#COVID19 Corona: Bila Barakoa huingii stendi ya Magufuli

Too late. Wasianze kutisha raia

Too late what do you mean? What should have been early?

Kuwataka watu kuchukua tahadhari ni kuwatisha?

Haya si madhara halisi ya kutokutangaza sababu za vifo vya watu kwa kuficha ukweli?
 
Acha wahudumie wateja jamani. Mbona nauli imepanda na wateja wanalipa...
 
Kwamba?

"Sikubaliani na msimamo aliouchukua Magufuli dhidi ya corona lakini huenda ndio msimamo uliokubalika na wananchi wengi zaidi, watanzania wengi tunapenda shortcut"

Badilisha pote penye "wengi" kuwa "wajinga."
 
Acha wahudumie wateja jamani. Mbona nauli imepanda na wateja wanalipa...

Kuna siku mtahitaji mhudumiwe na maji ya kuchambia. No wonder hata katiba mpya tunasubiri kuhudumiwa.
 
Kuhimizana kuvaa barakoa bila kupeana elimu ya matumizi sahihi ya uvaaji wa barakoa sijui inasaidia vp kuzuia maambukizi ya corona.
 
TUVAE BARAKOA ILI KULINDA WENGINE. KAMA WEWE HUAMINI CORONA IPO JARIBU KUWAHESHIMU NA KUWALINDA WANAOAMINI KUWA IPO.
 
TUVAE BARAKOA ILI KULINDA WENGINE. KAMA WEWE HUAMINI CORONA IPO JARIBU KUWAHESHIMU NA KUWALINDA WANAOAMINI KUWA IPO.
Sasa ulinde wengine ki vp wakati kila mtu mwenyewe ndio anatakiwa kujilinda, sasa unataka mtu mwengine avae barakoa ili akulinde wewe? Hata kwenye ukimwi ni wewe ndio unatakiwa uzingatie condom na si kutegemea mwengine.
 
Kwa Tanzania watu waliaminishwa kuwa Corona haipo. Kuvaa barakoa wanaona kama adhabu ndio maana nawaambia kama wewe huamini Corona ipo vaa kuwalinda wengine.
 
Huko mkoani kwetu bila barakoa dukani haupewi hata chumvi
Unadhani inasaidia katika nini hilo jambo? mfano na huku mkoani kwangu kwamba ukitaka kwenda stendi ya Magufuli au Muhimbili ndio nibebe barakoa ili tu niweze kuruhusiwa kuingia ndani ila leo nikienda kusngalia simba na yanga sina haja ya kubeba barakoa, sasa hapo tunafanya nini?
 
Kwa Tanzania watu waliaminishwa kuwa Corona haipo. Kuvaa barakoa wanaona kama adhabu ndio maana nawaambia kama wewe huamini Corona ipo vaa kuwalinda wengine.
Watu hawajaaminishwa bali wamepewa uhuru, huo uvaaji wa barakoa ulikuwa kwa kiasi gani serikali inasema corona ipo? watu walikuwa wanajificha kwenye daladala wasionekane na traffic kipindi kile cha level seat ndio hao unasema wameaminishwa hakuna corona?

Vaa barakoa ujilinde mwenyewe na sio kutegemea mwengine avae ili akulinde wewe.
 
Mkuu kwani ukivaa barakoa utapungukiwa nini? Unataka wafe wangapi ndio muanze kuvaa barakoa?
 
Kuna watu ndani ya nchi hii hawajaguswa kabisa na corona, yaani si rafiki au ndugu au mfanyakazi mwenzie aliyeguswa na huyu mdudu.
Lakini kuna watu utadhani waliwekwa wa mfano; Unakuta yeye mwenyewe alishanaswa akanusurika , mara ndugu ,mara rafiki ,,na baadhi yao wamepoteza maisha.
Nawashauri mjikinge na huu ugonjwa kwa jinsi taratibu zake zinavyoelekezwa. Kama unashusha nett kujikinga na mbu,, basi kwa corona vaa barakoa kwenye watu wengi au unapoongea na mtu uso kwa uso na unawe mikono.
Chanjo imetamkwa ni hiari, ni vema mtakaopata nafasi ya kuchanja mkaitumia hiyo nafasi. - Siasa zisitangulizwe mbele ( hapa namaanisha kwa baadhi wanaopinga matumizi ya njia za kitaalamu kwasababu wanadhaji ni kama kumsuta Maghufuli). Hizo ni siasa tu, nyie chukueni njia zilizo sahihi.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…