CTI Kutumika kukodisha Majenereta ya DOWANS: Fikra Pevu


If you go out of your way kutafuta mchawi huwezi kumkosa. But does it worth it? We care if there is umeme na taifa halihujumiwi. If you can show me how CTI kununua mitambo ya Dowans taifa linahujumiwa then tutaelewana. Tatizo ni conspiracy na paranoia (part of it is serikali to blame) that folks are not using their common sense kupembenua kati ya mchele na pumba.

The notion that we have been discussing about Dowans since 2006 bila suluhu inaonesha tusivyokuwa serious. The society, her people, and her institutions have failed. It sounds like Dowans is the only problem with this country, and that shows our smallness. Sometimes, u get a picture that if Rostam Aziz die today then Tanzania will be the highest economy in the world. That proves our smallness. And we blame opposition for that. Chadema thinks the path to maendeleo is getting rid of Rostam and that narrows the debate humu ndani on other means to alleviate poverty.
 
Habari za kuaminika toka ndani kabisa (ka nzi).........................


Penye red huwa na kutana na hilo neno lakini sielewi maana yake hivyo huwa nasita kidogo kuchangia kitu ambacho sijakielewa, na nimefanya juhudi kulijua kabla sijaomba msaada lakini nimefeli. Naomba msaada kujua nini maana ya (ka nzi)
 

You said it Selemani; it is more to do with fanatism than objective analysis. Akiondoka Rostam na Dowans yake atatafutwa mchawi mwingine na mchezo unaendelea.

Hapo ndipo walipotufikisha wanasiasa wetu, siasa za kulipua mabomu/skandali na wala hazijaanza leo na akina Chadema, zimekuwepo tangia miaka ya mwanzo ya mageuzi, wakati mwingine nafikiria labda tunachezewa kufuata agenda ambayo is likely to expire then we start again at the borrom!
 

You still dont get it dude. Who is Rostam after all and what hole did he crawl out of ? Our war is not with Rostam but with the system, the system that lets filthy rats like Rostam roam our streets with impunity plundering everything that crosses their path. Our war is with sycophants and traitors the type of Selemani and Majimshindo, who would rather look the other way as their masters tear and destroy the fabrics that hold us together as one country.

The bottom line is that as long as Tanzania remains a haven for thieves, drug traffickers, con men and what have you, we are dead though we continue to live !
 
Huku ni kuleta propaganda kwenye masuala ya maendeleo ya nchi. Ni upumbavu kila wakati kufikiria kwamba kila uamuzi unalenga uchaguzi wa mwaka 2015. Inaonyesha kuna watu wanaweweseka na uchaguzi wa mwaka 2015 na kudhani kwamba kila mtu akili yake ni huko huko. Ni upumbavu kwa sababu haiwezekani kila mradi wa maendeleo unaofikiriwa basi kuna watu wanataka ulaji. Kuna watu tunaendeshwa na fikra za kutenda na kupata matokeo ya kutenda. Haiwezekani tuwe watu wa kuzungumza tu kila siku.

I have no connection whatsover with RA na EL kwenye Urais au mpango wowote wa kisiasa. I say this loud and clear. I am not supporting anybody. I, myself, am ambitious. Siwezi kuingia kwenye miradi ya watu kutaka Urais kwani wote mnaowataja na kuwaunga mkono au kuwapinga naona hawana uwezo wa kuongoza Taifa hili.

Usinifanyie propaganda za kijinga. Ninafanya kazi yangu kwa mujibu wa kanuni za Bunge. Sasa kama unataka niwe mwenyekiti posho, kukaa bila kutoa masuluhisho ya maendeleo ya nchi, go and hang yourself. I am not like that. I am action oriented. Call me arrogant or whatever the names, i am different. Mark my words! Acha propaganda kwenye maendeleo ya nchi.

NSSF
Sitafuti support ya mtu yeyote yule. Hoja za NSSF kukabidhiwa Kiwira nimeziweka wazi. Wala sijajificha kama wewe unavyotumia pen name hapa kwa unafiki wako. NSSF wameikopesha sana TANESCO. NSSF wana haki ya kuwekeza kwenye jambo lolote litakaloleta faida kwa mfuko. Hoja zako za kitoto eti why not TANESCO. Mbona Ngaka na Mchuchuma watakaozalisha umeme ni NDC? Nao tuwatoe tuwape TANESCO? Hayo ni mawazo mgando. It is stupidity to stay out there and wait for people to come with solutions and start criticising the solutions. It is even more stupid to link every initiative in Tanzania with Rostam Aziz! Who is Rostam Aziz anyway to be linked to everything. This is cheap propaganda. Yeye amekuwa Pweza anajitandaza kila mahala?

Tuogope kufanya maamuzi kwa kuwa atahusishwa Rostam Aziz? Acha upuuzi.

Kwamba Caspian watapewa tender ya kuchimba makaa. Huu ni upuuzi tu ili kujenga chuki na fikra hasi za initiative ya kuhakikisha Kiwira inafufuliwa. I dont care nani atachimba makaa pale. What i care ni kuona Kiwira inafufuka, makaa yanachimbwa na umeme unazalishwa. Hizi mbinu za kuhusisha makampuni yanayomilikiwa na watu wenye mawaa ya ufisadi na miradi ili ikwame ni mbinu za kitoto, za kijinga na za kipuuzi.

Hizi ni propaganda za kishenzi kabisa!

On my agenda - moja mchuchuma na Liganga miradi ianze. Mbili, Ngaka coal fields mradi uanze. Tatu, Kiwira ifufuliwe. Nitahakikisha kwa kupitia kamati yangu tunawezesha NDC na NSSF wanatekeleza miradi hii na kuliondoa taifa kwenye tatizo la umeme katika muda wa kati.

I dont care about the next election. I do about the next generation.

Endelea kumwaga sumu zako. Sibabaiki. I do the right thing and inshaallaah i will succeed for the benefit of my country!
 

The fabrics of our society is dialogue, not monologue. Respect for our those who we disagree and prevailance of common sense. We have become a society that embrace the loudest politicians who are also populists. We can not solve our problems because the politicians and we the people are tied down into minute details. Issue ya Dowans could have been solved if Bunge la Sitta lingeacha siasa na kufanya maamuzi magumu. But today they are hailed as wakombozi.

Tanzania system is not clean, our society by itself is not clean. You can't find me 100 Tanzanians who have never ask or receive rushwa. There is an entire class of bureaucratic entrepreneurs out there--mid-level government officials who are stealing our monies kila siku. And those are the same guys wanalalamika kuhusu ufisadi. My point is, hauwezi kuzuia safari kwa sababu abiria mmoja hajalipa nauli. Tanzania has tons of problems, and Dowans is just a small, small ishu. Wanasiasa waache kutuchezea and fix it, so as we can move on to fix education, inflation, barabara na mambo mengine kibao.

Hatuwezi kukaa miaka 5 tunaongelea Dowans tu. Ni nchi gani sisi?
 

Wapi Moelex23 kasema kuwa Caspian wamesign mkataba na NSSF/TANESCO?

Tupe matokeo ya utafiti uliofanya kuwa Tanzania tunapoteza billions (dollar? shillings?, kuku?)

Heshimu mawazo mbadala kuliko kumwambia mtu kuwa ana bwabaja, au you can't even think
 
Asante sana mh,ZITTO,Kwa mawazo yako mazuri, lakini mh, huoni ni kututesa watz,nssf wazalishe wauze tanesco,tanesco watuuzie sisi,kama Nssf wanaweza kuzalisha, kwa nini wasizalishe na kuuza moja kwa moja kwetu?

Kwa nini Tanesco awe kama dalali? Tutafute mashirika pinzani na Tanesco, ndiyo tutaweza kuondoa tatizo la umeme Tz, kinyume na hapo hadithi
 


Mkuu Zitto hebu kidogo jikumbushe hatari ya RA then usiseme hujali nani atachimba!

Hoja ya Rostam Bungeni hii



Na Mwandishi wetu - Imechapwa 29 April 2008

Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipatia nafasi hii ya kuzungumza mbele ya Bunge lako tukufu ili niweze kutoa maelezo na vielelezo kuthibitisha hoja nilizotoa katika mchango wangu wa maandishi nilioutoa katika kikao kilichopita cha Bunge wakati wa mjadala wa Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura ulioipa ushindi "Richmond Development Company LLC" ya Houston, Texas Marekani mwaka 2006.

Mheshimiwa Spika, wakati akifungua mjadala wa hoja hiyo, Mwenyekiti wa Kamati Teule, Mheshimiwa Dr. Harrison Mwakyembe, siyo tu alinitaka nithibitishe hoja yangu kwamba Kamati Teule hiyo ilikuwa inaendelea kumalizia kazi zake hadi wiki ya kwanza ya kikao kilichopita cha Bunge lakini pia aligusia maeneo kadhaa ya ripoti ambayo yananihusu.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa uniruhusu nitoe maelezo ya kina pamoja na ushahidi wa vielelezo kuhusiana na masuala hayo yote aliyoyazungumzia Mheshimiwa Mwakyembe ili Bunge hili na Watanzania kwa ujumla waujue ukweli, tena ukweli kamili kuhusiana na suala hili.

Mheshimiwa Spika, nianze na hoja ya hati ya wito wa kunitaka nifike mbele ya Kamati Teule kutoa ushahidi.

Ni lazima nikiri nimesikitishwa sana ingawa sikushangazwa na maelezo marefu ya Mheshimimiwa Mwakyembe aliyoyatoa kueleza jinsi hati ya wito ilivyofikishwa nyumbani kwangu Oysterbay na kupokewa kwa dispatch na mtu aliyedaiwa kuwa ni ndugu yangu.

Sikuona umuhimu wala haja ya maelezo hayo kwa sababu katika mchango wangu wa maandishi nilioutoa katika mjadala ule, hakuna sehemu yoyote niliyosema kuwa hati ya kiapo haikufikishwa nyumbani kwangu tarehe waliyoitaja.

Kwa hivyo, ule utungo mrefu wa kufikia kulieleza Bunge lako kwamba Kamati Teule ina hata hati ya kiapo ya mtumishi wa Bunge aliyefikisha summons (wito) hiyo nyumbani kwangu ilikuwa na muendelezo tu wa kipaji cha usanii cha Mheshimiwa Mwakyembe.

Mheshimiwa Spika, nilichosema mimi, na ambacho Mheshimiwa Mwakyembe amekikariri vizuri katika maelezo yake, ni kuwa hati hiyo iliandikwa tarehe 24 Desemba, 2007 ikinitaka nifike mbele ya Kamati Teule tarehe 27 Desemba, 2007 na kwamba mazingira ya tarehe hizo ni magumu kwa barua kuwafikia walengwa kabla ya sikukuu kupita.

Mheshimiwa Spika, kupokelewa hati ya wito nyumbani kwangu ni suala moja na hati kunifikia mimi ni suala jengine.

Sidhani kama Mheshimiwa Mwakyembe anapofikishiwa barua nyumbani kwake wakati yeye akiwa nje ya nchi, basi wanafamilia yake husafiri kumfuata aliko ili kumfikishia barua hiyo kwa hivyo, wala haikuwa ajabu kama Kamati Teule ilivyotaka ionekane kwa mimi kupokea barua hiyo baada ya kurejea kutoka safari yangu nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza katika mchango wangu wa maandishi, mimi nilikuwa nje ya nchi kuanzia tarehe 17 Desemba, 2007 hadi 3 Januari, 2008. Nawasilisha kwako nakala ya photocopy ya Paspoti yangu ikiwa na mihuri ya Idara ya Uhamiaji inayoonyesha kutoka na kurejea kwangu hapa nchini kama kielelezo kinachothibitisha maelezo yangu hayo.

Mheshimiwa Spika, naendelea kusisitiza kuwa Kamati haikuwa na nia ya kweli na ya dhati ya kutaka maelezo yangu maana kama ingetaka kufanya hivyo, ingeniita katika siku yoyote kabla ya Desemba 24, 2007. Lakini kwa kusubiri siku 7 tu kabla ya kumalizika kwa muda ambao walipaswa wawe wamekamilisha kazi yao, tena ikiwa ni kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka ambapo familia nyingi zisizo na kazi za serikali huchukua likizo, kunaonyesha wazi kuwa kulikuwa na malengo ya kutaka kuchafuana tu kwa kujua kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kutopatikana yule anayehitajika kutoa ushahidi. Iwapo Mheshimiwa Mwakyembe hapendi kuona nina siku za mapumziko, ni bahati mbaya sana kuwa mimi sina cha kumsaidia katika hilo.

Mheshimiwa Spika, narudia kusema kwamba kama Kamati Teule ilikuwa na nia ya dhati ya kutaka maelezo yangu basi wangeweza kufanya hivyo hata baada ya mimi kurejea kwa sababu kama nitakavyothibitisha kwa ushahidi Kamati iliendelea na kazi hadi baada ya Desemba 31, 2007.

Mheshimiwa Spika, kabla ya kuliingilia hilo, napenda pia nieleze ukweli kuhusu hoja nyingine ambazo Mheshimiwa Mwakyembe alijaribu kuzipotosha akitumia usanii wake wa kuwasilisha na kujibu hoja. Nianze na ile inayohusu kuitafutia Richmond kampuni ya ushauri ya uandishi wa habari (G&S Media Consultancy) ili Richmond iandikwe vizuri na vyombo vya habari Tanzania.

Mheshimiwa Spika, hoja hii inaonekana imeibuliwa kutokana na ushahidi wa Ndugu Salva Rweyemamu alioutoa mbele ya Kamati Teule. Nimepata nafasi ya kupitia Hansard za Bunge zinazohusu shughuli za Kamati Teule na nilichokiona ni kuwa Ndugu Salva Rweyemamu mwenyewe hakuwa na uhakika wa kile alichokisema pale alipoulizwa juu ya nani aliyemtambulisha kwa kampuni ya Richmond na yeye akajibu, "Nadhani ni rafiki yangu Rostam Aziz".

Mheshimiwa Spika, ni juu ya Ndugu Salva mwenyewe kuweka sawa kumbukumbu zake na kujua kwa uhakika ni nani aliyemtambulisha na Richmond badala ya kusema "anadhani". Inawezekana kama binadamu alichanganya mambo kwani mimi sikuwahi kumtambulisha kwa Richmond, maana mimi mwenyewe siwajui hao akina Richmond hata niweze kuwatambulisha kwa mtu mwingine. Mimi nilimtambulisha Ndugu Salva kwa kampuni ya FFT inayoshughulika na utoaji wa mizigo bandarini (clearing and forwarding) ambayo ndiyo ninayoitumia katika shughuli za kibiashara za kampuni zangu ili kuweza kujitangaza yaani kufanya promotion. Kuthibitisha hilo, nawasilisha mbele ya Bunge lako hati ya kiapo, affidavit ya Ndugu Hassan Dhala, mmiliki wa kampuni ya FFT, ambayo imesainiwa na kamishna wa viapo inayobainisha ukweli huu.

Mheshimiwa Spika, hoja ya pili ambayo mheshimiwa Mwakyembe katika maelezo yake alisema Kamati Teule ilitaka nieleze ni ile inayohusu uhusiano kati ya kampuni yangu ya Caspian na kampuni ya Dowans. Kamati Teule imehoji kwanini barua pepe na anuani ya posta ya kampuni yangu ya Caspian pia ilitumiwa na Dowans na kwamba baadhi ya wafanyakazi wa Caspian wanadaiwa, naomba nirejee wanadaiwa, kuifanyia kazi pia Dowans.

Mheshimiwa Spika, kabla ya kuzijibu hoja hizo, napenda nimfahamishe mheshimiwa Mwakyembe kuwa mimi, tofauti na labda alivyo yeye, sina wapambe eti wa kunisimulia yaliyoandikwa katika Ripoti ya Kamati Teule aliyoiongoza. Nataka nimhakikishie kuwa nimesoma ukarusa hadi ukurasa wa ripoti waliyoiandaa pamoja na kwamba haikuwa kazi nyepesi ukitilia maanani kwamba ripoti hiyo imepotosha na kupindisha mno hoja zinazohusu masuala ya fedha, uchumi na biashara.

Mheshimiwa Spika, hakuna hata mfanyakazi mmoja wa Caspian anayeifanyia kazi Dowans. Isipokuwa narejea tena maelezo niliyoyatoa katika mchango wangu kwamba watumishi wa kampuni yangu wanaweza kushirikiana na kampuni yoyoye ambayo kampuni yetu ina nia ya kufanya nayo biashara. Na hilo lilifanyika kama ambavyo pia ni kweli kuwa kampuni ya Caspian ambayo mimi ni Mwenyekiti wake iliruhusu Dowans kutumia anuani ya posta na barua pepe yake kwa sababu tulikuwa tunatarajia kupata kazi ya ukandarasi wa ujenzi kutoka kwao, ambayo ndiyo biashara kuu ya kampuni ya Caspian.

Mheshimiwa Spika, hiki si kioja kama ambavyo Mheshimiwa Mwakyembe na Kamati Teule alitaka ionekane. Ni taratibu za kawaida kabisa katika shughuli za biashara kuwa na kitu kinachoitwa "hospitality arrangement" yaani kupeana fursa za kutumia baadhi ya huduma baina ya kampuni zinazokusudia kufanya biashara au kupeana kazi. Hili linaweza likaonekana ni jambo kubwa la kuzua maswali kwa watu wasio na uelewa wa uendeshaji biashara lakini ni jambo la kawaida kabisa katika ulimwengu wa ushindani wa kibiashara ambapo kila kampuni inatafuta kandarasi kutoka kwa mwenzake.

Mheshimiwa Spika, kama ilivyoeleza kampuni yangu ya Caspian ni kampuni ya kandarasi ambayo huwa inatafuta kazi kwa kampuni nyingine zenye shughuli hizo. Caspian iliwasilisha zabuni ya kufanya kazi ya kandarasi ya ujenzi kwa ajili ya uwekaji wa mtambo wa General Electric 40MW LM6000 Gas Lurbine kwa Dowans ambayo hatukufanikiwa kuipata. Hata hivyo, tuliomba kazi nyingine ndogo ya kandarasi ya ujenzi wa ukuta wa uzio ambayo tulifanikiwa kuipata.

Nawasilisha mbele ya Bunge lako nakala za barua mbili kutoka Dowans kwenda kwa Caspian kuthibitisha haya, moja ya tarehe 10 Machi, 2007 ikitueleza kutofanikiwa kupata kazi tuliyoomba awali, na ya pili ya tarehe 25 Oktoba, 2007 ikitufahamisha kuwa zabuni yetu imefaulu.


Mheshimiwa Spika, aina ya kazi za ujenzi ambazo kutoka kwa Dowans tuna ujuzi nazo na tumejijengea jina zuri kwa jinsi tunavyozifanya. Tumewahi kufanya kazi kama hizo kwa ufanisi wa hali ya juu kwa kampuni ya WARTSILA ya Finland baada ya kushinda zabuni ya kimataifa. Nawasilisha kwako Mheshimiwa Spika, nakala za barua mbili (ya kwanza ya tarehe 31 Machi, 2008) kutoka kwa WARTSILA kwenda kwa Caspian kuthibitisha ukweli huu.

Mheshimiwa Spika, kwa taarifa ya Bunge lako tukufu, WARTSILA ni kampuni iliyosifiwa na Kamati Teule kwamba mradi wake ni wa kuigwa katika uzalishaji wa umeme hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, hayo ndiyo mahusiano ya kikazi kati ya Dowans na Caspian ambayo ni ya kawaida kabisa, yaliyofuata taratibu zote na yaliyofanyika kwa uwazi. Ni mahusiano ambayo kama Kamati Teule ingetaka kuyajua ingeweza kufanya hivyo. Hata hivyo, Kamati Teule iliamua kukwepa wajibu wa kuujua ukweli huu na badala yake ikaamua kuibua maswali yaliyoandaliwa kwa usanii mkubwa ili yatimize lengo lililokusudiwa la kutuchafulia majina baadhi yetu na pengine hata kuhujumu sifa njema za biashara tunazofanya.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuweka kumbukumbu sawa kuhusiana na hoja hizo zilizoibuliwa na Mheshimiwa Mwakyembe, sasa nijielekeze katika hoja ya msingi ambayo ndiyo hasa niliyotakiwa niithibitishe. Hii ni ile inayohusu hoja yangu kwamba Kamati Teule iliyochunguza mkataba wa Richmond iliendelea na kazi zake hata baada ya muda wa siku 45, yaani baada ya tarehe 31 Desemba, 2007, na mpaka wiki moja kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge na hivyo kama ilikuwa na nia thabiti ya kuupata ukweli kutoka kwangu ingeweza kufanya hivyo.

Mheshimiwa Spika, nimesikitishwa ingawa sikushangazwa na kitendo cha Mhe. Mwakyembe kujikakamua katika ukumbi mtukufu wa Bunge lako kwamba eti madai hayo ni uongo.

Mheshimiwa Spika, nina ushahidi wa hoja hiyo kwamba kamati iliendelea na kazi zake hadi baada ya muda iliyopangiwa kumalizika. Ushahidi huo nauwakilisha hapa mbele ya Bunge lako ili lione ni nani kati yangu na Mhe. Mwakyembe anayesema kweli.

Mheshimiwa Spika, sisi wengine hatuna kawaida ya kuja na mbwembwe nyingi za kujisifu hata kama ni kwa gharama ya kulipotosha Taifa na kuwapotosha wananchi. Tuna asili na rekodi ya kusema kweli, tena kweli tupu. Tunaamini katika kutenda na kutendewa uadilifu. Kwa hivyo, kila tunachokisema na kukitenda kina misingi yake. Leo hii, nimeona niwasaidie watanzania kupitia Bunge lako tukufu kuujua ukweli kamili ambao umejaribiwa kufichwa sana kwa malengo wanayoyajua wajumbe wa Kamati Teule.
 
Kwani CTI hii nayoijua si imesajiliwa kama shirikisho na sio kampuni sasa wana nguvu kisheria ya kufanya biashara zaidi ya ile iliyoainishwa kwenye Memo of Association yao,au na kuzalisha umeme ipo humo? Naomba nipate ufafanuzi tafadhari!

 
Hawa CTI si wanunue mitambo yao, halafu ndiyo wa negotiate na Tanesco kuuziwa umeme? Kwa nini wanang'ang'ana na Dowans? Hapo pana walakini!!!!!!!!1
 
Nimekumbuka hoja ya PM kuwa sio lazima Serikali inunue mitambo ya DOWANS bali hata watu ama kampuni binafsi zinaweza kununua mitambo hiyo pia..., inawezekana alikuwa anaweka mazingira kwenye mkondo tarajiwa!!!!
Mh....... Taff... Umeshawahi kuona mchezo wa karata tatu?
Matapeli wanakuweka kati wanajifanya hawajuwani kumbe wapo pamoja? Basi ndicho kinachoendelea sasa.
Ona hii story ya Mwananchi hapa chini.... eti "Mitambo ya Dowans yadaiwa kuuzwa nje" na huku huyo anayejiita Mkurugenzi wa Fedha wa Dowans (Tanzania), Stansalus Munai akijigamba "Mitambo yetu haijakosa soko. Wanaoihitaji ni wengi na ni wanaotaka kuisafirisha nje ya nchi." ...kisha anasema wako tayari kujadiliana na serikari kama wanataka kununua hii mitambo.....
Hawa matapeli target yao kubwa ni mitambo inunuliwe na serikali na hapa hili gazeti limetumika ku-create mazingira ya uharaka wa serikali kununua hii mitambo kwani tukichelewa chelewa itachukuliwa na wengine.... kitu amabacho sio kweli....
 
Nadhani inabidi tufikie "point" ya kukubali kuwa for whatever means at our disposal umeme upatikane haraka iwezekanavyo!

Hivi ile mitambo ya DOWANS/Richmond ndiyo tatizo au MIKATABA ndiyo tatizo?

Tunahitaji umeme, na kama mitambo ya DOWANS inaweza kuzalisha umeme na izalishe!

Wajasiriamali wa kati na chini wanaathirika vibaya sana na huu mgawo to the extent kwamba hata hizo pesa za kuwalipa DOWANS ni cha mtoto!
 

Toto la FISADI lazoza JF!!!
 
MAJIMSHINDO HUMU WATU WANADISCUSS DOWANS WE UNAANZA KUMDISCUSS MTU KWANI NI LAZIMA UCHANGIEW HOJA KAMA HUONI CHA KUCHANGIA NI BORA KUKAA KIMYA.
:focus:
MI NINACHOONA HAPA KNY SAKATA LA DOWANS BADO WAKUBWA WANAUMIA SANA KWAMBA ULAJI UNAONDOKA KWAO SASA ILI WAENDELEE KULA INABIDI WATAFUTE GIA YA KUINGILIA WE UNAFIKIRI CTI WATATOA WAPI HIZO PESA ZOTE ZA KUKODISHA MITAMBO? AFU BADO SUALA LA EXPERTISE NA LENYEWE LITAWAUMIZA HIVYO ITABIDI WARUDI TENA CASPIAN KUOMBA WATAALAM AMBAKO HUKO WATAKUTANA NA KINA R.A PAMOJA NA EL KWA HIYO NGOMA INAKUWA ILEILE KAMA AWALI.

SAMAHANINI JAMANI NIMESEMA CASPIAN MAKUSUDI HAPO SIYO KWAMBA NIMEKOSEA MAANA KWA MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA KNY KESI YA DOWANS NA TANESCO AWALIOKUWA WANAIWAKILISHA DOWANS WALIKUWA NI CASPIANS NA HAPO NDIPO KNY UTAMU.
 
I dont care about the next election. I do about the next generation.

Endelea kumwaga sumu zako. Sibabaiki. I do the right thing and inshaallaah i will succeed for the benefit of my country!

Zitto,

Ninapajua Kiwira na environmnetal setting yake. Sio kumpeleka mtu pale akazalishe umeme halafu baada ya mda watu wanasuffer eti kwa kuwa tunataka umeme (Mind next generation and our country). Kama umeenda pale na ukaangalia how the site has slightly suffered kutokana na uchimbaji wa kipindi kile utakuwa nami.

NSSF kwa sasa haina competency ya uchimbaji, coal processing to power. Kwanini wao wasi-finance????? what is wakatafuta competent company wakaipa fweza? any idea???
 

Nawasiwasi na kauli zako Zitto. Je, jana Tanesco katika hotuba yao walitoa tamko kuwa kusini kuna kampuni inaendesha uduma ya umeme kupitia mgongo wa Tanesco na wanatanecso wanapata taabu na walishakubaliana na hiyo kampuni Tanesco ijitoe kwenye operation kusini ila kukawa na kukwepana. na isitoshe wanatoa uduma mbovu na mitambo yao ni mibovu na hivi sasa CTI inataka kunua mitambo ya Dowans then iingie kwenye mchakato na tanesco maswali yangu ni haya

Tokea tamko la kataka umeme mpaka leo Kweli Serikali aina fedha ya kununua Mitambo mipya Mpaka hiyo ya DOWANS?

Kila kukicha nyie wanasiasa hamna fikra za kutafuta wawekezaji wengine katika Umeme ila ni DOWANS tuu?

Vipi kuhusu sheria ya manunuzi ya vitu chakavu kweli serikali inakubali kupisha sheria ya kununu vitu chakavu? tumefikia hapo? serikali gani duniani inanunua vitu chakavu hata kama wako kwenye critical situation?

Kwenye zunguka kwako mpaka leo embu tupe outcome ya mradi hata mmoja ambao umeshaanza kazi au ndio kama Pinda? Au kauli zenu (ipo kwenye mchakato) na ukizingatia ni kodi za wananchi mnaendelea kuzikomba.

Elimisha umma, usiwe na jazba
 
Zitto povu lote hilo la nini?

Tulia mkuu acha munkari......wacha watu watoe mawazo yao na wewe pendekeza yako na sio kututisha kwa matusi...... jibu hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…