Complications of blended families

Complications of blended families

na sheria zetu pia,mfano sheria za kiislam hazimtambui kabisa mtoto wa nje, sasa kama utambuliki utashirikije shuguli za kijamii?

Hii nayo kali manake sasa wanaassume ni wanyama ama ni watu??
Hii ni mbaya zaid
 
Hivi hayo malezi unataka mtu anaye blend in aleleweje?
Imagine mtt haombi achague aina ya familia kuchaguliwa mbaya zaid unajikuta tayari ushazaliwa unataka kufanyeje?
Ama je huyu mtoto alipozaliwa kosa ni la nani
Kikubwa kinachangia na malezi ambayo mtu analelewa kabla ya kublend in.
 
Duh shida juu ya shida Mwanaume kuoa mwanamke mwenye mtoto utadhani vigoli vimeisha mwisho wa siku mwenye mtoto akianza mawasiliano na Mama (mzazi mwezake) tafrani haziishi.
mwanamke naye akiolewa na mwanume mwenye mtoto, lazima watawasiliana na mama wa mtoto mwisho wa siku ni tafrani tu.
Mbaya zaidi kuna hali ya kutengwa kwenye hizi familia
 
Hivi kwani tatizo la kutokuwa na amani kwenye hizi familia huanzia wapi?
Kwani akina baba je hawawez kukumbatia watoto wao na kuwaacha wale waliozaliwa na mama?
tatizo lililopo ni la kimfumo na mara nyingi husababishwa na mwanamke (huyo mama aliyeolewa) kwanza hupenda kila alichonacho mme wake kiwe ni kwa ajili ya watoto aliozaa na mumewe au wa kwake aliozaa kabla sio wa mwanaume aliozaa kabla au nje.

Kutokana na hilo hujengwa mazingira magumu ya hao watoto kutokuwa na chao kwenye familia hiyo ndio hapo matatizo huanzia,maana na hao watoto wanapokuwa wakubwa hushindwa kufanya jambo la maana kwao kwa vile mama muhusika hawahitaji au watoto wa mama huyo watakuwa wamedokezwa hivyo kuwa wao ndio wastahili.
 
af unakuta tayari umeshakuwa mtu mzima.
Kila ukikaa huoni mtu wa kushea nae jambo lake kisa tu wenzio wana bond wewe uko kaa kitoto cha kunguru.
very touching
I real feel you ...saaana ila usijiskie hivyo teeena..yuko rafiki zaidi ya ndugu naye yuko karibu zaidi ya vazi lako..daah tangu niifahamu siri hii upweke ulikwisha natamani uijue
 
Hivi kwani tatizo la kutokuwa na amani kwenye hizi familia huanzia wapi?
Kwani akina baba je hawawez kukumbatia watoto wao na kuwaacha wale waliozaliwa na mama?
Kwa uzoefu wangu wababa wengi si watu wa kukaa nyumbani muda mrefu mama anaweza na hasa ndiye chanzo cha chokochoko nyingi maana yeye kama hajakuzaa hawezi kuwa na uchungu na wewe (wengi wao)na atafanya kila namna kuhakikisha baba yako anakuchukia ili asikuhudumie....kwa hili huwezi kumuelewa baba ako hasa kama ulikua unampenda na kumuamini kuwa ndio mtetezi wako..usimchukie wengi ni wadhaifu kwa wake zao ..usiwafikirie wala usijiulize kwanini..wasamehe ili uweze kusonga mbele na maisha yako pia ili wasikuzuilie baraka zao.
 
Hii nayo kali manake sasa wanaassume ni wanyama ama ni watu??
Hii ni mbaya zaid

ndio hivyo katika uislam mtoto wa nje ambaye sio wa wanandoa hatambuliki kabisa.sasa katika mazingira haya unakuta anateswa mtoto ambaye hana makosa maana yeye hakuomba kuzaliwa nje,badala ya kuadhibiwa wazazi anazibiwa mpaka na mtoto.ni mbaya sana
 
Unakuta mtoto kwa baba wako sita kwa mama wapo wanne...lakini yeye yupo alone...very lonely for some...
Hapo bado yule ambaye mama kaja naye yaani kazaliwa na baba mwingine ..wewe wa baba ambapo naye alikuzaa ujanani huyo huna undugu naye hata punje ila sasa sababu ya mamaake pale ndio anapafanya kwao..anakua mtu mzima keshaolewa ila akikosa hg anakimbilia pale wakati wewe mwenye baba huwezi kumpeleka mtoto wako pale...jamani ambao hamjaoa/hamjaolewa jifunzieni hapa...hiii inaumiza mnoooooooooo zaidi ya unavyoweza kuitamka usipoweza kupotezea unaweza kumchukia kila mtu
 
Hivi kwani tatizo la kutokuwa na amani kwenye hizi familia huanzia wapi?
Kwani akina baba je hawawez kukumbatia watoto wao na kuwaacha wale waliozaliwa na mama?

ni ngumu sana kwa mwanaume kufanya hivyo, hasa ukiangalia kuwa anayekaa na watoto muda mwingi na anayewajua zaidi ni mwanamke,maana mwana mateso ya hao watoto kwa malezi huwa kwenye chakula,mavazi .ndio maana nyingi tunasema wanamke ndio wanaoharibu zaidi.
 
vipi kuhusu mwanaume kuwa na mtoto na kuoa mwanamke asiye na mtoto..unalizungumziaje hili?
Duh shida juu ya shida Mwanaume kuoa mwanamke mwenye mtoto utadhani vigoli vimeisha mwisho wa siku mwenye mtoto akianza mawasiliano na Mama (mzazi mwezake) tafrani haziishi.
 
Nianze kwa kukiri kwamba sina nia ya kuhukumu manake hakuna msafi kati yetu. Lakini pia napenda tu niseme hili ili kama kuna aliyekusudiwa kupona basi apone.

Kuna hizi famila ambazo siku hizi wanaziita blended family maana yake familia iliyochanganywa. Imechanganywa watoto hasa hasa. Unakuta baba kabla ya kuoa alisha wahi kuwa na mtoto/watoto ama mama kabla ya kuolewa alisha wah kuwa na mtoto/watoto. Halafu kwa makubaliano yao (wazazi) wkaamua kuunda familia moja yenye watoto mchanganyiko wa upande tunashea baba upande tunashea mama.

Kwa experience yangu hizi familia ni matatizo sana hasa watoto wanapokuwa wakubwa. Achilia mbali wakiwa wadogo wapo watakao lalamika kuteswa na mzazi asokuwa wake lakini ukubwani hali huwa mbaya zaidi. Nimeangalia familia nyingi ambazo nazifahamu hili limekuwa ni tatizo na cha ajabu zaid ni tatizo kwenye umri wa utu uzima. Maugomvi ya kila siku, kesi kila iitwapo leo, wakikutana utafikiri wamekutana kwa amani lkin baada ya muda kidogo ni vita yaani familia inageuka Gaza. Alafu sababu zenyewe za ugomvi nyingine unazikuta ni za kitoto kama sio za kijinga.

Wenzangu nyie mmewah kuona familia za aina hii?
Kama ni familia yako wewe huwa unafanyaje?
Binafsi mie nimechoka.
rainyforest mimi nadhani kunajambo la muhimu amabalo ulitaka kuliweka hapa lakini ukaamua kuja juu juu, kama ulivyo sema kwa experience yako. mimi nadhani sio familia zote za aina hiyo zina shida kwa maana pia zipo familia zisizo blended lakini zina matatizo lukuki. matatizo katika familia yanatokana na malezi mama aliyokulia na baba alio kulia. usitegemee from the worst to get the best
 
Ni kweli hata kwa upande wa mwanaume kuna shida laikini si kama kwa mwanamke.Unajua Baba ni kichwa cha familia akiwa na ubongo mzuri anaweza kuhandle hiyo issue vyema lakini kwa upande wa Mama hasa tukizingatia mila na desturi zetu unakuta Baba ndiye kila kitu na ukija hata kwenye masuala ya urithi mara nyingi Baba ndiye mgawaji sasa fikiria umekuja na mtoto wako unafikiri ataambulia kitu tukianza na mapenzi ya mzazi,Elimu,Afya...... na hata familia ya Baba yaani ukoo wake hawatakubali mtoto asiye na damu yao.

vipi kuhusu mwanaume kuwa na mtoto na kuoa mwanamke asiye na mtoto..unalizungumziaje hili?
 
Hapo bado yule ambaye mama kaja naye yaani kazaliwa na baba mwingine ..wewe wa baba ambapo naye alikuzaa ujanani huyo huna undugu naye hata punje ila sasa sababu ya mamaake pale ndio anapafanya kwao..anakua mtu mzima keshaolewa ila akikosa hg anakimbilia pale wakati wewe mwenye baba huwezi kumpeleka mtoto wako pale...jamani ambao hamjaoa/hamjaolewa jifunzieni hapa...hiii inaumiza mnoooooooooo zaidi ya unavyoweza kuitamka usipoweza kupotezea unaweza kumchukia kila mtu
Unajua kuna maswala ya mabinti kuwaza kwamba nikizaa nitaweza kupata mume na akanikubali mimi na watoto wangu, well sikatai utapata, lakin asikwambie mtu hili ni jambo gumu sana kuliishi. linaumiza sana na linaleta hata chuki miongoni mwa watoto.

Af kuna mabinti wengine wanaona ni rahisi kuishi na mtoto wa mume ndio ni rahisi sana kuish na mtu yeyote ndani ya familia yako lakin inapokuja kwamba ni swala la mtoto wa kambo jamani lataka moyo wa ziada sana. Labda uwe ni mama uliyetulia katika maombi na uwe na moyo usiochunguza makosa ya wengine.

Kimsingi vijana wanatakiwa wajuae kwamba kuzaa tu bila kuwa na ufumbuzi wa kina juu ya hatima ya mtoto anaye mzaa ni jambo baya sana. Utaona wakina dada wanadai mie sijui nitazaa tu mtoto na kumlea mwenyewe afu siku ya mwisho unashangaa anataka kuolewa sasa hivi kweli hawi selfish kwa mtoto wake mwenyewe?

Sisemi kuwasema watu ila nimejionea mwenyewe blended family ni matatizo sana na ukweli ni bora kwangu nikafia kwenye ndoa yenye mateso kuliko kutoka kuanza kuchanganya watoto.
 
rainyforest mimi nadhani kunajambo la muhimu amabalo ulitaka kuliweka hapa lakini ukaamua kuja juu juu, kama ulivyo sema kwa experience yako. mimi nadhani sio familia zote za aina hiyo zina shida kwa maana pia zipo familia zisizo blended lakini zina matatizo lukuki. matatizo katika familia yanatokana na malezi mama aliyokulia na baba alio kulia. usitegemee from the worst to get the best
Sikiliza mkuu mie nia yangu ni kusema hivii mara nyingi sana blended families ni ngumu sana kuziishi. Na hizi matatizo huanzia watoto wakisha kuwa wakubwa. Wakiwa wadogo wataishi vizuri tu ila sasa wakisha kuwa wakubwa, utajuta kuwa nao. Amani nyumban hutoweka visasi na maugomvi hayakomi, kila mtu ni mbabe ndani ya nyumba alafu unakuta yule ambaye ndo hana ndugu ndo mkorofi kila sasa anaona yeye ndo anaonewa.
 
Nianze kwa kukiri kwamba sina nia ya kuhukumu manake hakuna msafi kati yetu. Lakini pia napenda tu niseme hili ili kama kuna aliyekusudiwa kupona basi apone.

Kuna hizi famila ambazo siku hizi wanaziita blended family maana yake familia iliyochanganywa. Imechanganywa watoto hasa hasa. Unakuta baba kabla ya kuoa alisha wahi kuwa na mtoto/watoto ama mama kabla ya kuolewa alisha wah kuwa na mtoto/watoto. Halafu kwa makubaliano yao (wazazi) wkaamua kuunda familia moja yenye watoto mchanganyiko wa upande tunashea baba upande tunashea mama.

Kwa experience yangu hizi familia ni matatizo sana hasa watoto wanapokuwa wakubwa. Achilia mbali wakiwa wadogo wapo watakao lalamika kuteswa na mzazi asokuwa wake lakini ukubwani hali huwa mbaya zaidi. Nimeangalia familia nyingi ambazo nazifahamu hili limekuwa ni tatizo na cha ajabu zaid ni tatizo kwenye umri wa utu uzima. Maugomvi ya kila siku, kesi kila iitwapo leo, wakikutana utafikiri wamekutana kwa amani lkin baada ya muda kidogo ni vita yaani familia inageuka Gaza. Alafu sababu zenyewe za ugomvi nyingine unazikuta ni za kitoto kama sio za kijinga.

Wenzangu nyie mmewah kuona familia za aina hii?
Kama ni familia yako wewe huwa unafanyaje?
Binafsi mie nimechoka.
Kukwepa jambo hili ni ngumu sana.Tatizo linakuja pale mnapotolea macho urithi kutoka kwa wazazi.Ila kila mti akijitahidi akawa njema kimaisha matatizo huwa yanapungua.
Kwa siku hizi utakuta hata watoto wa baba mmoja mama mmoja nao hawapatani.
 
ZD hapa mali zio tatizo manake kuna familia nyingine watoto wako na hali nzuri zaid kuliko wazazi na hakuna anyetolea macho mali za wazazi. Yaani hapa unakuta kuna ugomvi kila mtu ni mbabe anataka aonekane na kauli yake isikilizwwe zaid kuliko wengine, Hakuna kuvumiliana kabisa.

Nilifikiri labda ni swala la ibada lakin sio kweli manake kwenye swala hili hadi watu wanashindania miungun kwamba Mungu wa nani ndiye mkuu zaid anayejua kujibu maombi nk. Mie kwa ninachokiona hizi familia ni shida sanaa.
 
rainyforest mimi nadhani kunajambo la muhimu amabalo ulitaka kuliweka hapa lakini ukaamua kuja juu juu, kama ulivyo sema kwa experience yako. mimi nadhani sio familia zote za aina hiyo zina shida kwa maana pia zipo familia zisizo blended lakini zina matatizo lukuki. matatizo katika familia yanatokana na malezi mama aliyokulia na baba alio kulia. usitegemee from the worst to get the best

Kweli kabisa mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom