Ukweli unabaki pale pale kuwa Lipumba aje na kujibu kwanini hawana mbunge hata mmoja?? Je ni kwanini ameshindwa kuongoza Chama hicho na mikakati Imara?? Je ni kwanini ameshindwa au kupunguza idadi ya Madiwani toka mwaka 200-2005, ukilinganisha kwa makini na minendo ya vyama hapa Tanzania utaona umarufu wa CUF umepungua sana
Kama ambavyo ukweli unabaki kuwa umeli ongopea jamvi
ha ha ha komini hivi hadhi ya CUF kuwa CCM -B iliisha lini au humu jamvini munabatiza majina kutegemea nyakatikama Lipumba amekuwa PUMBA ajiuze kwa wauza komoni, maana amekosa cha kusema. tena yeye ni fisadi mbaya zaidi anapandikiza chuki kwa watoto wetu wakati anakula hela ya serikali na CCM pia. yawezekana CUF nayo ni CCM-C
Siwezi na sijawahi kutumiwa na chama chochote cha siasa ikiwamo hiyo CCM. Nafahamu unajua hata CUF haijawahi kunitumia na hata pale nilipofanya kazi za CUF, CCM, Chedema, NCCR-Mageuzi, TLP, TADEA, nilifanya hivyo ikiwa ni sehemu ya majukumu yangu ya kawaida. Hivyo ndivyo ilivyo JF. Hoja za msingi ni kwa CUF kusafisha hizo kelele kuhusiana na matatizo ya ndani ambayo si vyema yakatumika kukichafua. Najua maneno ya ufadhili yamekera lakini nimegusia nikijua mulio ndani mutaelewa na kusafisha hizo tuhuma ikiwa ni pamoja na zile za mpakani.
Quote:
[/B] Mkuu Halisi..
siku nyingi una maneno kama haya,na niliwahi kujibu matamshi yako,the way ulivo na maneno yako ni tofauti kabisa.. tatizo lako na mafisadi limalize mwenyewe,sijui niseme ni miongoni mwa watu wanaotumiliwa na ccm kukipakazia Cuf kama walivofanya nyuma,walivokuwa wakipakazia ni chama cha udini,cha warabu na mengineo sasa unaleta propaganda nyengine..sawa mkuu wasaidie hao ccm,lkn huna ushahidi na unaloongea.. lkn kaka yangu siko unapokwenda,rudi kwa Mola wako...[/I]
Kimsingi CUF ikijipanga inaweza lakini ijiepushe sana na watu wanaojifanya kuwa ni wema kwao, hasa wale wenye mikono michafu na umekiri mwenyewe kwa kusema, "tatizo lako na mafisadi limalize mwenyewe", pamoja na kufumba kwako, najua umelenga nini na hii inanitia faraja kwamba umenielewa. Bila kusema hatuwezi kujirekebisha na bila CUF yenye nguvu hakutakuwa na mageuzi ya kweli katika nchi hii. CCM imekuwa makini sana kupenyeza agenda za kuua nguvu za upinzani. Wametumia mbinu za kubeba ajenda ya ufisadi ya kina Dk SLaa na Hamad Rashid, wameibua hoja ya kujifanya Bunge la wabunge wengi wa CCM lina nguvu, yote ni kupoteza mwelekeo kabla ya 2010 na kuwanyang'anya hoja wapinzani. Huko Zanzibar nako wameibuka na kubeba hoja ya mafuta ambayo Maalim Seif amekuwa akiimba miaka yote, leo imekuwa hoja ya Karume na shemeji yake Mansoor na CUF wanashangilia. Lazima muamke.
Kama ulivyosema "mafisadi ni tatizo langu" ikiwa na maana ya kuwa halikuhusu, narudi tena kwenye hoja yangu ya pili kwamba CUF isipopima upepo unavyokwenda itaendelea kupoteza mwelekeo na labda iwekeze kuelekea 2015 ama 2020 na si 2010.
Kumbukeni niliyowahi kusema kuhusu "Operesheni ZInduka ya CUF" kuhusiana na jinsi watakavyoipeleka. Wameanza vyema na sasa tumeona Lipumba ameanza kumsafisha Lowassa kama ambavyo aliwahi kumtetea Rostam. Inawezekana isionekane hivyo lakini kwa kusema kwamba uamuzi wa Richmond ni wa Baraza la Mawaziri lote chini ya Kikwete ambaye naye aliridhi, ina maana sasa Lowassa alionewa> Hata kama ni kweli (jambo ambalo siamini) kisiasa si CUF wa kuliweka hilo. Wangejiepusha nalo. Itachukua muda (si 2010) kwa wananchi (wapiga kura) kuwaelewa CUF kwa kuibua suala la Richmond kwa staili yao. TAFAKARI
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/33226-ujumbe-kwa-salim-dimani-wa-cuf.html
Re: Ujumbe kwa salim dimani wa cuf
Quote:
Iliunga mkono TLP na Opresheni ZInduka inakejeli "kulipua mabomu ya ufisadi", jambo ambalo ndio nguzo ya sasa ya Chadema na baadhi ya wana CCM, mkakati uliopata uungwaji mkono mkubwa wa umma. Sasa CUF kwa kuungana na TLP na NCCR Mageuzi katika chaguzi ndogo zilizopita wako sahihi? na je, wataing'oa CCM kuelekea 2010 ama ni mkakati wa 2020?
Tune ya TOT hiyo!!Hah ha ha ha ha
Nani alikwambia wapinzani wanatafuta kuing'oa ccm ? Hapo umenowa mkuu ,wapo pale kwa masilahi binafsi, kwa dhamila ile ile ,mlengo ulele,nia ile ile ,sababu zile zile,hamu ile ile na uwezo ule ule
Hawana kabisa mpango huo na pia sasa wamebaki na majungu yasio na maana yoyote ileNimezinduka, CUF hawana mpango tena wa kushika dola ndo maana wameacha kupambana CCM na badala yake wanaelekeza mapambano kwa CHADEMA.
Kweli na ndo mana,chadema waliwahi kumfata Mustapha wandwi wa cuf wakampa na pesa ili aingie chadema, kweli kabisa maneno yako,na ndo mana chadema wakabambwa live wakiongea na Lwakatare ktk hoteli moja kubwa,wakati huo Lwakatare bado ni naibu katibu mkuu wa cuf,kweli maneno yako,ndo mana chadema wakaenda kufunga matawi ya cuf kule bukoba. he! bado cuf wakae tu wanyamaze, kweli maneno yako,ndo mana cuf walikuwa wanawaachia baadhi ya majimbo chadema lkn walipotaka kusimamisha wao cuf,chadema wakawajibu UPEPO UMEBADILIKA. Duh! kumbe cuf imevumilia saana. sasa sijui nani yupo kwa ajili ya mwenzake,akili kichwani mwako....Nimezinduka, CUF hawana mpango tena wa kushika dola ndo maana wameacha kupambana CCM na badala yake wanaelekeza mapambano kwa CHADEMA.
Chadema bila ushirikiano na vyama vingine mjue mta-angukia pua katika uchaguzi ujao.
Mwaka 2000, Chaguzi zote za kule Zanzibar na kila wakati walikuwa karibu sana katika siasa za Tanzania lakini CUF walikuwa hawaoni haya na sasa baada ya CHADEMA kuchukua uhalisi wakeWashirikiane na vyama vipi? CUF au?
Siku zote ambapo CUF wamekuwa wakiungwa mkono na CHADEMA hawakufahamu kuwa ni chama cha mafisadi, leo baada ya kuona mwendo unashika kasi ndio wanafanya uvumbuzi wa Mzungu kuvumbua mlima Kilimanjaro!
Siku zote naamini ushirikiano wa vyama hauwezi kuleta tija. Kinachowezekana na kuvivunja na kujenga chama kimoja, vinginevyo, hao waliovianzisha walikuwa na malengo na misingi ambayo daima haiwezi kuvifanya vitengemae katika ushirikiano!
Kweli na ndo mana,chadema waliwahi kumfata Mustapha wandwi wa cuf wakampa na pesa ili aingie chadema, kweli kabisa maneno yako,na ndo mana chadema wakabambwa live wakiongea na Lwakatare ktk hoteli moja kubwa,wakati huo Lwakatare bado ni naibu katibu mkuu wa cuf,kweli maneno yako,ndo mana chadema wakaenda kufunga matawi ya cuf kule bukoba. he! bado cuf wakae tu wanyamaze, kweli maneno yako,ndo mana cuf walikuwa wanawaachia baadhi ya majimbo chadema lkn walipotaka kusimamisha wao cuf,chadema wakawajibu UPEPO UMEBADILIKA. Duh! kumbe cuf imevumilia saana. sasa sijui nani yupo kwa ajili ya mwenzake,akili kichwani mwako....