Sethshalom
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 581
- 1,000
Kuna kitu tunastahili kujua ,Serekali ya Cuba na chama chao vilianzishwa na watu ambao walikua na maono na uchungu wa nchi yao. Kumbuka barua ambazo alikua anamwandikia mama yake alipotembelea Southern America kuhusu Maisha ya watu na alivyojitolea kuwa anawatibu for free. Castro alikua na maono kuhusu Maisha gani anataka kuwapa ndugu zake. Hawakua motivated na hela wala utajiri lakin utajiri wa nchi kwa ujumla. Ndio maana walipokamata nchi waliweka educational policies kwamba mwananchi anahitaji wa kumfundisha kulima vizuri, Dkt wa kumtibu akiumwa na mwalimu wa kufundisha watoto wake. Haihitaji sana mwanasheria , social work au mtu aliesoma political science... Ndio maana wakaweka msisitizo kwenye elimu ya science. Lakin kila kitu huanzia jutaChe Guevara alikua anafanyaje kazi au Castro mwenyewe?? Ni viongozi wangapi Africa wanaweza kufanya kazi hivo. Wanaoweza wananyimwa nafasi au wanabezwa au wanauawa. In 2007 nilifanikiwa kukaa siku kama 7 na jamaa wa Trinidad and Tobago, alikaa Cuba anasema ndio nchi aliona haikua na wezi vibaka au makahaba, na kila mfanyakazi alipata his fair share na kila mtu anafanya kazi kwa ajili ya taifa na si kwa ajali yake maana nahitaji yake mengine taifa litamfanyia. So kama viongozi wanataka utajiri binafsi kuliko utajiri wa taifa, hakuna utaratibu wa taifa kujali watu wake hata wale waliojitolea Maisha kulitetea wakati wa nahitaji msaada...huo moyo wa ubunifu na kuumiza vichwa utatoka wapi?? Hii ni Africa kwa ujumla.Cuba njaa sana daktari2 analipwa dola 100kwa mwezi
Kuhusu malipo madogo, standard of life kwao ziko hivo hiyo unayoita ndogo kwao nyingi, kumbuka education Cuba is free kuanzia kindergarten to PhD. So kuna reforms nyingi zinahitajika mpaka Africa tufike hapo