Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
- Thread starter
- #21
barikiwa sana HorsePower kwa mawazo mazuri.Labda kabla ya kuchangia tujiulize urafiki ni nini hasa? Na unajengwa na nini? Na kigezo cha kuwa na rafiki ni kipi? Na yapi yanawaunganisha ktk urafiki?
Nikianza na hili swali la mwisho, urafiki mara nyingi hujengwa kwa njia mbali mbali ikiwepo kuunganishwa na watu au ndugu au marafiki wengine, kukutana kazini au shuleni au vyuoni nk, kwenye shughuli za biashara, kwenye vyombo vya usafiri, kwenye maeneo ya starehe, nyumba za ibada nk.
Lakini mvuto wa urafiki huletwa na vitu fulani common kati ya mtu na huyo rafiki. Inaweza kuwa wote ni wapenzi wa kitu fulani, washabiki wa mpira, majirani manosaidiana nk nk. Ktk hali hiyo ya urafiki hujikuta wakitoka pamoja, kuenjoy pamoja, kutembeleana, kuongelea mambo fulani yenye mtazamo unaofanana nk
Hali hii hulazimisha jamii kuona kuwa marafiki wanatabia zinazofanana, Na hata kama ikitokea kuwa wanatabia ambazo hazifanani, basi kuna uwezekano mkubwa wa mmoja wapo kuiga tabia za mwenzake pasipo yeye kujijua na kujikuta wakidumisha urafiki wao. Ni vigumu ingawa inawezekana sana kuwa na urafiki na mtu ambaye mmepishana sana kitabia au interest. Ktk hali hii pia ni wachache sana wenye uwezo wa kuwa ndani ya urafiki lakini wakaweza kudumisha imani, tamaduni na taratibu zake za kawaida za maisha bila kuwa influenced na tabia za marafiki wengine kwenye kundi lao na ndiyo maana kuna usemi wa ndege wenye rangi moja huruka pamoja!!!
Lakini hata hivyo naunga mkono hoja yako kwamba si vyema sana kuhukumu tabia ya mtu kwa sababu ya urafiki wake na mtu mwingine au kukatazwa kuwa rafiki na mtu kwa sababu za tabia za huyo kama kweli wewe ni mtu mzima na unajua nini unachofanya. Tahadhari ni kuwa mob psychology ni kitu hatari na hutokea pasipo kujua, so ni muhimu kuwa makini sana kwenye mahusiano haya.
Nashukuru sana
hapo kwenye RED ndo hasa kwenye kiini cha hii mada...
Kwa nini watu wengi wanafikiri kama mna tabia zisizofanana na hasa kama mmoja wenu ana tabia ambayo haipendezi machoni kwa watu basi na mwingine ataiga hiyo? kwa nini wasiangalie the other way around?
Last edited by a moderator: