Waberoya, nakuomba tuwe wakweli kwenye nafsi zetu, tuache ushabiki wa kisiasa, hivi kati ya wanasiasa walioko CCM na wale wa Chadema, nani wako kimaslahi zaidi?. Just be genuine.
Kuna watu wamejiunga CCM na wako CCM sio kwa sababu wanaipenda CCM bali kwa sababu ya opportunities zilizoko CCM. Kuna wana CCM safi ambao wanajua CCM inanuka rushwa na imehodhiwa na wenye pesa, wanaendelea kubaki CCM kwa sababu hawana guts za kukubali kufa njaa. Mimi binafsi sina chama wala sijajipanga kujiunga na chama chochote, nikiamua kuingia siasa ili kupata ulaji, nitajiunga na CCM na kujikomba komba kwa kwenda mbele mpaka niukwae ulaji, siamini kuwa CCM ina uchungu na umasikini wa Tanzania na inatawala kwa malengo ya kuuondoa umasikini huu, CCM inatawala kwa mazoea.
Nikija kwenye Chadema, hivi kuna mwanasiasa anayejiunga Chadema ili kupata ulaji?. Chadema kitakapo pata fursa ya kushika dola (nothing is impossible under the sun), ndipo wanachama wachumia tumbo watakapo kivamia, na wale CCM opportunities ewakishajua there are opportunities no more nao watakihama.
Dhana ya utopia sipingani nayo, ndio maana Mwalimu alisisitiza 'Ujamaa ni Imani', ila utopia huu wa imani kisiasa ni utopia mzuri zaidi, kwani hata usipofanikiwa bado imani itakufariji kuwa the right time is not yet, but one day yes!. Utopia mbaya zaidi ni ule wa kupreech "maisha bora kwa kila Mtanzania", but not practice what you preach!.
Ila pia nakubaliana na wewe, kuwa wako wanasiasa ambao wanataka kuwa kote kote, kupigania maslahi ya taifa na pia, kuchumia tumbo.
Mkuu wanasiasa sio watu wa kuwaamini kivile....
Leo wanaweza wakaonekana wapiganaji wazuri kwa sababu hajawapata nafasi ya kufanye yale madudu yanayofanywa na wenzao. mpaka sasa upiganaji wa chadema uko kwenye maneno, sera nzuri na wishful thinking at least we can have a hope kwa sababu ya wanachokisema lakini si kwa sababu ndivyo walivyo!
Sita, mwakyembe, kilango et al nao wanaweza wakawa anaonekana kuwa ni wapiganaji wazuri ,laini ukija kwenye logic za ethics hawafai kuwamo ndani ya ccm, lakini ukweli katika maisha yao wanafanya yaleyale wanaoyafanya wenzao
ushaihidi upo, Kibaki aliyeaminiwa na wakenya kumuondoa moi, ndiye aliyekuja kusababisha vita mud mfupi tu.....yuleyule ambye alionekana mkombozi leo hii kaonekana alivyo
Hivi CCM wasingemuangusha Slaa kwenye kura za maoni si Slaa angekuwa CCM, au kwake yy muonekano wa CCM miaka hiyo ulikuwa positive na ghafla imegeuka. au unataka kusema nini akina marando walifahamu lini chadema na wamejiunga lini na kwa nini? akina mpendazoe wametokea wapi? we have very very reason to believe that we have people whose their behaviours are so dynamic and unpredictable..
The only way to overcome this is to establish robust system,systems that they will accomodate any character and punish it accordingly. Ukiwa na system nzuri akina mr.Clean kama akina Mkapa ambao wanatoka wachafu wanashughulikiwa vilivyo na sio kuanza kutumia akili zetu na kujudge eti amefanya mazuri hivyo mwache aende.
I am still believing kuwa viongozi wengi CCM ni wezi na wanaweza ghafla wakawa malaika na wazuri kama system ya kuwafanya hivyo ipo..yaani kuwa accountable kwa matendo yao.
However to touch that achievement we need fight and changes....ambazo kwa uelewa wangu wa siasa za kushiriki na kusikia hatuna vyama vya style ya akina Odinga,Sata na akina morgan Tsvangirai!!!! chadema lacks clear startegy kuichukua nchi na wakitaka uwezo huo wanao, ila sijaona wakifanya hivyo. sijaona wakija na utatuzi mbadala kwa kila tatizo linaloikumba nchi hii. Nimeona nguvu nyingi ikitumika unnecessary na ukija nyuma ya pazia....tetesi au ukweli wowote wa kuihusisha chadema na akina Lowassa NA YA kuwa mwaka 2005 akina JK na Lowasa wangeamia CDM (confirmed) kama wasingepitishwa na kk ya ccm ni skendo nyingine ambayo inakiweka CHADEMA KUWA ANOTHER MISSION TOWN party!
hatuna vyama vya upinzani, chadema ni kivuli cha chama kizuri cha upinzani ambacho kingekuwepo CCM wasingetamba hivi.
Tunataka maandamano ya kudai katiba, tume huru ya uchaguzi, kushiriki uchaguzi ambao unajua mwisho wa siku uamuzi wa nani awe mshindi uko mikononi mwa tume ambayo ya CCM still vyama hivi vinapokea ruzuku kwa ajili ya uchaguzi while we are crying poverty every corner BADO kuna maswali mengi sana.