Connect dots hapa kuhusu Jaji Mujulizi na Kikwete

Connect dots hapa kuhusu Jaji Mujulizi na Kikwete

FaizaFuska mbona unatetea mwizi kwa kutaja mwizi mwingine?! Kwani kila tuhuma ya serikali ya JK lazima wewe uijibu au uko JF kwa kazi hiyo?
Too harsh bro,punguza ukali wa maneno, japo tunatofautiana kimitazamo mara kwa mara na FaizaFoxy ila sidhan kama ashawah kumtukana mtu,binafsi huwa nna conversations nyingi zinazopingana nae ila matusi hapana
 
FaizaFuska mbona unatetea mwizi kwa kutaja mwizi mwingine?! Kwani kila tuhuma ya serikali ya JK lazima wewe uijibu au uko JF kwa kazi hiyo?

Ukiona mtu anaanza matusi ujuwe hoja imemshinda.
 
Magamba ni genge la wahuni , wezi na walaghai...kiongozi wenu kikwete ni janga lisilo na mfano.

Azimio la Tano: Linasomeka; "Bunge linaazimia kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aunde Tume ya Kijaji ya Uchunguzi kuchunguza utovu wa maadili dhidi ya Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania"

Azimio hili nimelipokea, tumelijadili hata hivyo, itabidi tufuate utaratibu wa kikatiba na kisheria wa kushughulikia masuala ya namna hiyo. Inatakiwa suala kama hili lianzie kwenye Mhimili wa Mahakama yenyewe na siyo kwa Rais au Bunge. Tume ya Mahakama ndiyo yenye mamlaka ya kumtaka Rais aunde Tume ya Kijaji ya kumchukulia hatua Jaji yeyote pale inaporidhika kuwa amepoteza sifa za kuendelea kufanya kazi hiyo. Nashauri suala hili tumuachie Jaji Mkuu wa Tanzania alishughulikie atakavyoona inafaa.

Wala halishghulikii yeye kawawwachia wenyewe mahakama na kaelezea kawaida yake huwaje, majaji watatu, mmoja kutoka nje ya nchi na huyo wa nje ya nchi ndiye anakuwa kiongozi wa hao wengine.

Kikwete angeamuwa yeye si ndiyo ingekuwa mwao. Hapo hauingilii Mhimili wa mahakama na mnakuja kudanganya eti "ndio anatakiwa kuwajibishwa na mamlaka yake".
 
Kuna mtoa matusi mashuhuri kama wewe hapa jf?
Yaani faiza foxy silaha yako kubwa ni matusi, vijembe na mipasho kama mwenyekiti wenu wa magamba

Vipi Kuhusu Jaji Ruhangisa yeye hausiki na habari ya mleta mada?
 
Hivi na wale Maaskofu wa Kanisa Katoliki waliotajwa na kulamba kutoka kwa Ruge, Kanisa Katoliki linasemaje?

Maana Kikwete karusha hilo, halafu Kikwete kaniacha hoi, eti wachungaji sijui Mashehe, hili yeye hayumo. Kulikuwa kuna shehe pale? kwa vijembe hajambo.
Wewe unafurahia nini nchi kiyumbishwa na hawa wezi unaowatetea kila siku??? au ashik za bungeni zile mbunge alisema hata wewe unazo??
 
Kwa madhumuni ya kuweka Uhuru wa mahakama Rais hana mamlaka ya kutengua uteuzi wa Majaji

Hukunielewa. Hatengui nafasi ya Jaji. Anatengua nafasi ya Katibu wa Tume ya kutunga she ria. Hivi ni vitu viwili tofauti
 
Wacha uongo, wewe kila uongo unaolishwa unakuja kuutupia hapa, hata hutumii akili yako hata kiduchu basi, Mbona Ruhangisa hujamtaja, au na yeye si jaji? soma:


Azimio la Tano: Linasomeka; “Bunge linaazimia kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aunde Tume ya Kijaji ya Uchunguzi kuchunguza utovu wa maadili dhidi ya Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania”

Azimio hili nimelipokea, tumelijadili hata hivyo, itabidi tufuate utaratibu wa kikatiba na kisheria wa kushughulikia masuala ya namna hiyo. Inatakiwa suala kama hili lianzie kwenye Mhimili wa Mahakama yenyewe na siyo kwa Rais au Bunge. Tume ya Mahakama ndiyo yenye mamlaka ya kumtaka Rais aunde Tume ya Kijaji ya kumchukulia hatua Jaji yeyote pale inaporidhika kuwa amepoteza sifa za kuendelea kufanya kazi hiyo. Nashauri suala hili tumuachie Jaji Mkuu wa Tanzania alishughulikie atakavyoona inafaa.

Wala halishghulikii yeye kawawwachia wenyewe mahakama na kaelezea kawaida yake huwaje, majaji watatu, mmoja kutoka nje ya nchi na huyo wa nje ya nchi ndiye anakuwa kiongozi wa hao wengine.

Kikwete angeamuwa yeye si ndiyo ingekuwa mwao. Hapo haingilii Mhimili wa mahakama na mnakuja kudanganya eti "ndio anatakiwa kuwajibishwa na mamlaka yake".


Hamna hata haya?

Wewe na Kikwete wako ndiyo waongo na wapotoshaji wakubwa.
Niliwahi kuandika hii kitu , ila sikujua kama huyo Mahabuba wako Kikwete ana mahusiano ya kifisadi na mujuluzi...
Jana tulimsikia Rais JK akishindwa kutoa maamuzi ya azimio la bunge la kuwavua ujaji majaji wawili (Ruhangisa na Mujuluzi).
Je Rais kushindwa kuwawajibisha Majaji waliopokea mgao wa fedha za escrow yupo sahihi kikatiba?
Je kutokana na ibara ya 110(6) ya katiba ya 1977 ,JK amekwepa kuunda tume ya kijaji kama katiba inavyompa hayo mamlaka na kumsukumia mzigo jaji mkuu?

"110 (6) Iwapo Rais anaona kuwa suala la kumwondoa Jaji kazini lahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mambo yatakuwa ifuatavyo:-

(a) Rais atateua Tume ambayo itakuwa na Mwenyekiti na
Wajumbe wengine wasiopungua wawili. Na huyo
Mwenyekiti na angalau nusu ya Wajumbe wengine wa
Tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni Majaji wa
Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchi
yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola.

(b) Tume hiyo itachunguza shauri lote halafu itatoa taarifa
kwa Rais kuhusu maelezo ya shauri lolote na
itamshauri Rais kama huyo Jaji anayehusika
aondolewe kazini kwa mujibu wa masharti ya ibara hiikwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya
tabia mbaya.

(7) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara
ndogo ya (6) itamshauri Rais kwamba jaji ambaye habari zake
zimechunguzwa na hiyo Tume aondolewe kazini kwa sababu ya
kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine
yoyte au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoa
kazini Jaji huyo anayehusika.

(8) Ikiwa suala la kumwondoa Jaji kazini limepelekwa kwenye
Tume kwa ajili ya uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibara
ndogo ya (6) ya ibara hii, Rais aweza kumsimamisha kazi Jaji
huyo anayehusika, na Rais aweza wakati wowote kufuta uamuzi
huo wa kumsimamisha kazi Jaji huyo, na kwa hali yoyote uamuzi
huo utabatilika ikiwa Tume itamshauri Rais kwamba jaji huyo
asiondolewe kazini.

(9) Masharti ya ibara hii yatatumika bila ya kuathiri masharti ya
ibara ndogo ya (12) ya ibara ya 109 ya Katiba hii.”

Wenye ujuzi zaidi tunaomba tafsiri zaidi ya hili jambo.
Aksante.
 
Back
Top Bottom