Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
- Thread starter
- #181
rafiki ulikuwa wapi siku zote hizi ukatunyima mchango wako mzuri? asante sana kwa mchango.Rafiki definition ya "Tabia mbaya" ni pana mno na ina differ kati ya watu na watu. Kwa mfano kuna watu wengine watakwambia Mama XYZ ana tabia mbaya sana, "Yule mama anaweza kwenda Bar na wanawake wenzake na wakakaa na kunywa bia zao." Hapa tabia mbaya ya Mama XYZ ni kwenda bar bila kufuatana na mumewe. Wengine wanaweza kukwambia yule Mama ABC ana tabia mbaya sana, "Anapenda kuva nguo za kisichana wakati ameshakuwa mtu mzima. Lazima atakuwa mhuni yule" Hapa tabia mbaya ya Mama ABC ni kuvaa nguo fupi juu ya magoti, kaptula, vimini, skin tight etc. Kumbe hizo nguo anazovaa mumewe ndiyo anapenda avae hivyo kutokana na umbo la mkewe basi yeye haoni tatizo la mkewe kupendeza.
Mama mwingine katika jitihada za kuongeza kipato anaweza kabisa kuwa anajiuza kwa namna anayoijua yeye ambayo si ajabu watu wengi wamemshtukia. Sasa Mama kama huyu kuambatana naye katika macho ya jamii ni kujiharibia reputation. Inawezekana kabisa muhusika anafuatana na mama huyu hajui tabia yake ya kujiuza lakini machoni jamii wote wanaonekana lao moja na si ajabu mama huyu akijua tabia ya rafiki yake anaweza kabisa kumuepuka.
Watu wengine wana ile tabia ya "Don't care attitude" hata kama jamii iliyowazunguka inasema fulani ana tabia mbaya na yeye anazijua kabisa tabia za huyu rafiki yake kwamba ni mbaya ali mradi kuna mambo ambayo wanaelewana basi anatia pamba masikioni na kuendelea na urafiki wao bila kujali jamii inayowazunguka inasemaje kuhusu hao marafiki kuwa na "tabia mbaya"
Marafiki wengine wanaweza kabisa kuwashawishi marafiki zao waachane na hizo "tabia mbaya" zao bila masharti yoyote yale na huku urafiki ukiendelea bila dosari yoyote ile.
Hebu fafanua hizi "tabia mbaya" unazozizungumzia hapa ni zipi? Ukiziweka hata mbili tatu utasaidia sana katika mjadala huu.
Sayonara Rafiki.
kama ulivyosema tabia mbaya zinatofautiana, zipo nyingi na mtu mwingine anaweza kuona hii ni tabia mbaya na mwingine aone wala siyo. mimi nilikuwa naongelea yoyote ile, hata hizo ulizozisema. point yangu hapa ni kwa nini watu wakufikirie na wewe una/utaiga tabia ambayo huyo rafikiyo anayo kisa tu ni rafiki yako?