Comment on this Photo Pse!!

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,460
kulogwa.jpg
 
Hivi si vile vijumba vya shamba vya msimu, vinatumika wakati wakulima kupalilia na kuvuna viaachwa hadi msimu mwingine
 
Aisee nafikiri wewe unaishi masaki ndo maana huelewi mambo haya kwamba hiyo inaweza kuwa nzuri zaidi kuliko nyingine. tembeleaa vijijini hasa dodoma na singida utarudi hapa na kutua comment tofauti
 
Huu ni umasikini na ujinga uliyokisili!hapa umbadili mtu hata kwa bakora!
 
Hata kama anaishi kwenye tembe,,,, lakini ana MAPENZI
mwacheni msimbughudhi
 
Angalie picha kwa makini zaidi ya dk 5, Tanguliza mbele uzalendo/ Utaifa kwamba sisi wote ni wamoja na Tanzania ni yetu sote - Then imba wimbo wa "Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote ki moyo moyo" then pima tena kizazi cha huyu jamaa anayeishi kwenye kibanda hiki? Fikiri tena then give me more comments plse!!

Gusia Elimu na Afya kwa kizazi cha huyu jamaa anayeishi hapa - then toa mapendekezo yako kwa ufupi
 
Hivi si vile vijumba vya shamba vya msimu, vinatumika wakati wakulima kupalilia na kuvuna viaachwa hadi msimu mwingine

Hapana, hii ni nyumba ya mwenyekiti wa kijiji, ndiye mwenye hali bora zaidi hapo kijijini
 
Hiyo ni nyumba au KIBUBUNSWA????

Kibanda poa sana hasa kwa vijijini maana kimekaa mbali na nyumba za Wazazi wa mabinti.

Na hivi imebandikwa sura ya Handsome Man, totoz hapo zinakuja kama Nzi kwenye Kibuyu cha Maziwa cha Mtusi.
 
Jamaa amejenga kwenye hifadhi ya Barabara sasa ili asibomolewe ametundika picha ya Handsome Boy... Jeikei...
 
Inasikitisha kuona bado watanzania tunaishi katika hali duni kama hii,hivi ni umaskini tusioujua au kuna jambo jingine?
Au tuna laana ya mwenyezi Mungu?
Hivi wanaoishi humu wajukuu zao watakuwaje?
Ndugu za hawa watu ni siafu,mijusi,nyoka,hawana choo na humaliza haja zao porini kama wanyama,hospitali zao ni majani ya mitishamba na hawaijui kesho itakuwaje.
Wamlaumu nani?
 
Safi majibu mazuri, Swali je huyu mtu anaelewa chochote kuhusu uongozi wa taifa? ana elimu ya uraia? Namuunga mkono Ndugu yangu sikonge kwamba kabandika pale ile picha kama pambo tu ili na yeye aonekane anaenda na wakati. sasa kumbukeni 80% ya watanzania bara ndiyo wanaishi maisha yanayofanana na haya.

Bila ukombozi wa kweli tutaishia kusindikiza kikundi kidogo cha watu wanaojifanya ndiyo wanaweza kuongoza nchi hii. Bila kumshirikisha mtu huyu kiuchumi atajikwamuaje? tumwanche azame na kizazi chake? hamuoni kufanya hivyo si haki? kwani mali asili za taifa hili zinamhusu pia anatakiwa apate percentage yake.

Uzuri hajui haki zake kama mtanzania, anafurahia maisha yake na picha ya mgombea akiiangalia ni kama kafika beach hotel vile. Sasa kiongozi bora ni yule atakayeshirikisha watu wate kwenye nguvu za kiuchumi wa taifa letu. Mtu huyu na kizazi chake bila kumshika mkono nduguzangu kaishia huko huko porini kuishi kama mnyama.

Hana elimu, Hana afya, ni mgonjwa hana matumaini - Tunahitaji mabadiliko, tunajitahi kutoa matumaini mapya kwa watu wa namna hii waliokata tamaa kama huyu bwana tena kwenye nchi yake akijisifu kwamba nchi yake ni huru miaka 46 iliyopita.

Nawaombeni watanzania wenzangu hii nchi ni yetu sote, tugawane kidogo tunachopata kwa pamoja, walio juu washikeni mkono wenzenu walio chini tuvuke pamoja hapa hapa duniani tunapita tu hakuna atakayeishi milele sasa kwa nini umnyime haki mwenzako? tena haki za msingi? (elimu, afya na makazi) wakati wewe (serikali) ndiyo umepewa mamlaka ya vitu vyote vilivyomo ndani ya nchi hii uviangalie?

Tafakari ndugu Mtanzania mwenzangu - Utaifa mbele. Narudia Mabadiliko ni lazima.
 
Hali hii ndio ninayoizunguzia kila siku,watu wengi huko vijijini hawaelewi hata faida au hasara ya kuwa na viongozi ,wao wanachojua ni jembe begani msimu ukifika,na ngoma kwa kwenda mbele wakati wa mavuno na huwaambii kitu kuhusu CCM,hata ikimsimamisha mwehu kwenye uchaguzi lazima atashinda tu,na ndio sababu CCM inahakikisha kuwa watu hawa hawaelimiki kwa gharama yoyote ile ili kulinda mtaji wao wa kura,Ni vyema basi vyama vya upinzani viwafikie watu hawa kwa nguvu zote kuanzia ngazi ya mtaa ili kuwaelimisha umuhimu na thamani ya kura zao katika maisha yao vinginevyo hali itakuwa ni ileile miaka nenda miaka rudi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom