Wacha uongo, wewe kila uongo unaolishwa unakuja kuutupia hapa, hata hutumii akili yako hata kiduchu basi, Mbona Ruhangisa hujamtaja, au na yeye si jaji? soma:
Azimio la Tano: Linasomeka; Bunge linaazimia kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aunde Tume ya Kijaji ya Uchunguzi kuchunguza utovu wa maadili dhidi ya Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Azimio hili nimelipokea, tumelijadili hata hivyo, itabidi tufuate utaratibu wa kikatiba na kisheria wa kushughulikia masuala ya namna hiyo. Inatakiwa suala kama hili lianzie kwenye Mhimili wa Mahakama yenyewe na siyo kwa Rais au Bunge. Tume ya Mahakama ndiyo yenye mamlaka ya kumtaka Rais aunde Tume ya Kijaji ya kumchukulia hatua Jaji yeyote pale inaporidhika kuwa amepoteza sifa za kuendelea kufanya kazi hiyo. Nashauri suala hili tumuachie Jaji Mkuu wa Tanzania alishughulikie atakavyoona inafaa.
Wala halishghulikii yeye kawawwachia wenyewe mahakama na kaelezea kawaida yake huwaje, majaji watatu, mmoja kutoka nje ya nchi na huyo wa nje ya nchi ndiye anakuwa kiongozi wa hao wengine.
Kikwete angeamuwa yeye si ndiyo ingekuwa mwao. Hapo haingilii Mhimili wa mahakama na mnakuja kudanganya eti "ndio anatakiwa kuwajibishwa na mamlaka yake".
Wacha = Acha
, Mbona = , mbona
? soma: = ? Soma: