CRDB acheni kuchezea pesa zetu wateja

CRDB acheni kuchezea pesa zetu wateja

Kuna tawi moja nchini nalihifadhi, ma teller wake ni mijizi kweli ukiweka mpunga mnene wanapohesabu wanakwambia bado elfu 10000 wakati wewe umehesabu home vizuri, sasa hiyo elfu kumi wakija wateja 10 si mpunga mzito.

Hii Benki itazamwe kwa jicho la ziada na serikali maana kuna uhuni mwingi unafanyika na kukwaza wateja.

Unakuwa na kias kikubwa benki lkn ukiangalia salio unakuta hakuna pesa ukifanya hivyo baadae unakuta pesa IMO wakati mwingine ukitaka kutumia huduma ya simbanking unaambiwa huna salio hata kama statement yako kuna ela za kutosha badiliken msipofanya hivyo kiama kinakuja.
 
Brnki nyingi wahufumu ni wezi sana,mimi kila nikienda kudiposit katika benk ya BOA naibiwa bila aibu,siku mija pale sinza nilikomaa eti teller akadai ananiongezea,jana tu nimeibiwa na dada mmoja nikamuangaliaaa,nikajua anapenda ela ya bure,namtegeshea tena yule dada nimuumbue,na siku nyingine dada mmoja aliniibua BOA ilala,sasa kwa wewe wa Africana take care
 
Tuliwahi kuhamasisha wateja wote wenye kutumia benki tuanzishe chama chetu, wazo hili halikupewa nafasi ndani ya "mioyo yetu".

Ili upate huduma bora lazima uwe mteja BORA. Huwezi kupata huduma bora wakati wewe ni mteja wa hovyo. Na mtu kuwa mteja bora lazima awe na weledi juu ya huduma anayopewa. Ajue haki zake na wajibu wake. Ajigeuze reli ili treni ipite kwa maana afanye juhudi kuondoa uozo na mapingamizi ya upatikanaji wa huduma bora kwa faida yake na vizazi vijavyo.

Ni kweli CRDB na benki zingine wana matatizo lakini Tatizo kubwa lipo kwa wateja. "If you want to change the world you must change you first"
 
Kwa sim banking yao nilitoa 3,390,000/- Wakanikata 640,000/-Sasa huu si wizi huu wa mchana??SINA HAMU NAO TENA MAISHA NA HUWA NAWASHAURI WATU WASIITUMIE KWANI NI UBABABISHAJI NA WIZI?
WEKENI WAZI SERVICE AMMOUNT ZENU SIO UJANJA UJANJA TU!0656880804

Nadhani ungeenda kufuatilia maana hiyo sio svc charge
 
Tuliwahi kuhamasisha wateja wote wenye kutumia benki tuanzishe chama chetu, wazo hili halikupewa nafasi ndani ya "mioyo yetu".

Ili upate huduma bora lazima uwe mteja BORA. Huwezi kupata huduma bora wakati wewe ni mteja wa hovyo. Na mtu kuwa mteja bora lazima awe na weledi juu ya huduma anayopewa. Ajue haki zake na wajibu wake. Ajigeuze reli ili treni ipite kwa maana afanye juhudi kuondoa uozo na mapingamizi ya upatikanaji wa huduma bora kwa faida yake na vizazi vijavyo.

Ni kweli CRDB na benki zingine wana matatizo lakini Tatizo kubwa lipo kwa wateja. "If you want to change the world you must change you first"

Wateja hovyo?
 
Tatizo unavihela vidogo kila saa unachungulia balance nani akuibie salari account yako acha ub..w...e..g..e
 
Hakuna bank iko vizuri Kama CRDB,ikitoake shida ujue kuna shida tu ya mitandao ambayo ina gusa bank zote hapa Tz. Kwajumla nawapenda sana wako juu.
 
CRDB wamesharidhika na wateja tena wamewazidi wanatamani wapungue. Hivi ni halali kulipishwa sh. 24,000/- kwa benk statement kisa ya miaka mitatu iliyopita, pamoja na hiyo sh. 24,000 unalazimika tena kulipia kila ukrasa sh. 1000! Huu ni wizi mkubwa sana, Serikali haina budi kupitia upya tozo hizi wanazotoza. Kulikuwa na huduma ya E mail statement sasa hivi hakuna tena japo makato kwa mwezi bado yanaendelea. Kwa mikoani siku za Jumapili na sikukuu ATM hawaweki hela hivyo kuwafanya raia wahangaike kama mbuzi wasiokuwa na mchungaji.
 
Crbd ni jipu lingine,yaan kuna vihera vidogo vidogo huwa vinayeyuka Kama theruji hahaha
 
Dah mimi leo n siku y tatu nasubiri tu salary lkn hawajaingiza mpaka dakika hii na ni mtumishi wa serikali hela. Zilitoka tarehe 24
 
  • Thanks
Reactions: Mss
CRDB ni mama au baba yako?
Una maanisha ahame huko si ndio eeh?

CRDB kweli wana vicharges vya ajabu ajabu. Wakati mwingine unakuta umekatwa ''ATM charge fees'' kwa siku hata tano mfululizo hata kama hujafanya transaction yoyote. Pesa huwa ni ndogo though na najua watu wengi huenda wasifuatilie. Lakini kama kwangu tu umepiga USD 7.5, assume wateja kama 5,000 wamepigwa, huu si mradi tayari?
 
Hawa jamaa walikuwa na huduma iitwayo E-banking ambapo walikuwa wakituma stayement kila mwisho wa mwezi, wameiondoa kimyakimya nahisi baada ya kuona wateja wanafuatilia wizi wanaoufanya. Kingine siku za sikukuu na mwisho wa wiki ATM zote wanaondoa hela kwa makusudi tu wamesahau kuwa ndio kipindi wateja wanahitaji huduma. Tabia hii kwa mikoani imekuwa sugu na hawajari kabisa
 
Back
Top Bottom