya umoja au sura ya kitaifa walikuwa wanamaanisha nini?Na je hiyo serikali wangeiunda na watu kutoka vyama gani?Mundo, you have nailed it all mkuu; kama kweli Hamad Rashid anaiponda CHADEMA kwa kutotaka kushirikisha vyama vingine vya upinzani zaidi ya CUF wao CUF na CCM wangeshirikisha vyama vingine pia kuunda serikali huko Zanzibra, kitu ambacho CUF hawakukifanya huko Zanzibar kwa nini wanalazimisha kifanywe na CHADEMA huku Bara? UNAFIKI!
Hapa ninachoona, na kipo wazi ni kuwa CUF kipo kwa manufaa ya Wazanzibari zaidi na si Watanzania, wao wamepata huko Zanzibar ambapo ndipo walipopapigania hadi kumwaga damu basi hawana haja na ukombozi wa Watanganyika!
Ukitafakari kura za wagombea uwakilishi SADC kwa upande wa upinzani utagundua kuwa Wabunge wote wa CCM, NCCR, TLP, CUF etc walimpigia mgombea kupitia CUF. Hii inathibitisha kuwa CCM na CUF ni kitu kimoja na ndio sababu mgombea wa CUF alijitoa kugombea unaibu spika ili apate support ya CCM kwenye uwakilishi SADC:nono:[/QUOTE
Ni sawa na Marando miaka ya nyuma kambi ya upinzani ilikuwa haimtaki awawakilishe kwenye ubunge wa afrika mashariki lkn CCM iliamua kumpa kura kibao ili kuwatesa upinzani.Lkn hivi leo hili halionekani kuwa ni tatizo.Ninachotaka kuanisha hapa ni kwamba ktk siasa kuna mbinu za kutumia kufikia malengo au baadhi ya malengo ya kiitikadi,sera au utekelezwaji wa ilani wa vyama sasa hili linaweza kufikiwa kwa njia ya makubaliano baina ya vyama viwili vyenye mtazamo tofauti na hii haimanishi kwamba kwa kufanya hivyo vyama hivyo ni mamluki.
cuf waweke mambo yao sawa kwanza kwa kuwa cuf zina mapande manne 1cuf mageuzi 2cuf upemba 3cuf udini 4cuf uccm tushirikiane na cuf ipi ili cuf ipi isichonge?maana kila cuf ina malengo yake....
Katika siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu.Mimi naona mambo matatu, kwanza kuwa ile mbegu ya udini aliyopanda Kikwete sasa inaanza kustawi, pili makombo toka kwenye meza y CCM sasa yameishibisha CUF mpaka imevimbiwa, tatu ile ndoa ya CCM na CUF sasa imejibu mimba changa ndiyo inawapa tabu CUF mpaka wanaweweseka.
Jamani kumbe CHADEMA wana maadui wengi ,CUF wanakeraa sana ,toka waunde serikali(waolewe) na CCM wana nyodo sana.Sijui mimba inawasumbua?? Khaa!!!!!!!!:angry:
Napata Wakati mgumu sana ni wapi democrasia ya kweli tunaipeleka CUF Ni chama kilichokubalina na CCMkuendesha Serikali ya pamoja Zanzibar leo tena kije kuungana na CHADEMA ilikufanya kazi pamoja YA UPINZANI BUNGENI.CUF inasimamia wapi kukosoa Kazi zake inayotekeleza kikiwa madarakani ama kusaidia kutekeleza Ilani ya CCM kama walivyokubali Zanzibarkwa ni sitashangaa kusikia JK akimteua Waziri toka CUF kwani ni wamoja hao.MKINISAIDIA HAPO BASI NITAJUA CHADEMA wanatakiwa kusimama upande wa CUF ama peke yao?tusiwe blinds kwenye hili... Lazima tuelewe ukweli kabla ya kudhani CUF hawana point
Much as we seek for changes, it has to be very systematic and sophisticated... nadhani kuna haja ya CHADEMA ku-take things slow and cut off drama ili wajipange upya, including kujenga kambi ya upinzani
Nakumbuka niliuliza kuhusu kambi ya upinzani, nikaambiwa kwamba CHADEMA ndio walikua na haki ya kufanya, lakini naamini kama wangeamau kukaribisha wapinzani wote, hilo lingeleta maana zaidi na ile courtesy ingezaa imani ndani ya upinzani
Najifunza hayo masiasa because i am for changes lakini nadhani kuna tatizo kidogo... haiwezekani wewe tu ndio uchukiwe na kila mtu
Having said that, nashauri wakuu chadema wakae chini na wa-shut down media for three months kupunguza impurities and reach out to wapinzani ili kujenga upya upinzani
Loud and clear... CUF wameamua kuwa wanafiki... lakini cha maana ni chadema kurudi kambini na kupanga upya mambo yao
Thanks for the post
Sijui wengine mmepokeaje taarifa hii, tutaona mtakavyochangia.
Mimi nilipoipokea tu moja kwa moja nikatafuta sentensi ambapo Hamadi ataeleza ni kanuni gani ya bunge ambayo CHADEMA wameivunja. Hakuna hata sentensi moja. Ni tatizo, kubwa tu la CUF.
Kuna ugonjwa mbaya unaoanzia hata kwenye jamii na kuendelea hadi kwenye makundi makubwa ya kitaifa kama vyama. Ugonjwa huo uko hivi: tunajua kwamba fulani anaweza kufanya jambo fulani tulipendalo kwa hiari yake na utashi wake tu.
Lakini badala ya kumuomba na kumuacha hiari yake na utashi wake vimsukume kufanya tupendalo kale ka-ugonjwa kanatusukuma tumshinikize hadi ile hiari yake igeuke kuwa kama lazima.
Ukweli unabaki palepale kwamba kelele hata kama ni za dunia nzima haziwezi kugeuza jambo la hiari kuwa la lazima. Tukifanikiwa kulilazimisha na hivi vishinikizo vyetu basi huo nao ni ufisadi mwingine wa kupora hiari ya mtu\chama na kuifanya lazima.
Ndicho wanachokifanya wenzetu hawa bahati nzuri Hamad haelezi kuwa kama CHADEMA waliwahi kushinikiza hiari kama wao sasa hivi.
Tumejadili kanuni za bunge kuhusu hili na hapa tuzisome tena vifungu vyake:
14(2):
Wabunge wote wa Upinzani wanaweza kuunda Kambi Rasmi ya Upinzani iwapo idadi yao itakuwa si chini ya asilimia 12.5 ya Wabunge wote.
14(3):
Chama cha Upinzani hakitakuwa na haki ya kuchagua Kiongozi wa Upinzani Bungeni, isipokuwa tu kama kina idadi ya Wabunge wasiopungua 12.5% ya Wabunge wote.
14(4):
Endapo kutakuwa na Vyama vya Upinzani zaidi ya kimoja ambavyo kila kimoja kina Wabunge 12.5% au zaidi, basi Chama chenye idadi kubwa zaidi ya Wabunge kuliko vingine ndicho kitakuwa na haki ya kuchagua Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, lakini, ikiwa kutakuwa na vyama viwili au zaidi vyenye idadi sawa ya Wabunge ambao ni zaidi ya 12.5%, Wabunge wa vyama vinavyohusika watachagua Kiongozi wa Upinzani Bungeni chini ya utaratibu watakaokubaliana wenyewe.
15(1):
Chama chenye haki ya kumchagua Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kinaweza pia kuchagua Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.
15(2):
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni atateua Wabunge wa Chama chake au Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambao watakuwa wasemaji wakuu wa Kambi ya Upinzani kwa Wizara zilizopo za Serikali.