Moja kwa moja kwako kwenye mada.
Hatimaye ninakundikia wewe ushauri huu wa bure nikifahamu fika kuwa hujapungukiwa na washauri, na kuwa uko nao washauri walio mahiri kabisa, wenye kulipwa vilivyo kutokana na kazi hiyo.
Hata hivyo kumbuka mheshimiwa, Goliath lilikuwa jitu la kutisha (lenye silaha hatari) ambalo kwa uweza wake mola lilisimamishwa ni kijana mdogo aliyekuwa na kombeo na jiwe tu, zana duni kabisa.
Kwa taarifa zilizopo hadi sasa katika Afrika peke yake watu wapatao 109 tayari wamesha kufa kwa covid-19 na hii inaendelea kuongezeka kwa kasi kubwa zaidi:
COVID-19: Coronavirus hits 46 countries in Africa, kills 109 people
Italy pana wahanga zaidi ya 10,000 waliokwisha kufa hadi sasa. New York peke yake ni wahanga zaidi ya 1,000. China wao wametangaza rasmi kufanikiwa kuutokomeza ugonjwa huu.
WHO wanaonya kuwa katika wiki tatu zijazo tokea sasa tunaweza kuiona Afrika ikiwa katika hali mbaya sana. Labda hata kuwa ni mbaya zaidi kuhusiana na ugonjwa huu kuliko hata ilivyo ulaya na marekani kwa sasa. Hii ni kama hatua thabiti kabisa hazitachukuliwa pasipo na kuchelewa zaidi.. WHO wanazo sababu za kutosha kabisa kuendelea kutoa maonyo haya.
WHO wanasisitiza umuhimu wa 'social distancing' yaani kuwatenga watu walio wazima na walio waathirika ili hatua zichukuliwe. Hii ikiwa ndiyo njia pekee iliyozaa ushindi na kuonekana kisayansi kuwa sahihi zaidi.
Hii ni vita kubwa wala si ndogo na wewe ndiye jemedari wetu.
Walioambukizwa Uingereza ni pamoja na Malkia Elizabeth, Prince Charles, waziri mkuu Boris Johnson (watu wazito kabisa) na wengi wengine mashuhuri na hohehahe, wakubwa kwa wadogo duniani kote.
Ugonjwa huu unaweza kumpata mtu yeyote na wakati wowote.
Ugonjwa huu unatishia kwa dhahiri kabisa uwepo wetu kama taifa. Muda wa kuchukua hatua ni sasa kabla hatujachelewa mno.
Wapo wenzetu tunao fanana nao katika mazingira kama yetu kuweza kujipanga hata kuamua ya nini cha kufanya katika namna inavyofahamika zaidi kuliko kusubiria zahama hili linalokuja litufikie tukiwa tumemwachia Mungu. Kumwachia Mungu hakuna maana ya kutochukua hatua.
Kwa hali inavyokwenda mkuu, ilikuwa vyema ukarejea Dar es salaam au Dodoma (yaliko makazi yako rasmi) kwa ajili ya kuongoza mapambano haya sasa wewe mwenyewe.
Mikusanyiko yote kila mmoja kwa jina lake ni muda wa kuisitisha sasa. Hivi vijiwe vyote, viwe vya kahawa au tangawizi ni muda wa kuvifunga maana vinachangia mikusanyiko ambayo ndiyo njia kuu ya maambukizi.
Mkuu, penye nia pana njia. Tutie nia pamoja sote kama taifa tutashinda.