#COVID19 Corona: Bila Barakoa huingii stendi ya Magufuli

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,226
35,151
Kuanzia Jumatatu bila kuvaa barakoa stendi ya Magufuli hakuingiliki tena.

Hata hivyo inashangaza kwanini kuwataka wenye mabasi kuwa na sanitizers kwa ajili ya abiria.

Kama ilivyo kwa barakoa, afya ya mtu ni wajibu wake mwenyewe. Hizi za kutwishana majukumu ya wengine ndiyo chanzo cha kupalilia jamii isiyokuwa na uwajibikaji kwenye mambo yake yenyewe.

Hatua zaidi kudhihibiti misongamano isiyo kuwa na tahadhari itapendeza zaidi.

Chanzo: ITV Habari.
 
Ila Tanzania kuna ujinga mwingi. Elimu bado haijasaidia kabisa watu. Kujikinga tu ugonjwa fulani ni jambo linahitaji mjadala kabisa. Mbona Ukimwi Kipindupindu Malaria nk matangazo ya tahadhari yapo miaka mingi mbona hampigi kelele?

Yaleyale ya mwenda zake unajifukiza halafu unatoka hapo na mipua na midomo wazi unaenda kuhemea na kukoholea wenzio.
Guys hii ni tahadhari tu. Na ni jukumu la serikali kutoa tahadhari hizo. Kesho mtakuja humu humu mara ooh serikali iingilie kati.
 
Hakuna mpumbavu wakuenzi huo ujinga ambao ye mwenyewe ulimponza Covid19 ikampiga
Mkuu ukweli mchungu ni kwamba wengi zaidi bado wanamuenzi, kama upo Tanzania jiulize maswali haya:
  • Hapo mtaani kwenu ni watu wangapi wanavaa barakoa ?
  • Hapo mtaani ni watu wangapi wanapeana social distance ?
  • Kwenye mabasi na vyombo vingine vya usafiri ni watu wangapi wanavaa barakoa ? Hayo mabasi yana social distance au yamejaza nyomi kama kawaida.
  • Kwenye viwanja vya mpira kuna social distancing ?
  • Mara ya mwisho kusikia kampeni ya kuelimisha watu kuhusu corona umeisikia mtaani kwenu lini ?
  • Watoto wa shule wanapewa elimu ya kujikinga na ugonjwa huu ?
  • Watu wakienda bar na club wanachukua tahadhari zozote ?
  • Katika rafiki au ndugu zako 10 ni wangapi wapo tayari kupokea chanjo ya corona ?
  • Lini serikali imetoa takwimu rasmi zinazoeleweka kuhusu maambukizi ya ugonjwa huu , zaidi ya kusomewa tu taarifa haraka haraka ambazo tuliambiwa tuna wagonjwa 100, wapo mkoa gani hatujui ? Taarifa mbona hazijafika WHO ?
Serikali ya sasa inachofanya ni kuiaminisha dunia kwamba tupo serious kwenye haya mapambano ili tupate mikopo na tusitengwe ila kiuhalisia ni kama tunaendelea vile vile, wananchi ndio kabisa wanaenzi yale yale ya mwendazake, sana sana utakuta raia wa kigeni ama wale wenye kipato cha kati na kwenda juu ndio wanavaa barakoa na kujitahidi kunawa mikono na kufuata ushauri mwingine wa wataalam wakiwa kwenye shopping malls ama migahawa mikubwa.

Sikubaliani na msimamo aliouchukua Magufuli dhidi ya corona lakini huenda ndio msimamo uliokubalika na wananchi wengi zaidi, watanzania wengi tunapenda shortcut !
 
Kuanzia Jumatatu bila kuvaa barakoa stendi Magufuli hakuingiliki tena.

Hata hivyo inashangaza kwa nini kuwataka wenye mabasi kuwa na sanitizers kwa ajili ya abiria.

Kama ilivyo kwa barakoa, afya ya mtu ni wajibu wake mwenyewe. Hizi za kutwishana majukumu ya wengine ndiyo chanzo cha kupalilia jamii isiyokuwa na uwajibikaji kwenye mambo yake yenyewe.

Hatua zaidi kudhihibiti misongamano isiyo kuwa na tahadhari itapendeza zaidi.

Source: ITV Habari.
Too late. Wasianze kutisha raia
 
Mama anatafuta hela za msaada kwa mgongo wa korona. Kashindwa kukusanya Kodi.

Ndiyo maana Mdude kaahidi kumnyoa huyu mama kwa wembe.

1625294827876.png
 
Kuanzia Jumatatu bila kuvaa barakoa stendi Magufuli hakuingiliki tena.

Hata hivyo inashangaza kwa nini kuwataka wenye mabasi kuwa na sanitizers kwa ajili ya abiria.

Kama ilivyo kwa barakoa, afya ya mtu ni wajibu wake mwenyewe. Hizi za kutwishana majukumu ya wengine ndiyo chanzo cha kupalilia jamii isiyokuwa na uwajibikaji kwenye mambo yake yenyewe.

Hatua zaidi kudhihibiti misongamano isiyo kuwa na tahadhari itapendeza zaidi.

Source: ITV Habari.
Safi sana. Taifa lazima lijali afya za watu wake. Nadhani hili liwe nchi nzima
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom