Kuhamisha fedha kwa SIM Banking ya CRDB kwenye mitandao ya simu ni gharama kubwa sana kwa nini?

Shapu

JF-Expert Member
Jan 17, 2008
2,111
790
Unakuta unatoa sh 500,000 kwenye Mpesa wanakukata 6,399 (1%). Hii ni ghali sana. Nimeshangaa sana kuhamisha tu hela toka account yako kwenda account ya simu yako iwe ghali hivyo? Halafu kuingia kwenye app ya SIM Banking kuulizia statement unakuwa charged? kwa nini? kuuliza statment kwa ATM sawa labda kupunguza foleni lakini mm kwenye simu yangu nataka kujua statment kwa nini wani charge.

Nina fikiria tena ku bank na CRDB sio sawa.
 
kweli kabisa na wala sio hii tu ya SIM BANKING bali huduma zote za kibenki inabidi kuboresha sana huduma zao, sisi kama walaji tunaingia mashaka na mara nyingine tunasitisha tumia huduma hizi!

mfano endapo kunatatizo la kimitandao, ukitoa hela alafu ikakwama, hapo utaambiwa usubiri masaa 24 kabla tatizo lako halijatatuliwa, na tena maranyingine kama ni jumamosi utaambiwa mpaka jumatatu!

jamani hivi kweli tupo kwenye hii dunia, kama nilikuwa na shida na fedha yangu? kama sina fedha nyingine?
 
CRDB yapaswa iingiwe na shaka..kuwa na wateja wengi si kigezo maana malalamiko yamezidi kuhusu gharama zao mitandaoni na wasipokaa chonjo ,bhasi wateja wengi watawakimbia haswaa wenye vipato vya kawaida
 
Unakuta unatoa sh 500,000 kwenye Mpesa wanakukata 6,399 (1%). Hii ni ghali sana. Nimeshangaa sana kuhamisha tu hela toka account yako kwenda account ya simu yako iwe ghali hivyo? Halafu kuingia kwenye app ya SIM Banking kuulizia statement unakuwa charged? kwa nini? kuuliza statment kwa ATM sawa labda kupunguza foleni lakini mm kwenye simu yangu nataka kujua statment kwa nini wani charge.

Nina fikiria tena ku bank na CRDB sio sawa.
Mkuu ndio unashtuka leo?? Hawa jamaa wanacharge ghali sana.
 
Nilichoka nilipotaka ku transfer kwenye hizi crdb min bank kutoka account yangu kwenda acount nyingine ya crdb kila elfu 10 ikakatwa 900.
Nikajisemea ki moyo moyo Vibubu lazima virudi hakuna namna.
 
technolojia ya mobile money.. imeletwa na telecom industry,,,. sasa bank zimeona kampuni za simu zinafaidika sana kuliko wao.. wameamua kuweka makato makubwa ili nao bank wapate chao.. maana kampuni za simu zinanufaika sana na hizo huduma kuliko bank wanaokutunzia fedha zako
 
mkuu bank zetu za kitz sio kabisa, niliwahi kupewa statement ya nbc charges zikwa 140,000 kama nisingeshtuka na kudai tena kwa muda mrefu, nilishapigwa.
Kwa habari ya simbaking nao gharama zao ni kubwa mno karibu bank zote

Back
Top Bottom