Ngida1
JF-Expert Member
- Aug 25, 2009
- 586
- 206
ngida eti kweli katika hili pilikapilika la kuoa kinguvu,Thabit kombo alioa mdosi kwa nguvu.waziri mkuu wa india akamuomba nyerere aingilie ili swala la watu kuozeshwa kinguvu-to the dismay of the world nyerere was powerless kumwambia strongman karume anything
Dear Son of Alaska,
Wewe ndugu yangu usinitafutie matatizo zaidi hapa ukumbini. Nishaitwa mbuzi sasa tena wewe unataka niitwe nini zaidi ya mbuzi? Au unataka niitwe Jack Ass?
Ninachojua mimi ni kuwa serikali ya Shah iliwahi kuleta maneno maneno kwa Nyerere. Lakini kuhusu Thabit Kombo na kinati chake sikuwahi kusikia kitu, kwani japokuwa alimuoa siku hizo hizo, lakini mama alikuwa ka-fall sana kwa Thabit na walikuwa siku zote wakionekana Forodhani wanakula ice-cream na mbatata za urojo kwa Adnan. Hii inaashiria kuwa ndoa yao ilikuwa ya mapenzi.
Saidi Washoto yeye yule mwarabu pia hakumuoa kwa nguvu kama inavyosemekana. Mume na mke walikuenda kwa Saidi Washoto pale Mnazi Mmoja wakati alikuwa RC wa Mjini ili wapatanishwe na Washoto. Katika mazungumzo Washoto akaona kuwa wale hawapendani tena na ndipo alipomueleza mume bora amuache mke. Siku ya pili Saidi Washoto akamuoa yule binti na akapata watoto nae. Sidhanii hapo kama Washoto alikosea, kwani jamaa alimuacha mwenyewe toto jeupe la kiarabu!