Wakati uongozi wa Yanga ukiitaka Wizara ya Nishati na madini kupitia Shirika lake lenye dhamana ya kusambaza umeme kuhakikisha hali ya umeme inakuwa katika ubora unaostahili leo jioni/usiku ili mtanange uweze kupigwa bila vikwazo wenzao wa upande wa 2 wameendelea kuja na sababu lukuki za utangulizi.
Baada ya kulalamikia Card nyekundu za kujitakia walizojipatia wachezaji wao wakidai kuwa walionewa sasa wamekuja na kali zaidi,kupitia Msemaji(ovyo) wao Ezekiel Kamwaga Simba imemlalamikia Mwamuzi aliyepangwa kuchezesha mechi hiyo Mathew Akrama ya kwamba hawana imani naye,nanukuu...
Tunajua sekretarieti ya TFF ndiyo huwa inahusika kupanga marefa, na ndiyo hii hii ambayo tunailalamikia haitutendei haki, sasa sisi tunamuomba mambo mawili makubwa Akrama, kwenye mechi ya Simba na Yanga; kuna watu huwa wanapoteza maisha wakifungwa. Kuna watu huwa wanapoteza fahamu, wanaweka rehani nyumba zao, mali zao kucheza kamari, na wanaliwa.kuna viongozi wengine wamewahi kutimuliwa madarakani kwa sababu ya kufungwa na Simba na Yanga.
Kwa hiyo, hii mechi ina mambo mengi sana, sasa sisi tunamuomba Akrama asiue watu, asifanye watu wakaliwa, asifanye watu wakapata mateso yasiyo na sababu"...mwisho wa kunukuu.
Binafsi napenda kumkumbusha kuwa kama mtu atazimia au kupoteza maisha kwa team 1 kati ya hizi 2 kufungwa ni yeye na mshtuko wake na systems za mwili wake ku'fail Mwamuzi kama Mwamuzi hana uwezo wa kuzuia hili kutokea kama ni lazima litokee,sawasawa na wale wanao'bet kwa kuweka rehani Mali zao.
Ninaona dalili za Viongozi wa Simba kutoiamini team yao ndani ya uwanja,ni kama vile wanaona nafasi yao ya kuifunga Yanga leo ni finyu sana na ndo maana wameamua kuja na mwendelezo wa sababu za utangulizi ili wanalolitilia shaka likitimia basi wapate cha kujitetea mbele ya mashabiki,wapenzi na wanachama wao, walianza na Card ya Okwi,wakaja na Card ya Maftah na sasa wameingia kwa Refa atakayechezesha mechi ya leo, what is this?