TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 23,914
- 23,079
Aisee! Unajua, Wakuu wangu mnanistaajabisha sana sana!Pole ndugu yangu Nguruvi3, mimi nimeinua mikono. How does one argue with this...
View attachment 1707920
Fikiria mtu mzima na akili yake timamu anaanzisha mada jukwaa la GT lenye kichwa cha habari...
COVID-19 is historical in Tanzania: Why don't USA, UK, EU and others copy from TZ how to fight against Coronavirus?
How does one respond? Where does one start? What does one say? Oh, I rest my case!
Nimejifunza mengi kutoka kwenu, na sijachoka. Pia ni ninyi mlionifundisha namna bora ya kujadiliana na mkisisitiza ili niwe mshiriki mzuri na bora wa mijadala lazima nijikite kwenye hoja na si haiba, huluka, maringo, mbwembwe( kwa kifupi personality) za mtoa hoja.
Najiuliza, hivi maelekezo yenu yale ya kushiriki mjadala vizuri bila kushambulia utu wa mtoa hoja yalikuwa ya kunidhiaki ama sasa hivi mnajidhiaki wenyewe!?
====
Kwenye hoja yako ya historia.
Tulianza na covid19(2019), mwaka jana mwishoni tuna covid mpya ya Uingereza/Afrika Kusini (2020), juzi Ijumaa (2021) tumeambiwa kuna covid mpya na imegudulika huko Norway.
Kilichotokea mwaka jana nchini mwetu Tanzania unakijiua mbali na vitisho kutoka kwa ndugu yetu ( anajijua) wa humu jamvini kuwa watanzania tutapukutika na miili yetu kuzagaa mitaani! Mungu alitusimamia vitisho vikashindwa vibaya sana kama H.R. Clintoni na kura za urais wa US 2016! Ni historia hii, unataka hivyo hivyo hutaki hivyo hivyo!
Binafsi, mnazidisha sana wasi wasi wangu juu ya ninyi wakuu kughadhabishwa na wale wanao hoji ubora na ufanisi wa mbinu zinazotumika kukabiliana na CORONA hasa kwa ndugu zetu wa nchi za Ulaya magharibi na Amerika.
Poleni kwa msukosuko wa hali ya hewa huko Texas!