Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,314
- 33,108
1. Wahi kununua Mask kwa familia, mlipuko ukianza hizo Mask hazitaweza kupatikana kiurahisi
2. Nunua hand sanitazer toka duka la dawa, hizi ni tissue zenye spiriti/alcohol ambavyo unavitumia kujipaka mikono kila mara unapohisi umegusa sehemu usiyoiamini
3. Kila mara unapogusa sehemu nyingine nje na kwako, hakikisha unanawa mikono kwa sabuni na kupaka sanitazer,
4. Usijiguse usoni hovyo hovyo kabla ya kunawa mikono yako kwa sabuni na kupaka sanitazer (spirit) ukiwa katika mazingira yanayo kufanya uguse vitu kama vitasa, kuta, milango inayotumiwa na watu wengi. Virusi vinasambaa kwa njia ya hewa, kwa mikono yetu, au kwe vitu vingine tunavyovitumia,
5. Acha kabisa tabia ya kusalimiana kwa kupeana mikono mpaka mlipuko utakapoisha duniani
6. Kama ikitokea kuwepo mtu atayekutwa na Corona Virus nchini, jitahidi sana kujizuia na safari zisizo za lazima! Jitahidi kuwa na mahitaji ya lazima kama chakula ya kutosha nyumbani yanayoweza anglau kukutosha kwa miezi mitatu au zaidi
7. Kwa wenye usafiri binafsi, katika kipindi cha mlipuko jitahidi kutumia usafiri wako unaposafiri na jiepushe kubeba abilia usiojua wanatoka wapi
Ukiweza kutimiza hayo masharti, utailinda familia, jamii na taifa letu kwa janga ili.
HII NI KWA KUJILINDA TU, KUMBUKA MPAKA SASA HAKUNA CORONA VIRUS NCHINI
chanzo:From Dr. Kasilima - Public Health Specialist
KINGA BORA KULIKO TIBA