binafsi huwa siamini dhana hii kwa mtu ambaye ni mzima na anautashi wake, ila tu hili linaweza kwa watoto ama wanafunzi.
mfano sio kwamba marafiki zangu wote nilionao wanatabia njema ila wapo ambao nawajua kabisa tabia zao ni mbaya na kuwa rafiki yao mimi natumika sana kuwarudisha kwenye mstari kila iitwapo leo.
mara nyingi sana ni vyema kumrekebisha mtu mwenye tabia mbaya kwa kuwa rafiki yake na kila siku akajifunza jambo toka kwako ama kwa kukusudia ama wakutokukusudia.
mf, ninaye wifi yangu ni MD sasa anapoishi kuna kijana mmoja mzazi wake alikuwa mkuu wa wilaya na sasa ni marhem huyu kijana kwa kukosa mtu wa kumwongoza amekuwa ni mlevi wa kupindukia hadi anajikojolea. sasa wifi yangu huyu kawa rafiki wa huyu kijana kiasi kwamba hata kwake anakuja wanaongea na wanatoka nae kwenda kunywa nia ya wifi ni kumbadilisha so anapokunywa nae yeye wifi anakunywa malta kijana anakunywa bia ila ana muhesabia zikifika 3 anamwambia haya sasa tuondoke uende nyumban ukalalale, kweli kijana kwa kuheshimu urafiki wake kwa wifi ananyanyuka na kurudi home kabla hajalewa. mumewe wifi imebidi amchukue huyu kijana awe anaenda nae kwenye kazi zake as a friend ili tu abadilike na kuacha pombe kabisa. kwangu mm niliwapongeza sana nikamwambia wifi yangu atakuwa na baraka sana manake anabadili wale ambao jamii inawadharau na kuwatenga.