Corona: Utamaduni wa kupenda kubishana bila sababu umetufikisha hapa

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,608
8,746
Tuna kundi kubwa sana kwenye jamii yetu ya watu kupenda kubishana bila kuwa na data zozote wala ushahidi. Kubishana ni hobby ya watu wengi hivyo tusishangae wakati mwingine hata kwa viongozi kuna mabishano ambayo hayana msingi.

Kuhusu Corona tunaweza kubishana kwamba kufunga biashara hatuwezi kwasababu tuna data lakini kubishana kama kuna Corona Tanzania ni upendaji wa ligi za mabishano lakini hoja ya kutokuwa na corona Tanzania ni upendaji wa mabishano yasiyo na msingi. Lakini vilevile kama tunavyo agiza chanjo nyingine tuagize chanjo za Astrazenica kama Uganda, Kenya na nchi nyingine. Kama tuna hoja za msingi za kiusalama tutoe data na sababu za kukataa dawa ambazo zinaokoa maisha ya watu badala ya kubishana tu bila msingi.

Nchi nyingi sana Duniani zinapenda wananchi wao kama sisi tukumbuke mpaka miaka ya 1980's kulikuwa wa watu wanapata ukoma hasa mikoa ya kati mpaka pale tulipoanza kuchanja. Wengine tusilazimishwe kukataa chanjo wakati wazazi wetu wanakaa bila amani. Kupata tatizo kwa chanjo ni bora sana kuliko kupata corona kama wewe ni mtu mzima. Nasema hivi kwasababu hakuna data za ubaya wa chanjo lakini corona inaua.

Utamaduni wa mijadala mizuri na inapunguza ugomvi lakini kubishana bila sababu kwenye maisha ya watu hatuwezi kufanya kama vile ni hobby zetu. Kuna wananchi wanakufa sasa kwa sababu ndogo sana kama kunawa mikono, kuvaa barakoa, na kukaa mita moja kwasababu ya watu wanaopenda ligi za mabishano na sifa za kushinda mijadala.

Tujiulize kama Watanzania binafsi tumefanya nini kusaidia maisha ya watanzania . Sio serikali lakini sisi binafsi kila mmoja umefanya nini kusaidia mtu.
 
Elimu ndogo inawafanya vijana wa ufipa wabishane bila sababu
 
Ubishi usio na msingi watu wanateketea! Halafu dhana kwamba huu ugonjwa hauathiri vijana imeongeza tatizo; wengi hawajali lakini wasijue ni vector wa kuusambaza kwa makundi hatarishi kama wazee na wenye maradhi nyemelezi.

In short, tuna kizazi cha kutojali maisha ya wengine. Ni zaidi ya uhalifu na ndipo hapo serikali ilitakiwa iingilie kati kuokoa the minority risky groups ila ndio hivyo ni as if "waache wafe hawana faida".
 
Ni ile kusema mwenye macho haambiwi tazama,na pia akili kumkichwa.
 
Mtu mmoja hapaswi kuwanyima watanzania haki ya kuishi. Yanayoendelea Tanzania ni unyimivu wa haki ya kuishi. Endapo kuna watu hawahitaji chanjo, wasilizamishwe, ila wanaohitaji wawekewe mazingira ya kuipata. Haiwezekani tuachwe tufe kwasababu tu ya imani ya mtu. Huu ni unyimivu wa haki ya kuishi na ni ukatili dhidi ya ubinadamu.
 
Waimba pambio ndio wanaotuvurugia taifa kwa mgongo wa maslahi kutoka kwa wanaowatuma,kama sio kuwatumia kufikia kuyapata maslahi yao.

Way forward ni kuwatolea uvivu tu. Hakuna namna nyingine.
 
Back
Top Bottom