Mjinga hujisifu ana mbio katikati ya viwete

Mjinga hujisifu ana mbio katikati ya viwete

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
466
Reaction score
1,209
Katika jamii yetu kuna tabia ya watu kujiona wakubwa kwa sababu wanashinda wale walio dhaifu kuliko wao.

Msemo huu unatukumbusha kuwa ushindi wenye maana hupatikana unaposhindana na watu wenye uwezo sawa na wako, siyo unapomponda mtu aliyeshindwa tayari.

Katika maisha ya kila siku tunaona hili kwenye siasa, biashara, michezo na hata mitandaoni.

Tatizo ni kwamba ushindi wa namna hii haudumu , Siku mshindani hodari anapoingia uwanjani ukweli unaibuka.

Jamii inapoendelea, inahitaji watu wanaojipima kwa viwango vya juu na wanaojaribu kushindana na bora zaid siyo wale wanaotafuta njia rahisi za kujitukuza.

Leo tunapojenga taifa, tunahitaji viongozi, vijana na wataalamu wanaotafuta changamoto kubwa. Ni rahisi kujisifu miongoni mwa dhaifu, lakini ni vigumu kujenga jina kati ya wababe.

Ushindi wa kweli ni ule unaokufanya uboreshe jamii nzima siyo ule unaokufurahisha wewe peke yako.

#Mwanasayansi Kalivubha
#Malenga wa Kiha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom