CTI Kutumika kukodisha Majenereta ya DOWANS: Fikra Pevu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CTI Kutumika kukodisha Majenereta ya DOWANS: Fikra Pevu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 16, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Habari za kuaminika toka ndani kabisa (ka nzi) zinataarifu kuwa Shirikisho la Viwanda Tanzania linampango wa kuwashaa mitambo ya Dowans baada ya kukodi mitambo hiyo toka kwa wamiliki.

  Mpango huu ambao bado unapingwa na
  TANESCO unaelekea kufikia hatua za mwisho baada ya vikao kufanyika leo ambapo shinikizo kama lililokuwepo wakati wa kuingia Richmond linaongezeka hatimaye TANESCO wakubali kuingia mkataba na CTI – Confederation of Tanzania Industries.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho CTI ambayo imekuwa kwenye ukasi haijaeleweka imepata wapi fedha za kukodisha mitambo hiyo na kwanini kusita kwa TANESCO kuingia kwenye mkataba mwingine hakuchukuliwa maanani. Shirika la
  TANESCO linadai kuwa hali ya dharura nchini imeanza kutengemaa taratibu na ya kuwa tayari IPTL na hata Kidatu wameanza kuzalisha umeme zaidi na kufidia pengo.

  Soma zaidi kwenye saiti dada ya JF(Fikra Pevu) - CTI kukodisha Dowans; Kuiuzia Tanesco umeme? | Fikra Pevu | Kisima cha busara!
   
 2. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Tumekwisha!

  Dowans iliirithi Richmond kinyemela kwa shinikizo la serikali dhalimu ya CCM chini ya Kikwete na sasa CTI nayo kwa msukumo wa serikali hiyo hiyo inataka kuirithi Dowans. Wezi na matapeli hawana wasiwasi Bongo kwani Kikwete, badala ya kuwalinda wananchi, ameamua kwa makusudi mazima kuwapakata wezi hata kama wanamnyea, si walimwingiza madarakani? Je, hatukushuhudia wezi wa EPA wakiombwa kurudisha hela walizokwiba?

  Linalosikitisha zaidi ni kuwa wanaoibiwa wanadanganywa kuwa njia pekee ya kudumisha amani na utulivu ni kubaki katika njaa, ufukara, maradhi na ujinga na wao wanakubali!

  Kalaghabaho !
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  MKJJ

  majibu yako ni very simple:

  Taifa linapoteza BILLIONS kwa kutokuwepo umeme

  Sijajua how much many lives kwa sababu ya direct au indirect loss of umeme

  Yes najua utauliza swali kuwa JE KUWASHA MITAMBO YA DOWANS ndio ufunguzi wa muda mrefu? Jibu ni NO SIO lakini thats the immediate alternative

  Pia kama sheria zikifuatwa then ziwashwe huku taifa linaendelea kutafuta long term solution to our power crisis

  Last but not least sijawahi kukuona ukiuliza role ya PPRA, Lawyers na officials waliotufikisha hapa ambao as we speak wako kazini kama kawaida

  Unless iitwe public enquiry at later stage kujua tatizo lilikuwa ni nini na nani ali play role gani...tena LIVE on Our own version of C-SPAN (Bunge TV ) perhaps?
   
 4. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  yetu macho kwa sasa!!!
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  SLIDINGROOF, kwanza, kweli unasema hilo halijawahi kuulizwa ? Pili, are you really sincere kwamba hujui kwa nini waliotufikisha hapo bado wako kazini ? Nani alitakiwa awawajibishe ? Mwanakijiji ?

  Unaongea kama vile hujui yanayotendeka nchini kwako. Ni kweli huoni juhudi za makusudi zinazofanyika kumnyamazisha yeyote yule anayejaribu kuhoji haya mambo kwa kisingizio cha kuifanya serikali ichukiwe na wananchi na hivyo kuhatarisha amani ? Hiyo public enquiry mfano wa C-SPAN itawezekanaje wakati hata hiyo airtime kwenye radio na tv za Umma na public zimehatamiwa na wanaotetea status quo kama Wasira, Simba, UVCCM n.k. ?
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mzee wewe ni mkongwe mwenzangu hapa; wakati watu wanauliza mambo ya PPRA leo mimi nilianza kuuliza tangu 2006. Tatizo langu huwa sipendi kujirudia huwa nang'ang'ania kitu kwa muda fulani nikiamua kuachana nacho ndiyo hivyo tena. Tatizo ni kuwa lawyers na officials waliotufikisha hapa wanasimamiwa na walio juu. Ndio maana wengine tumewang'ang'ania hawa kwani hawa wasipowajibika hawa waliochini watawajibishwa na nani?

  Sidhani kama kuna mtu ana tatizo na majenereta hayo kuwashwa tatizo kubwa ni kuwa hayapaswi kuwasha kana kwamba hakuna sheria na bila kujali jinsi Taifa lilivyochezeshwa shere hapa. Namna pekee ya kuyawasha (kama kweli wanaamini kuna tatizo ambalo ni urgent la umeme) ni kwa Rais kutangaza hali ya dharura; kususpend sheria ya manunuzi, na within days kuagiza majenereta yetu ya kudumu bila kuhangaika na suala la tenda. Haya yamo mikononi mwa Rais.

  Lakini hatofanya hivyo kwa sababu akifanya hivyo na kutatuta tatizo hili la nishati, marafiki zake watapata vipi fedha zao. Tunasahau kuwa Rais Kikwete alikuwa waziri wa nishati na madini kwa karibu miaka sita na sasa amekuwa rais kwa miaka mitano na katika pande zote mbili ameshindwa kuonesha uongozi kwenye suala la nishati. Tatizo siyo umeme, ni uongozi.
   
 7. A

  August JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Halafu wenye viwanda hao hao ndio wenye kupewa misamaha ya kodi, na kuruhusiwa kupandisha bei wanavyo taka kisa biashara huria, akifanya hivyo mwenye daladala, mwalimu, daktari nk ni muhaini, au anakwenda tofauti na sera za chama tawala
   
 8. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  mh!mambo yanatokea mchana kweupe mbuzi anakula majani.Kweli Wabongo msumari viongozi nyundo
   
 9. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kaazi kweli kweli, ya kiwira nayo tunaendelea kuyasubiri.
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Kwani billions na' lives' zimeanza kupotea mwaka huu? Si JK aliingia madarakani na tatizo hili. Unaposema 'longterm solution' ipi kama miaka 6 hatujaweza kupata. 'Longterm solution' inapatikana kwa kuachia Dowans iendeleze uhalifu.

  Hakuna sababu ya kutafuta dagaa wa PPRA, lawyers na officials. Bunge lilimwambia JK hawa ndio mapapa kwa majina, alifanya nini zaidi ya kuwazadia kustaafu, vipi tuwabebeshe mzigo wabeba 'vimemo'.

  Kwani huoni Makinda anavyozuia Dowans isijadiliwe, bunge TV itawezekanaje.

  Sheria ya manunuzi inabadilishwa kukidhi haja ya mtu mmoja, sasa CTI nayo inaingizwa kutupumbaza.
   
 11. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hivi ule umeme wa upepo kule Singida uliishia wapi?
   
 12. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Ni kama ule wa KIwira,Nyerere's gorge(stieglers') ulikoishia...ili waendelee kutukamua
   
 13. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  mimi nasubiri umeme wa NSSF
   
 14. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwanakijiji kwa ufupi ni kuwa nguvu za Rostam na EL, Tanzania ni ABSOLUTE. Yaani mkwere nchi si yeye anayeongoza.

  Bunge lijalo kwa nguvu ya Rostam na EL, PPRA (2011) itapitishwa ili tu mitambo ya dowans iweze kununulika.

  Kwa kupitia Zitto, January na Dau wa NSSF, Kiwira italazimishwa kupelekwa NSSF ili ulaji mkubwa wa at least 100billion uwepo ambao utawezesha rais wa 2015 kutoka miongoni mwa chaguo la EL na RA.

  NSSF wanangangania kuown na kugenerate umeme through Kiwira wakidai wana strategic investor, lakini inajulikana Caspian na sub contractors wao ndio wanataka kuchimba coal na kudeal na masuala yote ya uzalishaji.

  Zitto ni kama amepagawa sasa hivi yaani kila kona akikutana na mtu anatafuta Support ili watu waisupport NSSF kuown na kugenerate umeme Kiwira.

  Suali la ajabu ambao wataalamu wanashangaa ni NSSF na TAnesco yote ni mashirika ya umma, sasa kwa vile NSSF wanazo hela kwa nini wasiikopeshe Tanesco hizo $400 million with GOVT Guarantee ili tanesco izalishe huo umeme ambao ndio MANDATE YAKE??

  Jibu ni kuwa NSSF through DAU ni kama agent wa EL na RA, kwa hiyo pesa ziko guaranteed kuliwa through NSSF than kuliko Tanesco.

  Fuatilieni vioja vya Zitto na January in the COMING DAYS mtaelewa zaidi.

  May God Bless Tanzania.
   
 15. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  Kwanza unaelewa nini kuhusu IPP in Tanzania au Independent Power Producer ? Kisheria NSSF kama IPTL na Songas sheria inawaruhusi ku zalisha umeme ila TANESCO bado wana monopoly ya distribution

  inanekana umeamua ku bwa bwaja bila kuleta ushahidi wowote ule waka kufanya utafiti wowote ule

  wapi Capian wamesign mkataba na NSSF au Tanesco?

  You cant even think!?
   
 16. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tanesco na NSSF yote yana maslahi na nchi, right??

  Tanesco ndio wana expertise na power generation, swali la kujiuliza wewe ni Kwa nini hutaki Tanesco waown KIWIRA?? NSSF wao hawana expertise na mambo ya umeme itawalazimu kuingia joint venture na kampuni nyingine ( ambao wewe na mimi tunajua RA & EL ndio wana push), sasa why not NSSF watoe hela wapate interest say 10% per yr kama investment zao nyingine, then Tanesco wapate kugenerate power ambao ni very profitable, na faida waitumie kwenye distribution systems costs?/ Win WIN right??

  Lakini tunajua kinachoendelea nyuma ya pazia, so let us wait all will come in the light soon, sababu nowadays kila kitu kitawekwa wazi hatua kwa hatua.

  Continue na matusi na kungangania vitu lakini this time it won't work.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  sidhani kama watapewa jinsi walivyo sasa.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Believe me... nafuatilia kwa karibu kweli hili..
   
 19. S

  Selemani JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Its getting old. Seeing and reading Dowans everydays is taking a toll in me. It seems like we as a country are obsessed with smallness. We should be ashamed of ourselves for discussing Dowans since 2006. What a country! Maybe wabongo tumelaaniwa. If as a country we can't reach a consensus on Dowans, we are doomed.

  Siasa, paranoia, propaganda and chuki got into reality and grown people cannot make their minds up on small issues like Dowans or Kiwira. Whatever happened to commonsense? Wabongo tuna matatizo.

  Kwani, it makes sense for CTI to want Dowans. They are in business that needs UMEME. And DOWANS generate UMEME. How hard is that to comprehend? Damn!
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Kama ulikuwa huelewi kuwa mwanakijiji ni fataani sasa ndio utamuelewa. Ushawahi kuona kitu chochote "positive" kutoka kwake? Mimi sijawahi, majungu, fitina, kuponda hayo ndio ayajuwayo yeye. Fikra zake ni kuanzia sasa kurudi nyuma, hana uwezo wa kutazama ya kesho tu licha ya mbele zaidi. Huu ni ugonjwa unaosabishwa na wivu, chuki, roho mbaya za kurithi "genetically". Hauna dawa.

  Hasad zimemjaa.

  Hiyo ni analysis yangu kwa mwanakijiji kutokana na maandishi yake.
   
Loading...