CRDB Sim Banking haipo salama

CRDB Sim Banking haipo salama

kamanda5ch

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2013
Posts
210
Reaction score
285
Leo niliamua nicheki balance kwenye sim banking ya crdb ,ofcoz mimi nina acount moja tu ya hiyo bank, basi nikabofya *150*03# nikaingiza pin then nikachagua balance ,nikakuta kuna acount namba 2, inabidi nichague mojawapo (si unajua mtu unaweza kuwa hata na account 10), nikaduwaa hii ya pili ya nani ,nikacheki jina likatoka la mtu mwingine so nikawa na uwezo wa ku access acount ya huyo jamaa nipendavyo kwa kutumia cmu yangu ,ningependa ningehamisha mpunga wake wote but m innocent nikajisalimisha bank kuwaambia hii ni hatarii kwenye acount zetu
Note
inawezekana account yako ya crdb inatumiwa na watu wengine bila kujua na hii ni kutokana na uzembe wa bank husika so tunza kumbukumbu zako za transaction kila unapofanya.
 
Dah, hatari.... mimi nilishangaa nikiangalia salio naambiwa nina 0.00. Nikahamaki... nikakimbilia pale CRDB Lumumba kuchukua statement. Nakuta pesa ipo ila nikiangalia salio lililopo nitofauti na salio lililotakiwa kuwepo. Kuangalia naona kuna miamala mingine haipo na mingine ipo katika tarehe tofauti. Kuwauliza nikaambiwa ni tatizo la system zao. Baada ya siku 2 pesa ikarudi. Ila imekaa siku 1 tu nakuta pesa hamna.. nauliza naambiwa kuna manunuzi ulifanya tarehe 9 August ndo yamepitishwa leo tarehe 3 September.

Kiufupi kama unaakaunti kwa hawa jamaa inatakiwa uwemakini na mwenendo wa pesa zako. Mi mpaka sasa nimesha ngaili kutunza pesa huko... nitawatumia kwa transaction ndogo ndogo tu.
 
mkuu you're scaring me. Nina acc crdb tu (baada ya kukimbia NBC), na Leo nimeiwezesha ishop online and it handles "ALOT" of cash, waki i hijack I'll be devastated. Sasa kwa hizi taarifa tena mbona napoteza imani.
 
yaani acha tu nime access account ya mtu mwingine zaidi ya masaa mawili kupitia simu yangu nikaamua nikawape taarifa bank
 
mkuu you're scaring me. Nina acc crdb tu (baada ya kukimbia NBC), na Leo nimeiwezesha ishop online and it handles "ALOT" of cash, waki i hijack I'll be devastated. Sasa kwa hizi taarifa tena mbona napoteza imani.

mkuu, mimi natumia CRDB Kufanya manunuzi mtandaoni mara nyingi. Ila wiki 2 hizi mambo imekuwa majanga. Ila mwanzo niliwakubali sana, but kama wakifanikiwa kurekebisha system zao wapema basi we utaenjoy.
 
Mbona hii ni hatari sana!
Kama umewapa taarifa ni jambo jema. Nadhani watakulipa maana umewasaidia kuboresha mfumo wao!
 
mkuu, mimi natumia CRDB Kufanya manunuzi mtandaoni mara nyingi. Ila wiki 2 hizi mambo imekuwa majanga. Ila mwanzo niliwakubali sana, but kama wakifanikiwa kurekebisha system zao wapema basi we utaenjoy.

safety is what scares me a bit. Baada ya kusaini form ile, ATM card nailinda ka nini cause crdb wamejitoa kabisa kama nitaibiwa hela.
 
we ni mwongo sim banking ya bank gani ndo salama nmb huko ndo watu wanalia kila kukicha we ni mfanyakazi wa competitor wa crdb unajaribu kudhoofisha product zao kutuaminisha upuuzi wako kwa story za kutunga ndo maana huja sema hiyo issue uli report tawi gani na kwanani.
product za crdb ni salama matatizo ni madogo madogo ya kawaida ambayo hata kwenye bank zilizoendelea yapo..
crdb bado ndiyo bank bora kabisa kwa sasa Tanzania.
 
Mkuu mbona hueleweki? "....wewe ni muongo... sim banking ya bank gani ndo salama..." mbona unaji-contradict? CRDB sio benki?
Mbona umekimbilia kutaja NMB wakati mleta mada hajataja benki nyingine? "Matatizo madogo madogo ya kawaida" ndo yapi? Hayana usumbufu kwa wateja? Kwani hili tatizo la mleta mada ni dogo au kubwa, kwa vigezo vyako?
 
we ni mwongo sim banking ya bank gani ndo salama nmb huko ndo watu wanalia kila kukicha we ni mfanyakazi wa competitor wa crdb unajaribu kudhoofisha product zao kutuaminisha upuuzi wako kwa story za kutunga ndo maana huja sema hiyo issue uli report tawi gani na kwanani.
product za crdb ni salama matatizo ni madogo madogo ya kawaida ambayo hata kwenye bank zilizoendelea yapo..
crdb bado ndiyo bank bora kabisa kwa sasa Tanzania.

Dar es Salaam. Benki ya NMB imetajwa kuwa Benki Bora Tanzania kwa mwaka 2013.

Tuzo hiyo ilitolewa na Jarida la Euromoney linalojihusisha na masuala ya fedha, kwenye hafla mjini London, Uingereza.

Mwaka 2012, NMB ilitajwa kama taasisi iliyofanya vizuri kwa kutoa huduma za fedha, kuweka mitaji na zaidi kusaidia wateja kwenye masuala ya benki na ujasiriamali.

Akizungumzia tuzo hiyo, Mhariri wa Jarida la Euromoney, Clive Horwood, aliisifu benki hiyo kuwa kati ya zinazopiga hatua Tanzania na kwamba, hiyo imesukumwa na kutawala asilimia 40 ya wateja wa benki mbalimbali nchini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Mark Wiessing, alionyesha kufurahishwa na tuzo hiyo kutoka Euromoney na kwamba, hizo ni jitihada za utendaji mzuri wa wafanyakazi na menejimenti.

NMB yenye matawi 150 Tanzania na wateja milioni 1.8, kwa sasa imesambaa wilaya mbalimbali kwa asilimia 95, huku asilimia 60 ya matawi yake yakiwa maeneo ya vijijini.
 
we ni mwongo sim banking ya bank gani ndo salama nmb huko ndo watu wanalia kila kukicha we ni mfanyakazi wa competitor wa crdb unajaribu kudhoofisha product zao kutuaminisha upuuzi wako kwa story za kutunga ndo maana huja sema hiyo issue uli report tawi gani na kwanani.
product za crdb ni salama matatizo ni madogo madogo ya kawaida ambayo hata kwenye bank zilizoendelea yapo..
crdb bado ndiyo bank bora kabisa kwa sasa Tanzania.
Dah.... unamejikanyaga sana kwenye maelezo yako. Back to school...

Na namini hunahata akaunti CRDB, kwa sababu ungekuwa nayo na unaitumia basi ungendua tatizo wiki hii CRDB.

Mtoa mada ni mteja wa CRDB na mimi ni mteja wa CRDB pia.... huwezi kimbilia kuropoka eti we ni muongo.... think twice...
 
we ni mwongo sim banking ya bank gani ndo salama nmb huko ndo watu wanalia kila kukicha we ni mfanyakazi wa competitor wa crdb unajaribu kudhoofisha product zao kutuaminisha upuuzi wako kwa story za kutunga ndo maana huja sema hiyo issue uli report tawi gani na kwanani.
product za crdb ni salama matatizo ni madogo madogo ya kawaida ambayo hata kwenye bank zilizoendelea yapo..
crdb bado ndiyo bank bora kabisa kwa sasa Tanzania.

Hata nilipokwenda ku report hilo tatizo wafanyakazi wa CRDB waliniambia ni mwongo kama wewe unavyosema lakini kwa kuwa nilikuwa na cm nikabofya halafu nikawaonyesha nikawauliza vipi nihamishe mpunga wote wa huyu jamaa kama mimi mwongo waka vibrate sana nikawaambia wawe makini kwenye system zao. ni ukweli tupu sitaki kusema wapi kwa sababu najulikna sana kwenye branch na waliniomba nisiseme so thats it
 
njooni nmb mnaangaika nin system mbovu crdb.
 
kuzunguka kooote,hoja yenu imekaa apo...wewe na ID zako zote unapost kuwakashifu crdb ili upigie kampeni nmb yako...system nzuri ni ya nmb???you cant be serious. Jipangeni upya,kuwaharibia crdb si rahisi ivyo...mimi ntabaki crdb na exim wangu ndo naona wako bora zaiidi apa tz
 
Kama ni tatizo la ki benki wafuate wahusika walione, walitatue na ni kwa faida ya wote hata kama pesa yako imeibiwa nenda wataangalia na kukurudishia, ukishindwa unaweza hata kuwasiliana na mkurugenzi mkuu atalitatua mwenyewe, jamaa ni mchapa kazi haswa. HUku kwenye JF hakuna msaada mzuri kama wa benki husika la kama ni ku promote benki moja dhidi ya wengine basi tumekuelewa. CRDB ni benki ya kizalendo iliyopiga hatua sana.
 
Leo niliamua nicheki balance kwenye sim banking ya crdb ,ofcoz mimi nina acount moja tu ya hiyo bank, basi nikabofya *150*03# nikaingiza pin then nikachagua balance ,nikakuta kuna acount namba 2, inabidi nichague mojawapo (si unajua mtu unaweza kuwa hata na account 10), nikaduwaa hii ya pili ya nani ,nikacheki jina likatoka la mtu mwingine so nikawa na uwezo wa ku access acount ya huyo jamaa nipendavyo kwa kutumia cmu yangu ,ningependa ningehamisha mpunga wake wote but m innocent nikajisalimisha bank kuwaambia hii ni hatarii kwenye acount zetu
Note
inawezekana account yako ya crdb inatumiwa na watu wengine bila kujua na hii ni kutokana na uzembe wa bank husika so tunza kumbukumbu zako za transaction kila unapofanya.

Learn from me people. Nina mgogoro na CRDB kwa wiki tatu sasa. Ilianza hivi, siku moja nikiwa katika mishe zangu nikasikia sms imeingia. Kucheki ni CRDB ikisema - ndugu mteja kadi yako inayoishia *** imetumika kutoa pesa shs 83,550. Nikashangaa kwani sikuwa nimetoa pesa yoyote.

Kesho yake tena ikaja sms na amount hiyo hiyo. Nikapiga simu iliyopo kwenye kadi, nikaambiwa piga baadaye kidogo. Kesho yake tena ikaja sms ile ile. Siku ya nne nikawa hapa mjini nikaenda kwenye branch yangu mnazi mmoja. Ndipo wakaizuia kadi ile pamoja na mimi kujaza form za malalamiko.

Ajabu: Nililazimika ku-print statement mara tatu kwa sababu zile transaction hazikuonekana. Pesa imetoka kweli, transaction hazionekani kwenye statement, nimebaki na sms za system tu kwenye simu yangu. Mpaka sasa nasubiri jibu ingawa nilimwona IT wao amepanic kweli nilipokwenda na hizo sms.

Nathibitisha kile nilichoandika ni kweli tupu.

10307.jpg
 
Leo niliamua nicheki balance kwenye sim banking ya crdb ,ofcoz mimi nina acount moja tu ya hiyo bank, basi nikabofya *150*03# nikaingiza pin then nikachagua balance ,nikakuta kuna acount namba 2, inabidi nichague mojawapo (si unajua mtu unaweza kuwa hata na account 10), nikaduwaa hii ya pili ya nani ,nikacheki jina likatoka la mtu mwingine so nikawa na uwezo wa ku access acount ya huyo jamaa nipendavyo kwa kutumia cmu yangu ,ningependa ningehamisha mpunga wake wote but m innocent nikajisalimisha bank kuwaambia hii ni hatarii kwenye acount zetu
Note
inawezekana account yako ya crdb inatumiwa na watu wengine bila kujua na hii ni kutokana na uzembe wa bank husika so tunza kumbukumbu zako za transaction kila unapofanya.
Mkuu hii hata mimi ilinitokea juzi nilikuta account mbili ikasema choose an account with which to transact nikasita... technology inawashinda CRDB siku nyingine ukiangalia salio kupitia sim banking unakuta hela pungufu ukienda ATM unakuta ziko sawa....ni hatari sana...hata hivyo account yangu hiyo ni ya kupitishia kamshahara ka madafu tu....
 
Back
Top Bottom