Nakuomba Rais Magufuli; Tafuta fikra mbadala ili kujenga uchumi na kukuza biashara kimkakati kama Farao wa Misri katikati ya changamoto ya Covid 19

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,466
2,860
Baada ya hali ya dunia kuwa tete kutokana janga mlipuko wa CONVID-19 duniani kote, Tanzania kama sehemu ya dunia itakwenda kushuhudia “a major shift” kwenye vipaumbele vya kitaifa na kimataifa (national and global priorities). Bila shaka hapa Tanzania tukafikia kwenye ulazima wa kuwa na zaidi ya utoshelevu (self-sufficient) ikiwa ni pamoja na kuboresha uwezo kwenye uzalishaji wa ndani ya nchi ili kuhakikisha tunakuwa na usalama wa chakula (food security) ili kuwa na maendeleo endelevu.

Ni ushauri tu kwa Rais na wasaidizi wako, licha ya uwezo mkubwa na mabingwa wa kujua mambo vitabuni waliopo serikalini, ila kuna haja ya kuwa na fikra mbadala na huku chini ntatoa mifano halisia. Aidha nasisitiza mkakati au mikakati kwani kwenye kila nchi natumia Tanzania pia itakuwa miongoni, huwa kuna off-book strategic operations ili kufikia malengo fulani. 90 minitues in Entebbe haikuwa bungeni wala kwenye procedures, ilikuwa ni lazima ifanyike ili kufikia malengo ya wakati ule. Hali kadhalika kwenye kujenga biashara na uchumi endelevu, kuna haja ya kufanya majamboz ya kimkakati ili ndani ya muda mfupi tunasogea kweli kweli.

Kwa kuwa “campus yetu” ni dira ya maendeleo ya Taifa 2025 yenye lengo lengo la kujenga tabaka watu wenye kipato cha kati (middle class earners) tuna wajibu wa kuendelea kuwa na mafungamano na ushirikiano kati ya Serikali na wadau mbalimbali hasa wananchi wa ndani toka sekta rasmi na sekta isiyo rasmi ili kufungamanisha mashirikiano kwa lengo la kushinda vita dhidi ya umasikini, ujinga na maradhi.

Umasikini na ujinga ni mapacha ambao wanazaa baadhi ya maradhi mengine ambayo watu wakiwa na maarifa na kipato kizuri wanaweza kuepuka. Mathalani, malnutrition kwa wamama wajawazito na under 5 malnutrition, hii inaweza kuwa mitigated kwa wamama tarajiwa kula vyakula bora (qualitative and quantitative diet) na mtoto aliezaliwa kupata lishe. Lishe ni matokeo ya uzalishaji wa chakula cha kutosha kwa makundi yote ya vyakula ili jamii ya Kitanzania iwe na lishe bora kwa ajili ya jamii bora ya sasa na Taifa la kesho.

Nitoe mfano hai, Qatar baada ya kuingia kwenye mgogoro wa jirani yake Saudia na UAE, alilazimika kuwa na short term plan na long term plan kwa mambo kadhaa. Kwenya uhitaji wa maziwa pekee, Qartar walilazimika ku-import machine za kuchataka maziwa, ng’ombe wanaotoa maziwa tayari, chakula cha mifugo na kujenga mabanda kwa muda mfupi ili ugavi wa maziwa kwa soko la ndani usipungue au kuisha kwa kuwa kuna mgogoro wa kisiasa na uchumi kati ya Qatar na jirani zake. Kwa sasa wana Ng’ombe wa maziwa sio zaidi ya 10,000 ambao wanakamuliwa kukidhi soko lote la ndani la maziwa (UHT, maziwa ya unga, maziwa ya mgando na products zingine za maziwa) kwa ajili ya matumizi ya chakula au chochote kile.

Turejee kwenye basic imports ambazo locally zaweza kuzalishwa kwa lengo la kupunguza bei ya manunuzi kwa soko la ndani Watanzania hii ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa ndani kuwa chanzo cha kazi/ajira rasmi.

Mathalani kwa mujibu wa ripoti ya CAG … “JWTZ walilinunua 'Combat suit' zenye thamani ya zaidi ya Tsh 4,242,319,008 (bilioni nne na ushee) bila kuwa na mkataba na muuzaji (M/S 21st Textile Ltd) [ukurasa 190]”

Kwa positive side, kwangu mimi ni milestone kubwa sana kwa JWTZ kununua combat suit kwenye soko la ndani maana 21st Textile ni kiwanda cha ndani mkoani Morogoro na bila shaka katika hayo mauzo kuna kodi ya VAT (18%) imerudi serikalini. Umeme wamenunua Tanesco, Maji kwa matumizi ya kiwanda wamenunua toka soko la ndani, wanfanyakazi wanalipwa mishahara, PAYE na makato ya pensheni yanaingia kwenye mzunguko wa ndani kwenye account za TRA na mifuko ya pensheni.

Huko nyuma mavazi au vitambaa bila shaka vilikuwa vikiwa imported toka ughaibuni jambo ambalo sio afya kwenye kujenga uchumi wa kati kwa kutumia viwanda.


Tuje kwenye facts zingine,
Tuna watoto wangapi wa shule za msingi (viatu, mashati, sketi, kaptura na masweta)
Tuna watoto wangapi wa shule za sekondari (viatu, mashati, sketi, kaptura na masweta)
Tuna wanavyuo wangapi (tuhakikishe viatu vyao na uniform au mavazi yao vinazalishwa na viwanda vya ndani)

Tuna hospitali ngapi kwa ajili ya (mauzo ya mashuka na uniform za wafanyakazi kama madaktari, nurses, wafamasia, medical attendants, sare za wagonjwa). Manunuzi yote ya products za nyuzi kwa kuwa tuna-import kuna fedha nyingi sana tunapoteza ambazo zingezunguka kwenye mikono, mobile monye na mabenki ya Tanzania.

Kada ya wanafunzi na wafanyakazi katika organized institutions ni soko kubwa sana. Hapa tungewekeza kwenye textile industry kwa kutumia pamba ya ndani, na tukawekeza kwa kuchakata ngozi za wanyama tunaochinja kwa ajili ya viatu na mikanda kwa soko la ndani tu kuna fedha nyingi sana tungeokoa kwenye imports na pia tax base kwa TRA ingekuwa kubwa. Kuna kazi nyingi sana zingezaliwa katika sekta rasmi na sekta isiyo rasmi ikiwemo.

Tunafikaje hapo.

Ushauri mkubwa hasa ni kwa Rais maana wewe ndiwe Farao wetu na amri jeshi mkuu, kila mmoja huwa anamtazama CIC wakati wa changamoto kamba ambavyo kila taifa kwa sasa linafanya. Tatafuta Watanzania wenye vision waliopo kwenye mifumo rasmi na wasio kwenye mifumo rasmi ambao wana sustainable investment projects. Term of reference ya kila project iwe mikakati ya 1) Kupunguza imports, 2) Kuongeza exports, 3) Kutengeneza ajira kwenye sekta rasmi na sekta isiyo rasmi, 4) Kuongeza tax base kwa TRA, 5) Kuongeza wanachama kwenye pension funds, 6) Kuongeza wanachama katika health insurance funds, 7) Kuongeza watu wanaoishi kwenye makazi bora. Hii ni mafano tu.

(Kwenye Kilimo, mifugo na uvuvi kuna lots of sustainable project zaweza kuzalishwa kwani dunia inakula kila siku.) Asbuhi, mchana na jioni. Kuna products za chakula za matajiri tunaweza kuzalisha, kuna products za watu wa kati, tunaweza kuzalisha na products za watu wa kipato cha chini. Kote huko fedha inazunguka.

Kwanini nimeshauri watu wenye vision hata kama currently hawana kitu au wana kitu kidogo sana ila wana investment projects za kutupeleke mahali kama nchi.

Mathalani; Mwl. Julius Nyerere hakuwa na kitu cha kuonesha kabla ya uhuru 1961. Ila baada ya Uhuru na kuwa Rais wa Nchi aliongoza Tanzania kama Taifa la watu wamoja, akavunja ukabila na kuongoza mapambano ya ukombozi dhidi ya wakoloni wa Msumbiji, Zimbawe, Angola na Namibia. Sio kila Rais Afrika alikuwa na vision na tofauti ya JKN na akina Kenyatta tumeiona kwa kwa Nyerere kukalia kiti cha Urais wa JMT.

Ruge Mutahaba, hakuwa na experience yoyote ya kuendesha Radio ikiwa ni pamoja na kuimba. Yet kwa miaka chini ya 20 yeye na Joseph Kusaga baada ya kufunguliwa Clouds media, wamefanya Watanzania wengi wazee kwa vijana kufurahia ulimwengu entertainment radio unlike serious radio program kaka RTD na kwa sasa TBC. Ruge kaibua vipaji vingi kupitia THT yet yeye bila shaka hatujawahi kumsikia akiimba hata chorus moja.

Yusuf “Jacob Isaac Ibrahim”. Huyu alikuwa mfungwa gerezani ambae alikwenda kwa Farao kumsaidia kutafisiri ndoto. Yusuf hakuishia kutoa tafsiri pekee, bali alipewa nafasi ya kuweka akiba ya chakula kwenye maghala wakati wa wingi wa chakula kwenye miaka 7. Kazi ile alifanya kwa miaka 7 ya njaa. Yusuf hakuweka akiba ya chakula kwa Misri pekee, aliwafikiria na mataifa jirani ambao wakati wa njaa wangefika Misri wakiwa na fedha ili kununua chakula.

Kuna mfanyabiashara mmoja mkubwa sana Tanzania. Naomba jina nilihifadhi. Miaka ya 90 hakuwa na kitu in term of assets. Ila baada ya kujihusisha na siasa na aliweza kujipenyeza kumiliki baadhi ya mashirika ya umma yaliyouzwa/kugawiwa. Jamaa huyo alitumia assets kukopa na kujenga biashara. Kwa sasa ni billionea na juzi hapa kafanya donation serikalini. Hakuna na utajiri wakati wa Mwinyi na JKN na baadhi ya wanafamilia wake wanafahamika, ila wakati wa Mkapa alitumia akili zaidi kujitajirisha.

Sasa hapa najikita kwenye kutafuta watu wenye kutumia akili zaidi kutupa National solutions. Of course wao watafaidika, ila faida wanayoiacha ni kubwa ukilinganisha na nini wao wanapata. JKN legacy aliyoiacha ni kubwa kuliko material wealth. Ruge alichokifanya, bila shaka wengi walishuhudia namna gani aligusa maisha yao.

Kama Taifa, ujio wa Covid 19 usitufanye tu-panic na kutumia mbinu zilezile na mikakati ile ile kutatua matatizo yetu. We need to come out with new strategic plans to see Tanzania Development Vision 2025 bado inaweza kuwa realized kwa kujenga uchumi kwa kutumia viwanda kwa kulenga kuingiza au kupanua wigo wa mapato ya serikali ndani ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu.

Wakati wa kusoma bajeti yam waka 2020/21 ikihitimisha ungwe ya kwanza ya JPM kuna lots should be done to strategies in the course of solving our problems which is aimed at increasing wealth in our motherland Tanzania.

Kwenye kutafuta vaccine ya Covid 19 na tiba, hakuna open game in the name of hizo ndiyo procedure za kufuata ili kupata dawa au kinga, bali wataalamu wamejifungia wakitafuta solution. Yule atakaepata sio faida kwa kampuni yake pekee, bali nchi nzima anayotoka kwa maana watu wengi watahusika kwa namna moja au nyingine kwenye mnyororo wa thamani.

Tukitumia Soko la Africa hata Ulaya, Putin anakuwa relevant kwa kusema ardhi tuliyonayo tukiitumia vyema, tunaweza kuwalisha Waafrika na Ulaya maana rutuba iliyopo na maji yanatupa hiyo advantage. Ni namna gani Benki Kuu, Benki ya Uwekezaji na Benki ya Kilimo zitafanya facilitation role kama wakubwa wataamua ili hao visionary waweze kununua technology na know how in term of shorttem consultation kwenye kujenga sustaible investment projects.

Kwa akili ile ile tunaweza kuwa na kikosi kukusanya taarifa nani kamsema vibaya Rais mtandaoni na kutafutwa, kuhojiwa na kushtakiwa, iko haja kuwa na watu wenye capacity kama Ruge, alimsikia Nandy na kumsaidia kuwa mwanamuziki bora wakati kabla ya hapo Nandy hakuwa ana jina na hakuwa na hela. Leo Ruge hayupo, Nandy anajua kuimba na anatengeneza fedha na katika mtiririko wengi wanafaidi ikiwemo TRA.

Ni muhimu Rais ukahusika kwani kuna conditions zingine ili mtu afike mahali ni mpaka kuwezeshwa. Mathalani, pamoja na uwezo wote wa Waziri Mkuu Majaliwa, ni mpaka awe mbunge ndipo a qualify kuwa Waziri Mkuu.

Kuna watu wanaweza kufanya makubwa sana, lazima kutafuta namna ya kuwa qualify ku-access finance kununua technology na kununua/kugharamia know how kwa kutumia watalaam wa ndani na nje ili kukuza uchumi kwa kupunguza imports na kuongeza exports ili tuwe na more balance trade surplus unlike balance trade deficit.

Ifikie wakati balance of payment iwe vizuri kwani hata service sector nje ya Tanzania ifanye vyema ni lazima tuwe na lots of tradings nje ya Tanzania. Kama tuliweza kuwakomboa Zimbabwe, kwanini leo tusiwalishe na minofu ya samaki toka fresh waters across Tanzania, huu ni mfano mmoja tu.

Ni mtazamo tu.

Nawatakiwa Pasaka Njema wakuu.
 
JPM is a great thinker. Toka kaingia mpaka sasa kafanya mengi na makubwa. Sio sawa kumdhania Rais wetu namna hiyo.

Kwa haya anayofanya kupitia watu wake, akipata na fikra mbadala toka nje ya circle yake kuna mengi anaweza kuyafanya na kuachana na kuendelea kutembeza bakuli kwa wazungu
 
Hoja yako ni nzuri matuja lakini jiwe anamwamini makonda tu ,leo hii zao la korosho linaoza majumbani lakini ni yeye alisema masoko ya mazao tunayo na kama hakuna tutakula wenyewe hivi mtu kama huyu anafiri kweli au ni mpuuzi tu flani
 
Hiyo inaitwa personification kwenye fasihi kukipa uwezo kitu kisicho binadamu kufanya kama binadamu.

Nadhani mnampamba nakumvimbisha bichwa pasipo sababu za msingi.
Kagame ameikuta Rwanda ni magofu 1994.
Mwaka huu kama sio Covid 19 bila shaka angefanikisha kuandaa mkutano wa jumuia ya madola.
Ana kumbi kubwa za kisasa, hotels za kuweza ku accommodate wageni wa kimataifa wa kutosha.
Kuna vitu amefanya kama marketing niche kwa size ya Rwanda.

JPM leo ana miaka 5 tu; kuna mengi anaweza kufanya kwa mikakati mbadala.

Bila shaka tuna haja ya kumuunga mkono kwa haya yanayofanyika, ila kuna mengine mengi huenda hayahitaji mtaji mkubwa kwa fedha za ndani; ila kuwasikiliza watu na kuwapa endorsement wafanye uwekezaji kwa rasilimali hizi hizo ili kufikia malengo yake yeye kama mkuu wa kaya, hali kadhalika Watanzania nao wakapiga hatua kubwa huku "kibubu" kikiwa na another reliable source ya kukusanya kwa kuwa biashara zinafanyika na mzunguko umeongeza hasa kupitia local investors ambao tunatumia technology sahihi yenye kutupaisha kwa muda mfupi na muda wa kati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wananchi , kama wanalipa kodi , serikali inapashwa kufanya yote hayo unayoyazungumzia. Wala sio swala la kumsifu Magufuli...uwo niwajibu wake.

Pia tukiangalia hali za wananchi mmoja mmoja bado ningumu sana .
Early '80 Rais wa Marekani Ronald Reagan alikuja na model ya kutengeneza economic stimulus package ili watu wafanye kazi, wazalishe wawe na fedha, ili wa-spend zaidi inturn tax base itapanuka.

Kama kuna eneo liko very reliable kupata kodi ni kwa wafanyakazi. Wanalipa PAYE, wanalipa indirect tax kupitia manunuzi mengi ambayo yako taxable kama umeme, maji, airtime, mafuta kama mtu ana gari, kodi ya ardhi, kodi ya kumiliki nyumba maana wafanyakazi wengi wanajenga, kodi ya makato kwenye bank deductions na mobile deductions kote huko kuna kodi ya serikali.

Point yangu, kama Taifa tuna import zaidi ya tani laki 4 za samaki, tukifanya ufugaji na uvuvi wa samaki ukawa wa kibiashara kwa kulisha kwa soko la ndani na kuuza samaki fresh au sausage za samaki au minofu ya samaki, fedha zikaingia katika mifuko ya watu ambao huko nyuma hawakuwa kwenye mfumo rasmi, it is simple mathematics tax base ya TRA inapanuka.

Ndiyo maana tuko hapa ku-advocate, pamoja na long term good projects kama Nyerere Hydro Power, SGR tunaweza kuwekeza kwenye value chain ya agro products likewise ku-fill the gap imports kwa vitu ambavyo tunaweza kuzalisha domestically.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom