oops!Hayo mengi katika bandiko hakuna lililotoka nje ya hoja zako. Ni sahihi unapoamua kuyakwepa, lakini werevu wanatusoma.
Hee unashangaa hilo, inategemea unatazama sayansi kwa mtazamo gani.Mkuu Nguruvi3 , una matokeo ya mwaka mmoja mbele ya chanjo ambayo tangu ianze kutolewa haijafikisha mwaka!!!!?????? UNALIPWA NA NINI KUTETEA UBATILI KWA GHARAMA KUBWA HIVYO?
Integrity ya majadiliano inapotea tunapoanza kuamini mapambio! na nyasi bila kuwa na uwezo wa kuzielezaUmepoteza integrity ya majadiliano, naomba nikuache kwa kukumbia hivi...
Soma bandiko lako hapo juu! Haya mambo ni magumu hayahitaji ufahamu wa bahati nasibuHakuna sehemu nimekuhoji kwamba kwanini hujibu baadhi ya hoja, kama ipo nioneshe.
Hapana ! Sayansi inaeleza chombo cha China ilikuwa ni 'human error kutokana na miscalculation'Mkuu Nguruvi3, JE KILA PREDICTION HUTIMIA KWA USAHIHI WAKE 100%?
Juzi chombo cha China kimeanguka kinyume na matarajio na matamanio yao, je haikuwa sayansi?
Kuna dawa za asili hazina doubts, na hizi tunazijua. Dawa zinatokana na miti lakini si kila mti ni dawa.Unazoita nyasi ni organics ambazo nyingine zipo kila siku katika Milo yetu....
Ipo na hiyo tunaihitaji, hata hivyo hadi itakapokuwepo hatuwezi kuamini tu kwasababu kuna mtu kasema jukwaani. Tunataka maelezo ya nini kinafanyika, inafanyike na kwanini.Kipi kisichowezekana kwako? Kwamba hakuna uwezekano wa uwepo wa Sayansi iliyo bora kushinda hiyo uipiganiayo, na huku bado isiweze kutafsiri mfupa wa goti unaungaje pasipo kuguswa mgonjwa ndani muda mfupi?
Ya madagascar iliua sana hadi wakapiga magoti WHO.Dawa ya Madagascar kama haijaletwa hadharani, basi tambua kuwa haijakidhi vigezo vya mamlaka husika, sawa na Chanjo leo.
Itoshe tu.
Wataalam walioshauri walipoteza kazi, tukaambiwa wanastaafu. Wakaletwa wapiga debe tukaambiwa watalaamInasikitisha sana kuona jinsi ugonjwa huu wa COVID 19 ulivyotuathiri hata kwenye fikra na mitazamo yetu!
Shukrani kwa wanasiasa wetu leo ghafla kila mtu amekuwa nguli na mtaalamu wa afya na tiba... ghafla wataalamu wa afya tiba hawasikilizwi tena ushauri wao unabezwa, ghafla kila anayeshauri kufuata kanuni za tiba anabezwa kuwa ametumwa na mabeberu kutudhoofisha kiuchumi!
Huyu bwana tunayeongea naye kasema '' watu wapo Poa, kuna watu hawajawahi kuvaa barakoa''Ugonjwa umeua ndugu zetu kwa wingi tu lakini bado tunajipa jeuri kwamba tuko salama...
Bila data jibu lolote ni sahihi, kwamba kuna Corona au hakuna. Data ndizo zina prove kama hakuna hakuna prooflabda kwa sababu tumegoma kutangaza data tumejificha vichwa ardhini kama mbuni.
Hapa Jamvini waliaminisha India ndio wenyewe kwa nyungu. Leo hali ipoje? Dunia inakimbilia kuokoa haliHatutaki kupima, hatutaki social distancing, hatutaki barakoa, hatutaki chanjo yote haya tunasema ni mbinu chafu za mebeberu tutumie tiba zetu za asili.... Lakini ukihoji tafiti za kuthibitisha kwamba kupiga nyungu au kunywa bupiji zinatibu corona hupati majibu! Ile dawa tuliyotuma ndege Madagascar kwenda kuichukua sijui nayo iliishia wapi! Lakini tuko mstari wa mbele kupiga kelele dawa za mabeberu na kuwabeza wanaoziongelea kwamba wametumwa!
Ukizungumzia vaccine, social distancing and mask unaambiwa umetumwa na mabeberu.Tumekuwa taifa la kusikiliza zaidi blah blah za wanasiasa zaidi kuliko kujielimisha, kila kitu tumegeuza kuwa siasa kila mtu amekimbilia huko.... ndio maana leo darasa la 7 anamdharau PHD kuwa hana mchango wowote kwa Taifa (only in Tanzania).
Hakuna mahali nimesema nina uhakika. Nipo katika record nikisema sayansi ni WIP na chanjo ni sehemu yakeNguruvi3, naona kama unazungukazunguka na hoja zilezile zisizo na misingi iNi vizurimara ya kutetea.
1. Hakuna Sayansi iliyo nje kabisa ya Human Errors. Hivyo madai yako ya kuwa una hakika wa usalama wa chanjo baada ya mwaka mmoja ni Uongo.
Vita ya uchumi sikusema mimi! please uliza waliosema kama wana majibu. Ninachosema hapa ni kuwa vita ya uchumi gani na watu wasioweza kujenga vyoo hadi balozi wa Japan akabidhi matundu hayo?2. Hoja ya Vita ya Kiuchumi wewe binafsi unaelewa aliyetoa hakuwa na maana hiyo unayoing'ang'ania Leo. Umekula kiapo cha Upotoshaji.
Ninaamini kabisa katika dawa za asili. Wamasai ni mfano mzuri sana.3. Hakuna mtu amesema kila mti ni Dawa, huu ni upotoshaji mwingine. Kama unakubali zipo tiba asilia nje ya sayansi ya leo, kukataa Nyungu kisa imesemwa na mtu unayemchukia, hilo ni tatizo lako si nyungu. Nyungu zipo hata kabla haijasemwa na huyo mtu.
Mamlaka itaahidhinisha nini? Dawa zinafanyaiwa tathmini maabara si katika majukwaa ya siasa4. Nilishasema mwanzo kuwa, Mamlaka haijaidhinisha bado au haitaidhinisha kabisa Chanjo. Ukiona kimya ujue kwamba bado hawajapata vigezo vya kuiidhinisha chanjo. Umeshupaza shingo mno.
chuki kusema tubadilike na tuwe sehemu ya dunia!5. Punguza Chuki Mkuu, ukishindwa kabisa jaribu kuzificha.
Watanzania hawafi kama yanayotokea India, Je Serikali inaficha vifo? Naona kuna wengi wanaopenda kuona Watanzania wanapoteza maisha yao kisa tu ku-prove hoja zao. Hii dunia ina mambo mengi Watanzania wanatakiwa kuwa makini hata na majirani zetu tu. Alikuwepo JK Nyerere ambaye alishindwa kukubaliana na Majirani zetu wa Kenya hadi pale alipotokea Moringe na kutoa ushauri, lakini tunaona hivi sasa jinsi Serikali inavyowakumbatia kama wao ndio wakombozi. Tuipende nchi yetu na hakuna taifa lolote lile ulimwenguni linaloweza kuwawezesha Watanzania kutoka kwenye umasikini wakati ina kila kitu.