Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,499
- 4,211
Habari za asubuhi,
Moja kwa moja niende kwenye mada kuhoji uendeshaji wa hii bank maana huenda wahusika wameshaikatia tamaa maana malalamiko ya wateja yamekuwepo kwa muda mrefu lakini hakuna hatua zinazochukuliwa zaidi ya kuongeza huduma zisizo na msingi kila kukicha. baadhi ya kero zake ni kama zifuatazo.
1: Kuchukua muda mrefu kufungua account
Hivi kweli kwenye zama hizi za ushindani wa kibiashara na teknolojia kama Mpesa, TigoPesa, AirtelMoney e.t.c unawezaje kumwambia mteja nenda urudi baada ya siku saba?
2: SimBanking USSD menu
Hapa ndio balaa! yaani kwanza mpaka uweze kupata hii huduma utaambiwa nenda uje wiki ijayo! Kasheshe inaanzia pale unapotaka kupata huduma kwa njia ya simu kwa kubonyeza *150*03# unaambiwa muamala haujakamilika! Yaani Account ni yangu na pesa ni zangu lakini kupata taarifa zake mpaka niwe na salio kwenye simu! Upuuzi mkubwa! Sasa hiyo SimBanking ina maana gani? Mbaya zaidi miamala inayofanyika kwenye ATM hautumiwi taarifa zozote kwamba kuna kiasi fulani cha pesa kimetolewa! Je kama ni wizi unafanyika? Kwa kifupi SimBanking is a crap service.
3: Kupata kadi ya ATM
Hapa ni tatizo kubwa! Yaani utaambiwa nenda urudi wiki ijayo! Kweli kwenye karne hii ambapo ID zinakuwa printed papo hapo unamwambia mteja ondoka urudi siku fulani? Najua kuna issue za security lakini ndio mchukue wiki tatu kutengeneza kadi?
Kama ni security kwanini isitumike biometrics tu kama finger prints hata kwenye atm kurahisisha mambo na kuongeza usalama?
N:B CRDB msipojirekebisha mtapoteza wateja wengi sana