Kero zangu kwa CRDB wakala

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,792
15,693
Nimefanya huduma ya uwakala wa CRDB kwa takribani miezi 8 sasa na hizi ndio kero zangu;

Kero nyingi ziko based na ubovu wa mtandao/Customer Care

Sijajua kama tatizo ni hizi machine mpya tulizopewa ama ni tatizo la machine zote (POS), maana kipindi naanza niliwekewa chip ya Airtel, kero ya mtandao ilikuwa ni kubwa sana japo niko ndani ya eneo ya manispaa (mjini), yaani kwa mfano umepata wateja 50 kwa siku basi wateja 25 unaweza ukashindwa kuwahudumia kwa sababu ya kufeli kwa mtandao, na mtandao unafeli mara kwa mara kwenye malipo ya bill hasa luku, ikifuatiwa na ving'amuzi, baada ya kero hii kuonekana kubwa nikaenda ofisini kwao na kuomba kama kuna uwezekano wanibadilishie chip, na kweli wakanibadilishia wakanipa Voda lakini bado kero haikwisha japo ilipungua kidogo.

>Ni jambo la kawaida kununua luku na kuambiwa imefeli huku balance yako ikionekana imetoka, yaani kama float ilikuwa mil 2, umenunua umeme wa elfu 10, unakuta balance ni 1,990,000 lakini ukiangalia status ya kwenye transaction history inakwambia 'failed'

Baada ya status kuwa failed na balance kupungua unaamua kuwapigia ili ujue tatizo; bahati mbaya customer care kuwapata inaweza kukuchukua dakika 15 hadi nusu saa, wakati huo unahitajika kuwahudumia wateja wengine (na kumbuka asilimia kubwa ya wanaoendesha huduma hizi wanakuwa na biashara nyingine pia).

Sasa kwa mfano muhudumu wakati huo uko peke yako, na uko na wateja wengi huwezi ukaanza kuwapigia huduma kwa wateja ambao wanapokea baada ya dakika 15-30 huku wateja wengine wanasubiria huduma, wakati mwingine unalazimika kumrudishia pesa mteja ukiamini muamala umefeli, sasa ukitulia ukaamua kuwapigia ccare ndo unapochoka, watakwambia huu muamala umefanikiwa ila bahati mbaya token zilishindwa kuwa processed hivyo tunakutumia token ya mteja kwa njia ya sms, kumbuka hapo mteja pesa umeshamrudishia na kaenda kununua luku kwingine na pengine huyo mteja humfahamu. Kwahiyo hapo moja kwa moja unahesabu LOSS.

> Kisa cha Muamala wa startimes -- Jana nilikuwa nabalance hesabu zangu za siku nikaona kuna upungufu wa sh efu 6,nikawapigia ccare nikauliza mbona sijaelewa hii elfu 6 maana leo sijamuhudumia mteja wa namna hii na kwenye transaction history haonekani ila nimeukuta kwenye mini statement, muhudumu akakiri kuuona huo muamala na kusema huo muamala inaonesha kuna siku uliucomand ila ukawa pending, nikamuuliza siku gani, akashindwa kunitajia siku ila akasema jaribu kufuatilia miamala yako ya nyuma, nikafualia miamala ya kuanzia tar 1 July hadi Jana sikuona, yaani inamaana pengine ni muamala wa mwezi mmoja au zaidi iliyopita ila Jana ndio ukafanikiwa kununua kifurushi, kwa maana hiyo mteja alisharudishiwa pesa zake kwahiyo hapo ni LOSS ya kusababishiwa na CRDB.

> Kisa cha Mteja kutoa pesa mara3 bila majibu; kuna siku mteja kaingia kadi yake kwenye poss na kutoa laki 8, majibu yakarudi imefeli, akarudia tena mara 2 ikafeli tukaona tuache. Mimi kuangalia salio majibu yakawa hayarudi, kuangalia transaction history haionyeshi chochote, basi tukaamini miamala imefeli. Mteja kesho yake kwenye kuangalia salio ATM anakuta pesa imepungua sana, akaingia ndani kuuliza kulikoni, akaoneshwa transaction zake 3 za Jana za laki nanenane yaani jumla 2,400,000 . Na mimi sikugundua chochote maana hadi sikuhiyo ya pili bado mtandao uliendelea kugoma kuonesha salio wala transaction history. Mteja alinirudia akiwa na copy ya transaction zake za jana, ikabidi nichukue maamuzi ya kufunga safari na kwenda naye ofisi kuu kuthibitisha hilo, nikampatia pesa yake baada ya kujiridhisha, sasa nikajiuliza kama mteja angekuwa anasafiri ingekuwaje, au ningeamua kumkana kwamba nimemuhudumia ingekuwaje?

>Nikiendelea kwenye upande wa Customer Care, kuna namba ile ambayo ipo kwenye risiti zao ndio nilikuwa na kawaida ya kuitumia, sasa kuna siku niliwapigia kwa dakika 31 simu yangu ilikuwa bado haijapokelewa na muhudumu ghafla simu ikakata, kuangalia meseji naambiwa muda wa mauongezi umeisha, nikashangaa sana maana sikufikiria kwamba namba yao ya huduma kwa wateja inakula muda wa maongezi kama line za kawaida. Na sikuzote sikuweza kujua kwasababu huwa nna kawaida ya kujiunga muda wa mauongezi kwa mwezi na nnapewa dakika nyingi. Kesho yake nikawapigia na kufanikiwa kuwapata, nikaeleza shida yangu ikiwa pamoja na kuwasilisha hiyo kero yangu ya namba ya ccare kula muda wa maongezi, nikaambiwa ni kweli inakula, ila wana namba ya wateja ambayo ni free, ikabidi niombe anitajie hiyo free, sasa nikajiuliza kwanini wanaificha kwenye risiti zao haipo?

NB: Kuna kero nyingi nimekutana nazo kwenye huduma ya CRDB Wakala hapo nimeelezea chache tu kama mfano, mimi sio mgeni kwenye hizi huduma za kifedha hivyo hadi nimeamua kuandika hivi ujue nimekutana na kero za kutosha na nnaamini CRDB wanapitia pia JF, watatafuta namna wa kurekebisha haya.

Niwapongeze mitandao ya simu naona wao wameendelea kidogo hasa upande wa Customer Care/ Ubora wa Mtandao kwa mijini/ na Usalama wa pesa wa wakala. CRDB wana mengi ya kujifunza, yaani viloss loss vya ajabuajabu kwa CRDB imekuwa kawaida, tofauti na mitandao ya simu ambayo viloss inakuwa ni uzembe wako mwenyewe wakala.

NAWASILISHA.
 
Daaaa...machine za crdb zinasumbua sana hasa upande wa luku na kulipia visumbuzi.
 
Daaaa...machine za crdb zinasumbua sana hasa upande wa luku na kulipia visumbuzi.
Vipi Azam Pesa una experience nayo? Nafikiria kuitafuta kama iko vizuri ili mambo ya kulipia bill nitumie hiyo, huku kwenye pos ya crdb ibakie kuweka na kutoa tu
 
Nenda branch omba wakupe card kwa sasa zinatolewa baada ya malalamiko mengi ya mawakala network, kabla mteja hajaondoka angalia statment na mteja wa luku usirudishe hela asubiri token atatumiwa
 
Vipi Azam Pesa una experience nayo? Nafikiria kuitafuta kama iko vizuri ili mambo ya kulipia bill nitumie hiyo, huku kwenye pos ya crdb ibakie kuweka na kutoa tu
Hapana.na sizan kama wana machine
 
Nenda branch omba wakupe card kwa sasa zinatolewa baada ya malalamiko mengi ya mawakala network, kabla mteja hajaondoka angalia statment na mteja wa luku usirudishe hela asubiri token atatumiwa
Sorry, hiyo kadi inasaidia nini?
 
Back
Top Bottom