Hapa kuna wasiwasi na mahusiano haya

SupuyaPweza

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
914
471
Muda kiasi uliopita...
"JAJI wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aloyce Mujulizi, amejitoa kusikiliza kesi ya kupinga ubunge wa Arusha Mjini inayomkabili Mbunge wa jimbo hilo, Godbless Lema (CHADEMA), ambaye alidai hana imani naye.

Mujulizi alijitoa jana baada ya wakili wa Lema, Method Kimomogoro, kudai kuwa mteja wake hana imani na jaji huyo kwani CHADEMA kiliwahi kuituhumu Kampuni ya Uwakili ya IMMA, ambayo jaji huyo alikuwa mmoja wa wamiliki wake kuhusika na ufisadi uliotokea kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kupitia Benki Kuu (BoT).

Alisema kuwa endapo watashindwa kufanya hivyo ndani ya siku tano wachukue hatua za kikatiba za kuwasilisha rasmi maombi kwa rais ili aunde tume kuchunguza suala hilo ili ukweli uwekwe wazi, kwani kwa tuhuma zinazomkabili hastahili kushika nafasi ya ujaji".

Kampuni hii ndio aliyokuwa akifanya mazoezi ya kisheria bwa mdogo ridhiwani

"Before joining GRK Advocates as a partner Mr. Kikwete worked with IMMA Advocates holding different challenging positions from January 2005 to December 2010".

Lakini mmoja wa waliokuwa wamiliki wa kampuni hii ni mheshimiwa...

linazo taarifa kwamba kampuni ya mawakili ya IMMA Advocates and Co. ya Dar es Salaam ndiyo ilisadia usajili wa Deep Green Finance Ltd iliyochota Sh. 8 bilioni kutoka BoT. Hakuna maelezo yoyote yaliyowahi kutolewa kueleza kwa nini Deep Green Finance Limited ililipwa mabilioni hayo na BoT wakati wa uongozi wa gavana Daudi Billali ambaye Rais Jakaya Kikwete alifukuza kazi miezi miwili iliyopita. Mtoto wa rais, ambaye anafanya kazi katika kampuni iliyosaidia kusajili Deep Green Finance Ltd., ni Ridhwani Kikwete. Deep Green Finance Limited ilichota fedha hizo kati ya Septemba na Desemba 2005 wakati wa mchakato kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. IMMA inasimamia majina ya wamiliki wa kampuni hiyo ya mawakili ambao ni Protase Ishengoma, Lawrence Masha, Aloysius Mujulizi na Sadock Magai".

huyu mkulu amehusishwa na EPA, kachomoa... akahusishwa na Deep Green kachomoa... sasa katajwa mambo ya Tegeta Escrow.. yumo kwenye orodha ya mgao... swali je anasingiziwa?
 
Back
Top Bottom