CUF waishambulia CHADEMA

kama yepi ?

kukubali vyama viwili kuunda umoja na kuviona vyengine kwa kua na uwakilishi mdogo si wapinzani ?

chadema mtulie muache makeke

ngoma yataka matao

Huwezi kuunda umoja na watu kama mrema ambaye ametangaza hadharani kumuunga mkono Kikwete na ccm hata katika kampeni za uchaguzi. Hata Mwenyekiti wa NCCR tangu mwanzo ni mpinzani wa chadema hadharani badala ya kuwa mpinzani wa ccm

Hivyo huwezi kuungana na watu ambao ni wapinzani wako
 
ALIYEKUWA kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni katika Bunge lililopita, Hamad Rashid Mohamed amewashambulia viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuwataka wawe na msimamo na wafanye uamuzi kisiasa kama watu wazima.

Hamad amewatuhumu Chadema kuwa wabaguzi kwa kuwa walitaka kushirikiana na Chama Cha Wananchi (CUF) kuunda kambi hiyo lakini walidhamiria kuvitenga vyama vingine ya upinzani.

Mbunge huyo wa Wawi (CUF) alimewaeleza waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, wao (CUF) hawana shida ya vyeo kwa kuwa waliwahi kuwa na madaraka makubwa kuliko ya kwenye hiyo kambi ya upinzani bungeni.

Amewataka viongozi wa Chadema wawe ‘matured’ na watambue pia gharama za kisiasa za kutomtambua Rais Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa Hamad, CUF wana msimamo, waliwahi kufanya uamuzi mgumu na wakautekeleza hivyo Chadema wajifunze kwao (CUF).

Alisema, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alimfuata akamueleza nia ya kushirikiana na CUF kuunda kambi ya upinzani bungeni lakini kwa kuvitenga vyama vingine vyenye wabunge katika Bunge hilo.

Hamad amesema, alikataa wazo la Mbowe na akampa ushauri ambao hadi sasa hajautekeleza.

Mwanasiasa huyo amesema, CUF wanataka kambi ya upinzani bungeni ushirikishe vyama vyote vya upinzani, Chadema hawataki.

Hamad amesema, viongozi wa Chadema wamemkwaza Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, hivyo waende wakazungumze nao wayamalize.

Source: Basil Msongo,HabariLeo ,Dodoma; Tarehe: 18th November 2010
Ni sawa wao si ni chama tawala wakishirikiana na CCM.
 
Chadema endeleeni na mipango yenu na kutekeleza majukumu yenu ya Bunge kwa mujibu wa katiba na kanuni za Bunge. CUF ni CCM na hayo maneno ya Hamad Rashid ni ya kuibomoa Chadema.
 
Nimecheka sana, Yaani sasa malengo ya CUF yanaanza kuwa crystal clear. Yaani CUF ndo wanawaonya Chadema kuwa kuna madhara ya kutomtambua rais aliyetangazwa na tume? CUF ambao wamemkataa karume kule Zanzibar hadi juzi juzi tu baada ya kurushiwa peremende? Sasa CUF wanaanza rasmi kuifanya kazi ya CCM ya kuishauri Chadema imtambue rais!!

Sasa iwe wazi, kwa wale wote waliokuwa wakiamini kuwa CUF inaweza ikawa mpinzani bara wakati Zanzibar wako serikalini, kuwa hilo halipo. Na anayesema CUF na Chadema wanaweza kuunda kambi ya upinzani haitakii mema kambi hiyo na pengine haoni haja ya kuwa na kambi ya upinzani. Na kusema kweli ni CCM pekee anayeweza kuona hilo la CUF kuungana na Chadema kwenye kambi ya upinzani ni jambo jema.

CUF walikuwa wanashirikishwa. Sasa huo usemaji wa vyama vingine CUF wamepewa lini? Yaani CUF wanaambiwa karibuni tuunde kambi ya upinzani, lakini wao wanasema ili sisi tuje inabidi na NCCR, UDP na TLP wawemo!! Si TLP, UDP wala NCCR waliokwishasema kuwa wanataka kuingia kwenye hiyo kambi. Sasa CUF wamepataje hiyo 'authority' ya kuvisemea hivyo vyama vingine??

CUF ni moja na CCM ni moja, kule Zanzibar na huku bara pia! Ni kujilisha upepo kuamini kuwa CUF na CCM sasa hivi watatofautiana kwa lolote, nasema ni kujilisha upepo. Sasa hivi wao, lao moja, nalo ni kuona kuwa ajenda za serikali zao zinapita bila kupigiwa kelele na yeyote.
 
Mkuu tukiangalia hivyo na tukienda down that road utaanza kuona kwamba wote wana makosa. Maana CUF wanaonekana ni Waislamu na Chadema Wakatoliki/Wachaga. Udini upo na ukabila upo sikatai. Hata katika hali ya kawaida mtu ukiwa na nafasi uka kutana na mtu wa kabila lako au dini yako una kuta ni rahisi zaidi kuwasaidia ila haimaanishi wewe ni mkabila au mdini.

Ila mkuu hamna haja ya mimi na wewe kubishana. Unaweza kuwa sahihi kusema udini umechangia nami nasema muafaka nao kwa kiasi kikubwa umechangia. Mbona wakati CUF ndiyo wameunda baraza kivuli bunge lililo pita wali washirikisha Chadema? Wakati huo udini haukuepo? Kwa mantiki hilo swala la kwanza linalo kuja kichwani mwangu ni kwamba it's not a matter of "udini" per se bali inferiority complex inayo izuia CUF kuwa chini ya Chadema kwenye baraza kivuli ndani ya Bunge.

political analyst
 
Kuna watu hawana Misimamo kisiasa ..Hawa Cuf nao waache longolongo zao tofauti zao wakae chini wamalize kama zipo..
Mapema hii wamenza vijimane lol:doh:
 
This is very absurd! Wamelaghaiwa na hao manyumbu (CCM) wanajiona wao nao wameula! Chamsingi hapa CHADEMA msikubali kuwa distracted! Mnatakiwa kuwa na agenda and you have to stand for it and push it loud and clear! Always agenda yenu iwe ni maslahi ya taifa hili! Tanzanians will always be your allies! TUKO PAMOJA. HATUDANGANYIKI
 
Jamani kumbukeni CUF ya leo sio ya jana, mimi naamini CUF ni moja kama vile CCM ilivyo moja, haiwezekani hata kidogo CUF zanzibar ikakubaliana na serikali wakati CUF bara ikasema haikubaliani na serikali kwani serikali anayoikataa Dr. Silaha ndiyo inayoongoza visiwani pia.

Then ni vigumu kwa CUF kuwa chama cha upinzani baada ya makubaliano ya zanzibar, hilo haliwezekani na halitatokea hata siku moja unless tunajidanganya kwa ndoto za mchana.

Lazima tukubaliane na hilo kuwa sasa CUF watatekeleza matakwa ya serikali na hakuna kingine, sasa tuangalie kwanini CHADEMA haikutaka kuungana na vyama vingine, chama kama NCCR Mageuzi mgogoro ulianzia kwenye kampeni baada ya habari za kuwa James Mbatia anachukua mshahara CCM, hapa hakuna jinsi CHADEMA inaweza kuungana na NCCR Mageuzi kwani hawataelewana hata maongezi hayatakuwepo hata kidogo

Chama kilichobakia hapo ni UDP ambacho nacho kinajulikana kwa kuwa CCM B, then CHADEMA hawakuwa na option zaidi ya kuunda serikali ya upinzani wao wenyewe.

Chama cha upinzani bungeni ni CHADEMA tu wengine wote wamepoteza credibility ya kuwa chama cha upinzani, hapa sina maana ya kuwa wapinzani wa kupinga kila kitu lakini lazima tuangalie conflict of interest kwa kila chama, kwani kwa CUF wako bound hawataweza kupinga hata kile ambacho kitakuwa sio kwa masilahi ya nchi.

Kwa mawazo yangu, CUF nao sasa ni Mafisadi kama CCM na wanahitaji kusafishwa pia kabla ya uchaguzi wa 2015 ili waweze kukubalika kama chama cha upinzani

Hii ni opportunity kwa CHADEMA kujipanga upya na kutumia hizi loop holes zilizojitokeza na kupata wanachama na washabiki zaidi, Dr. Silaha azunguke nchi nzima na kujipanga upya, CHADEMA hamuhitaji kumkataa Rais Kikwete kwani itasabisha vurugu mtashindwa hata kujipanga upya, naamini the war is not over but you lost the batle so wake up jipangeni upya hachaneni na vyama vingine, hacheni marumbano na watu simamieni mnapoamini kuwa mko sahihi

Thats my view, i stand to be corrected nilipokosea
 
Huyu Hamad anataka CHADEMA iwashilikishe Mrema (TLP) na Mbatia (NCCR - Mageuzi) ambao ni wazi ni vibaraka wa CCM. Angalia HAMADI huyu huyu kwa kushindwa kuungana na CHADEMA haihalalishi kuuinga mkono CCM hii ni aibu na Muelewe CUF ni Chama MFU kwani kina kiti kimmoja bara walipo watu zaidi ya 95% ya nchi. RIP na udini wao VIti vyote vya ubunge walivyonavyo ni vya waislamu na huyu mmoja ameolewa na mwislamu. Makafiri hao.
 
Jamani kama CUF sio wabinafsi ilikuwaje wakafanya mwafaka bila kushirikisha wapinzani wengine?

Kwanini ni wao tu wanajiona wako sahihi kila siku, ile hali wao wamekubali kuungana na CCM zanzibar vyama vingine vikawapongeza ikiwemo chadema.

Kwanini leo wao wanataka kuipangia chadema chama cha kushirikiana nacho, Hii ni aibu kwa chadema.

Kama CUF si wabinafsi mbona zanzibar hawakushirikisha chama hata kimoja.

Mimi nafikiri tumeichagua Chadema kwa zaidi ya kura mil. 2 kwahiyo wanahaki ya kujipangia mambo yao kwa maslahi ya wananch na si kwa maslahi ya CUF kama ambavyo CUF inataka.

Kwanza CUF ni Chama cha Zanzibar kwahiyo huku bara hatuitambui hata kidogo, na Wabunge wengi wa CUF ni mamluki wanaotumwa na CCM hatuna imani nao.

Peoples Powe
r
 
na la mwisho ambalo hata na mm ningependa kujua kua Chadema imewakwaza viongozi wakuu wa NCCR na CUF kivipi ?

Mkuu ishu ya Kawe kule kipindi cha uchaguzi.

Mwenyekiti wa NCCR aliambiwa anabana mno pua na kulegeza vidole ndo ugomvi mkubwa
 
hapa ndipo ninawasifu CCM just like Kenya ili kuiua KANU kibaki na raila wamewaingiza serikalini. In few years, KANU will be no more. uchaguzi ujao CUF itakuwa kama UPDP.
 
Nimecheka sana, Yaani sasa malengo ya CUF yanaanza kuwa crystal clear. Yaani CUF ndo wanawaonya Chadema kuwa kuna madhara ya kutomtambua rais aliyetangazwa na tume? CUF ambao wamemkataa karume kule Zanzibar hadi juzi juzi tu baada ya kurushiwa peremende? Sasa CUF wanaanza rasmi kuifanya kazi ya CCM ya kuishauri Chadema imtambue rais!!

Sasa iwe wazi, kwa wale wote waliokuwa wakiamini kuwa CUF inaweza ikawa mpinzani bara wakati Zanzibar wako serikalini, kuwa hilo halipo. Na anayesema CUF na Chadema wanaweza kuunda kambi ya upinzani haitakii mema kambi hiyo na pengine haoni haja ya kuwa na kambi ya upinzani. Na kusema kweli ni CCM pekee anayeweza kuona hilo la CUF kuungana na Chadema kwenye kambi ya upinzani ni jambo jema.

CUF walikuwa wanashirikishwa. Sasa huo usemaji wa vyama vingine CUF wamepewa lini? Yaani CUF wanaambiwa karibuni tuunde kambi ya upinzani, lakini wao wanasema ili sisi tuje inabidi na NCCR, UDP na TLP wawemo!! Si TLP, UDP wala NCCR waliokwishasema kuwa wanataka kuingia kwenye hiyo kambi. Sasa CUF wamepataje hiyo 'authority' ya kuvisemea hivyo vyama vingine??

CUF ni moja na CCM ni moja, kule Zanzibar na huku bara pia! Ni kujilisha upepo kuamini kuwa CUF na CCM sasa hivi watatofautiana kwa lolote, nasema ni kujilisha upepo. Sasa hivi wao, lao moja, nalo ni kuona kuwa ajenda za serikali zao zinapita bila kupigiwa kelele na yeyote.

I Think CHADEMA is now officially own its own.
Vyama vingine vyote Gagali
 
aliyekuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni katika bunge lililopita, hamad rashid mohamed amewashambulia viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) kwa kuwataka wawe na msimamo na wafanye uamuzi kisiasa kama watu wazima.

Hamad amewatuhumu chadema kuwa wabaguzi kwa kuwa walitaka kushirikiana na chama cha wananchi (cuf) kuunda kambi hiyo lakini walidhamiria kuvitenga vyama vingine ya upinzani.

Mbunge huyo wa wawi (cuf) alimewaeleza waandishi wa habari mjini dodoma kuwa, wao (cuf) hawana shida ya vyeo kwa kuwa waliwahi kuwa na madaraka makubwa kuliko ya kwenye hiyo kambi ya upinzani bungeni.

Amewataka viongozi wa chadema wawe ‘matured’ na watambue pia gharama za kisiasa za kutomtambua rais jakaya kikwete.

Kwa mujibu wa hamad, cuf wana msimamo, waliwahi kufanya uamuzi mgumu na wakautekeleza hivyo chadema wajifunze kwao (cuf).

Alisema, mwenyekiti wa chadema, freeman mbowe, alimfuata akamueleza nia ya kushirikiana na cuf kuunda kambi ya upinzani bungeni lakini kwa kuvitenga vyama vingine vyenye wabunge katika bunge hilo.

Hamad amesema, alikataa wazo la mbowe na akampa ushauri ambao hadi sasa hajautekeleza.

Mwanasiasa huyo amesema, cuf wanataka kambi ya upinzani bungeni ushirikishe vyama vyote vya upinzani, chadema hawataki.

Hamad amesema, viongozi wa chadema wamemkwaza mwenyekiti wa nccr mageuzi, james mbatia na mwenyekiti wa cuf, profesa ibrahim lipumba, hivyo waende wakazungumze nao wayamalize.

Source: Basil msongo,habarileo ,dodoma; tarehe: 18th november 2010

cuf wanamimba ya makamba na watazaa karibuni
 
Jamani naombeni niwakumbushe tena maneno ambayo yamekuwa yakisemwa na Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA. Amekuwa anasema kwamba ....SUALA LA KUUNGANA KAMA WAPINZANI LITATEGEMEA KAMA MALENGO YENU YANAFANANA... MNAWEZA KUWA WOTE NI WAPINZANI, LAKINI MKAWA NA MALENGO TOFAUTI... Pia amekuwa akisema kuwa ....TUKO TAYARI KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHOCHOTE CHA UPINZANI CHENYE NIA YA DHATI KUUNDA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI.

Sasa ndgu zangu mnaosema CHADEMA wanatakiwa kuunda kambi ya upinzani na vyama vingine, nambieni kati ya hivi vyama vingine, kipi kina qualify, kwa kuwa na nia ya dhati na malengo sawa na CHADEMA?

Kama mmekuwa mnawasikiliza CUF mwaka huu mtagundua malengo yao ni tofauti sana na CHADEMA. Akijitoa katika kugombea unaibu spika juzi, Bw Mnyaa wa CUF alisema dhahiri kuwa ...nia ya CUF kwa sasa ni kujenga umoja na kuimarisha ushirikiano wa kitaifa (akimaanisha kuimarisha ushirikiano na Serikali)...

Malengo ya CHADEMA ni kujenga sera na kuonyesha mwelekeo wenye matumaini ya taifa, na kuiwezesha kuchukua dola siku za mbeleni. Haina kabisa malengo ya kuungana na serikali ya kifisadi ya CCM...

CHADEMA bado na hawatakaa wanyooshe mikono kusalimu amri mbele ya CCM kama walivyo CUF...

CUF sio wapinzani tena, bali ni washirika wa serikali katika CCM...
 
Ndugu zangu waJF, kauli ya Hamadi siishangai. Hamadi anajua fika kuwa mambo ya private huwezi kuyaongea hadharani, wala mambo ya hiari huwezi kuyalazimisha, lakini mnajua ni kwa nini anafanya haya? Mimi naamini kuwa cuf sasa hivi ni ccm B, baada ya kuungana na ccm na kumegewa keki ya mgawo wa madaraka hawawezi tena kuipinga. Wako meza moja, lao ni moja. Ni vyema tukaelewa kuwa cuf kiliacha kuwa chama cha upinzani rasmi kilipoungana na ccm. Anachofanya Hamadi ni kukihujumu CHADEMA kwa makusudi, sio kwamba hajui, na ndio sababu gazeti la ccm ndilo lililoripoti hayo.

Lakini baya zaidi ni kwamba, kwa muungano huo, sasa ccm ina nafasi ya kuwatumia cuf kujaribu kukidhoofisha CHADEMA machoni mwa jamii. Mambo mengine cuf itakayokuwa inawafanyia CHADEMA fahamuni yanafanywa na ccm, cuf ni puppet tu. Mmesahau ccm ni bingwa wa propaganda? Miaka mitano hii cuf itatumika sana dhidi ya CHADEMA, la msingi CHADEMA na jamii wajifunze kusoma btw the lines, na kuwapuuza.

Lingine la kujikumbusha ni kuwa kambi yoyote ili kweli iwe kambi ni lazima wanakambi wawe wamoja. Kama hakuna umoja wa dhati hiyo siyo kambi. Cuf wameonesha dhahiri kuwa hawako pamoja na CHADEMA, hivyo hata kama wakikaribishwa kwenye kambi rasmi ya upinzani watakuwa virusi wa kuharibu mipango ya upinzani bungeni. Upo usemi wa kweli usemao, "wawili hawawezi kwenda pamoja wasipopatana." Cuf ni wa kuogopwa kama ukoma sasa hivi, kujiunga nao ni kujiunga na ccm. Tunataka umoja wa kweli, sio umoja na virusi. Virusi wakiruhusiwa ndani ya CHADEMA wataimaliza. Tujue sasa hivi hata Zanzibar hakuna tena upinzani imara. Tuukubali tu ukweli kuwa chama cha upinzani chenye nguvu sasa hivi ni kimoja, CHADEMA.
 
Maadam wameshindwa kushirikiana wakati wa uchaguzi basi hata bungeni hawataweza...
 
Jamani kama CUF sio wabinafsi ilikuwaje wakafanya mwafaka bila kushirikisha wapinzani wengine?

Kwanini ni wao tu wanajiona wako sahihi kila siku, ile hali wao wamekubali kuungana na CCM zanzibar vyama vingine vikawapongeza ikiwemo chadema.

Kwanini leo wao wanataka kuipangia chadema chama cha kushirikiana nacho, Hii ni aibu kwa chadema.

Hicho hasa ndiyo chenyewe. CUF waeleze wazi kuwa siyo wapinzani tena. Watuambie wanampinga nani maana kule Zanzibar wameungana na CCM na pengine huu mwafaka unahusu Serikali ya Muungano.

Kama CUF si wabinafsi mbona zanzibar hawakushirikisha chama hata kimoja.

Mimi nafikiri tumeichagua Chadema kwa zaidi ya kura mil. 2 kwahiyo wanahaki ya kujipangia mambo yao kwa maslahi ya wananch na si kwa maslahi ya CUF kama ambavyo CUF inataka.

Kwanza CUF ni Chama cha Zanzibar kwahiyo huku bara hatuitambui hata kidogo, na Wabunge wengi wa CUF ni mamluki wanaotumwa na CCM hatuna imani nao.

Peoples Powe
r

Hicho ndicho chenyewe. CUF siyo wapinzani tena. Kama ni wapinzani wanampinga nani maana kule Zanzibar wameungana na CCM na huu ndio mkakati wao kwenye Serikali ya Muungano
 
Kwa mara ya kwanza naaanza kuona madhara ya serikali ya umoja wa kitaifa ZNZ. Hamad lazima aseme wazi maamuzi yake yanatokana na nini.

TLP ya Mrema si kambi ya upinzani kwa sababu zilizo wazi. NCCR ya Mbatia imewafungulia kesi CHADEMA hata kabla kambi haijaundwa.

UDP ya Chey alishafuatwa huko nyuma juu ya kuvishirikisha chama akaingia mitini.

CUF na CCM wana ndoa.

CHADEMA go, goo gooo, achana nao. with time it will pay. Hoja zenu zitalipa. Bunge lililopita linasifika kwa kuwa nyie ndo mliibua kashfa na si CUF ambao walikuwa luluki bungeni tena wote toka Zanzibar.

Give us a break.

QED
 
hawa CUF tangu wapate mwanaume wa kuwalea sasa wanaboa
ndoa yenyewe haina mwisho mzuri, huyo ccm sio mtu wa kukaa
nao ukasema uko salama, kweli CUF sasa ni kama
lap top
 
Back
Top Bottom