Corona imekuwa mradi wa Serikali au Mradi wa watu? Wanaowekwa karantini walalamikia bei kubwa ya hoteli wanazopelekwa

Mimi nadhani wangebaki huko huko walipo.
Maana hata wakikaa karantini na ikigundulika wana corona basi lazma tujue ni janga letu hilo na Idadi ya wagonjwa itakuwa imeongezeka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mwanafunzi anayerudi nyumbani kutoka masomoni atapata wapi pesa za kujikarantini kwenye mahoteli makubwa makubwa, acheni hizo siyo kila arudie home amejaza madolari kwenye begi
 
Pdidy,
Huyo Ummy Mwalimu mwenyewe mnafiki pamoja na aliemteua, anajifanya hajui/anashangaa na wakati hiyo deal amecheza Makonda huku akiwaahidi kuwapelekea mgao, na kwa akili ya viongozi wa serikali hii wanadhani polisi wanaweza kulinda washukiwa wa Covid19 kwa kutumia virungu, kwamba wao hawawezi kuambukizwa,, na wao polisi wakishatumwa kazi huwa haufikirii risk inayowazunguaka
 
Sky Eclat,
Labda baadaye watasaididiwa na serikali maana kwa gharama hizo za hotel, ni wazi kuwa baada ya karantini mtu atajikuta anadaiwa fedha ambazo hawezilipa!
 
Labda baadaye watasaididiwa na serikali maana kwa gharama hizo za hotel, ni wazi kuwa baada ya karantini mtu atajikuta anadaiwa fedha ambazo hawezilipa!
Wewe acha hela yenyewe ughaibuni ni ya kucheza upatu baada ya child benefits.
 
Wewe acha hela yenyewe ughaibuni ni ya kucheza upatu baada ya child benefits.
Mimi nadhani serikali itawasaidia maana kama mtu atakaa hotel kwa mfano ya TZS 100,000 kwa siku, kwa hiyo ni zaidi ya TZS 1.4 ukiweka na huduma zingine za chakula n.k.

Si rahisi watu wote kumudu gharama hizo. Hata kule Entebe wasafiri wamelalamikia uamuzi wa kuwaweka karantini katika hoteli za bei ya juu!
 
Hatari sana...

Hizo sehemu zilitakiwa zijengwa temporarily pembeni ya mahospitali makubwa.
Na siyo kwenda kuwarundika kwenye ma-hoteli ya kifahari.

Waliyokuja na hayo maamuzi najua wamewaza kwamba, kama wanauwezo wa kusafiri nje watashindwaje kulipia kwenye hizo hoteli.



Cc: mahondaw
 
Sio mradi ukiangalia kwa jicho la tatu ni namna pia ya kuwafanya watu wasije Tanzania kwa sasa mana hoteli za kishua na gharama zako so itawafanya wengi wasitishe safari kuepuka gharama kiasi falni watu waoingia watapungua automatic tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom