Rais Kikwete kuwawajibisha majaji-Escrow

Rais Kikwete kuwawajibisha majaji-Escrow

asakuta same

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2011
Posts
14,829
Reaction score
5,041
Jana tulimsikia Rais Kikwete akishindwa kutoa maamuzi ya azimio la bunge la kuwavua ujaji majaji wawili (Ruhangisa na Mujuluzi).

Je, Rais kushindwa kuwawajibisha Majaji waliopokea mgao wa fedha za Escrow yupo sahihi kikatiba?

Je, kutokana na ibara ya 110(6) ya katiba ya 1977, Kikwete amekwepa kuunda Tume ya kijaji kama Katiba inavyompa hayo mamlaka na kumsukumia mzigo Jaji Mkuu?

"110 (6) Iwapo Rais anaona kuwa suala la kumwondoa Jaji kazini lahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mambo yatakuwa ifuatavyo:-​
​
(a) Rais atateua Tume ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili. Na huyo Mwenyekiti na angalau nusu ya Wajumbe wengine wa Tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni Majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchi yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola.​
​
(b) Tume hiyo itachunguza shauri lote halafu itatoa taarifa kwa Rais kuhusu maelezo ya shauri lolote na​
itamshauri Rais kama huyo Jaji anayehusika aondolewe kazini kwa mujibu wa masharti ya ibara hiikwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya.​
​
(7) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (6) itamshauri Rais kwamba jaji ambaye habari zake zimechunguzwa na hiyo Tume aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoa kazini Jaji huyo anayehusika.​
​
(8) Ikiwa suala la kumwondoa Jaji kazini limepelekwa kwenye Tume kwa ajili ya uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (6) ya ibara hii, Rais aweza kumsimamisha kazi Jaji huyo anayehusika, na Rais aweza wakati wowote kufuta uamuzi huo wa kumsimamisha kazi Jaji huyo, na kwa hali yoyote uamuzi huo utabatilika ikiwa Tume itamshauri Rais kwamba jaji huyo asiondolewe kazini.​
​
(9) Masharti ya ibara hii yatatumika bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (12) ya ibara ya 109 ya Katiba hii.​

Wenye ujuzi zaidi tunaomba tafsiri zaidi ya hili jambo.
Aksante.
 
Uliwahi kumsikia wapi Kikwete akitaja kifungu chochote cha Katiba?

Hatumii na wala hasomi katiba utakuwa unamuonea ukianza kuleta vifungu vya katiba hapa.

Kumbuka hata watuhumiwa wa EPA aliwasamehe kinyume cha katiba, Rais wa Tanzania anamamlaka ya kusamehe wale waliokwisha hukumiwa na si watuhumiwa ndivyo katiba inavyosema.
 
Uliwahi kumsikia wapi Kikwete akitaja kifungu chochote cha katiba ? Hatumii na wala hasomi katiba utakuwa unamuonea ukianza kuleta vifungu vya katiba hapa. Kumbuka hata watuhumiwa wa EPA aliwasamehe kinyume cha katiba, Rais wa Tanzania anamamlaka ya kusamehe wale waliokwisha hukumiwa na si watuhumiwa ndivyo katiba inavyosema.
Ni kweli mkuu jk sijawahi kumsikia akinukuu kipengele cha katiba , lakini jana alileta blah blah kwenye hii ishu kwa kisingizio cha katiba.
Kwa tafsiri ya haraka haraka mimi naona katiba imempa mamlaka ya kuunda hiyo tume.
 
Ni kweli mkuu jk sijawahi kumsikia akinukuu kipengele cha katiba , lakini jana alileta blah blah kwenye hii ishu kwa kisingizio cha katiba.
Kwa tafsiri ya haraka haraka mimi naona katiba imempa mamlaka ya kuunda hiyo tume.

Hakuruhusu maswali kulikuwa na wazee wakuda pale wangemuomba vifungu vya katiba ungeona prof kijasho kinamtiririka.
 
Hakuruhusu maswali kulikuwa na wazee wakuda pale wangemuomba vifungu vya katiba ungeona prof kijasho kinamtiririka.
Kwani wale wazee walifanya random selection au walikuwa wazee wao wa siku zote?
 
Mkwere alikuwa dhaifu mbona kwa mwenzie wanaomba kujiuzulu wenyewe?
 
Hivi huyu jaji alimfanyia nin rugemarila mpaka akampa 404m
 
Labda alimshauri kisheria jinsi kuchezesh ile drama....maana hata ilifika mahakama za London huko kama sikosei!! Maana Jaji amelamba nyingi zaidi ya Ngeleja.....aliekuwa Waziri
 
Back
Top Bottom