director1, usitake kumdanya mwenzio aachie ulaji hapo CUF!, mwenzako hapo ni naibu katibu mkuu ambayo ni very senior position. Juzi wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga, Mtatiro aliidhinisha malipo ya milioni 50 kulipia ile helcopter bila kushauriana na yoyote hapo CUF, hii ikiwa ni ushahidi kuwa pia anayo purchasing power kubwa, unataka aende chadema akafe njaa?!.
Kwa Tanzania tuna wanasiasa wa aina mbili, aina ya kwanza ni wanasiasa ambao siasa kwao ndio professional na ajira zao za kudumu kuendeshea maisha yao. Hawa wanaingia siasa ili waweze kuishi ndio maana Lipumba ndiye mgombea wa kudumu wa urais wa muungano kwa tiketi ya CUF.Wengi wa wanasiasa walioko CCM na CUF ndio wa kundi la kwanza. Kundi la pili la wanasiasa wa bongo, ni wale wanaoingia siasa kwa kutaka kuwatumikia wananchi, hawa wanauchungu na umasikini wa Tanzania hivyo wanaingia siasa ili kuleta mabadiliko, wengi wa walioko Chadema ndio kundi hili la pili.
CUF ni chama cha siasa cha wachumia tumbo, kinagombea uongozi ili kupata ulaji, baada ya kufunga ndoa na CCM, wanagawana ulaji, hapo sasa hakuna kingine wanachotaka ni kugawana tuu keki ya taifa na kula kwa ulaini, hivyo Mtatiro hapo alipo ni pazuri sana kwa ulaji, msimdanganye ahame aachane na ulaji aje Chadema kwenye struggle ambapo kwa sasa anakula kwa kuypewa, akienda Chadema, itambidi ale kwa jasho lake!.
Mtatiro usidanganyike, jitulize tuu hapo hapo ulipo, endelea kujilia kwa ulaini, 2015 kombea tena ubungo uendelee kusindikiza huku ukijilia kwa ulani. Kama unaweza kujipatia ulaji kwa ulaini na mteremko kama huo ulionao hapo CUF, kwanini ukapande milima na mabonde kama Chadema?.
Tena kutokana na jina la Julius, wewe ni mtaji muhimu sana CUF, naomba usifikirie kabisa kuhama, chama kitakufanya mgombea wa kudumu wa jimbo la Ubungo kama alivyo Prof. Lipumba ni mgombea wa kudumu wa urais wa muungano.