#COVID-19: Tuwajibishane

Ni hatari sana... Hatua madhubuti zinatakiwa zichukuliwa na siyo kupeana moyo bila vitendo...



Cc: mahondaw
 


Tunamaliza vipi Corona wakati mwenye kuweza kuamua ili tatizo liishe hawajibiki?

Hakuwa na mkakati wa kuzuia ugonjwa kuingia. Hana mkakati wala mikakati ya kuzuia ugonjwa kusambaa.

Ugonjwa unazidi kusambaa na watu wanazidi kufa.

Hadi lini mkuu?
 
corona ishakuwa mtaji wa kisiasa kazi kweli kwelii
chukueni hatua za kujikinga acheni lawama mnalaumu utafikiri hiyo corona imeletwa na magufuli
Kama corona hajaileta yeye kaileta nan?

Alipoambiwa afunge mipaka na viwanja vya ndege toka mwanzo alikubali?

Alipoambiwa afunge bar na kumbi za starehe alikubali?
Alipoambiwa azuie mabasi ya kutoka dar kuingia mikoan alikubali??

Mpaka sasa ni hatua gani madhubuti aliyochukua???

Unapimwa leo corona mwanza unasubiri vipimo viende dar mpaka virudi ushakufa,huo si ukichaa??

Think.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vita vinapigwana kisasa, the command post ni Chatto. Usually the command post inapaswa iwe established mahali ambapo ni safest place in the area. Save heavens zetu kwa sasa ni Chatto.
P

Tokea kwenye hiyo command post, what have we achieved?

1. Je ugonjwa haukuingia?
2. Je ugonjwa hausambai?
3. Iko mikakati gani kuzuia ugonjwa kusambaa?
4. Hii ya maombezi nayo ni sehemu ya mikakati yake?

Huyu ni vyema akabakia kwenye maombezi.

Ni muda wa jemedari mwingine.
 
Zitto, siungi mkono hoja, kwa sasa tuko katikati ya Mapambano, huu sii wakati wa kunyoosheana vidole kulauniana, kushutumiana na kutafuta mchawi tuwajibishane. Huu ni wakati wa kusimama pamoja, stand together united and fight as one.

P
Paschal hata Kama unataka ubunge kupitia CCM, lakini kwa hili acha unafiki. Kwanza nikuulize, Magufuli yuko wapi? Huko anafanya nini? Kwa nini sisi Wananchi tukimshauri hatusikilizi ila anataka tumsikilize yeye tu?

Mwisho tuambie kwa nini anafikiri ni haki sasa Watanzania tujifiche nyuma ya Mwenyezi Mungu na si wakati ule maiti zilipokuwa zikiokotwa kwenye viroba baharini, huku akina Lisu wakipigwa risasi zisizo idadi?

Kwa nini alisema, "tusitishane, kaugonjwa haka ni kadogo tu," huku akijua na kuona korona ikiuwa maelfu huko China, Italy, Ufaransa, Uingereza n. k.

Paschal kuwajibishana ni muhimu, na wa kwanza ni Mr. President.
 

Mkuu we are not that impotent.

Kwa nini ndege bado zinaruka? Kwa nini mabasi yanatembea? Kwa nini mikoa yenye waathirika haikuwa locked down? Na yote ya namna hiyo siyo ya wataalamu wa afya.

Aliyetufikisha hapa tunamjua indeed sasa katuchosha. Hana nia ya kupambana na ugonjwa huu.

Matendo yanaongea zaidi ya maneno.
 

Mkuu si ungejipa muda ukaelewa maana ya lockdown kwanza?

Lockdown haina maana ya watu kufungiwa vyumbani. Nchi zilizo kwenye lockdown, wakulima na shughuli muhimu zote zinaendelea wala hakuna watu wanaoteseka kwa kukosa chakula. Hizi tafsiri zenu mnapeana wapi?

Kabla ya ugonjwa kuingia serikali ilipaswa:

1. Kuzuia ndege na wasafiri tokea nchi zilizo kuwa na maambukizi.
2. Kuwaweka wageni wote tokea nje quarantine kwa siku 14 kabla ya kuwaruhusu kuingia nchini.
3. Kufunga mipaka kwa watu kupita (abiria) kasoro mizigo (kama kwingine wafanyavyo).

Hawakufanya hayo kwa uzembe wao japo waliambiwa sana. Ni kama wanavyoambiwa sasa hivi nini wafanye na bado hawachukui hatua na ugonjwa unazidi kusambaa.
 
Kila nchi ina njia zake,sio lazima Rais atoke kwenye tv atroti ndani ya ofisi kama museveni
Rais anaongoza nchi na wasaidizi wake wapo
Rais alitoa picha akiwa ikulu,mlitukana sana na kukebehi mpaka kufikia kusema hamtaki kujua Rais alipo
Kama marekani na maguvu yake wamekufa 3,000 hapa Tanzania unataka nani awajibishwe?Andika tu barua world bank tunyimwe misaada na mikopo kwa ajili covic 19,kwa sababu hatukusikiliza maoni yako
 
Mtaulinda uozo hadi lini!!!? Uongozi wa awamu ya tano mi uozo mtupu.
 
Yule mzee mbona ana roho mbaya hivi?Hashtuki tuuu!!!!
 
Zitto, siungi mkono hoja, kwa sasa tuko katikati ya Mapambano, huu sii wakati wa kunyoosheana vidole kulauniana, kushutumiana na kutafuta mchawi tuwajibishane. Huu ni wakati wa kusimama pamoja, stand together united and fight as one.

P
Sawa tusimame pamoja tupigane, shauri basi tupigane vipi
 
Zitto, siungi mkono hoja, kwa sasa tuko katikati ya Mapambano, huu sii wakati wa kunyoosheana vidole kulauniana, kushutumiana na kutafuta mchawi tuwajibishane. Huu ni wakati wa kusimama pamoja, stand together united and fight as one.

P
wewe nawe una uchama sana, stand together ipi! tangu kitambo wanashauliwa wafunge mipaka hawakusikia, nyinyi ndio hamtufai kabisa nchini,mnanidham ya uoga!
 
Paschal jibu maswali yangu, "like" ina maana gani!!? Haiwezi kuwa badala ya majibu.
Mkuu Zakaria, humu jf si mtu unajibu maswali kama jibu unalo la kujibu?, ukiulizwa swali kama huna jibu, kukaa kimya pia nalo ni jibu!.
Like zangu ni kukupa taarifa kuwa nimekusoma, mimi humu jf, mtu yoyote anayejibu hoja yangu anakula like.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…