COL.MAHFUDHI: Zanzibari and Tanzanian internationalist | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

COL.MAHFUDHI: Zanzibari and Tanzanian internationalist

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JokaKuu, Sep 12, 2009.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Sep 12, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,802
  Likes Received: 5,094
  Trophy Points: 280
  ..jamani huyu askari wetu naambiwa alifariki na kuzikwa Msumbiji.

  ..mchango wake ktk vita vya ukombozi Msumbiji ni vizuri ukawekwa wazi.

  ..naambiwa marehemu Field Marshal Samora Machel, Raisi wa kwanza wa Msumbiji, alimpenda sana Col.Mahfudhi.

  ..Mahfudhi alikuwa kati ya makamanda wa JWTZ waliobaki Msumbiji baada ya nchi hiyo kupata uhuru. mwingine ni marehemu Brig.Gen.Makaranga.

  ..
   
 2. K

  Kudi Shauri Senior Member

  #2
  Sep 12, 2009
  Joined: Nov 1, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Col. Ali Mahfudh was one of the early commanders of TPDF from Zanzibar. Nafikiri alikuwa Chief of Operations and Training in the late 1960s and in 1972 he was somehow allegedly implicated in the Karume assasination. He was detained together with Abdurahaman Babu on the mainland and Mwalimu refused to send them to Zanzibar for trial as demanded by the Zanzibar government. They were released in the late 1970s.

  Mahfudh had played a leading role in the initiation of the FRELIMO's guerilla campaign in 1965/69 and he was very much liked by the FRELIMO leadership. On his release from detention he was invited by Samora to Mozambique as his defence adviser and remained there until the late 1990s when he died was buried as a hero of Mozambique at the Heroes Cemetery in Maputo.

  In Zanzibar politics he was associated with the radical UMMA Party which merged with ASP before the 1964 revolution. It is claimed he was one of key fighters during the Zanzibar revolution.
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Sep 12, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,802
  Likes Received: 5,094
  Trophy Points: 280
  kudi shauri,

  ..asante sana kwa maelezo yako.

  ..mimi nadhani mchango wa Col.Mahfudhi na wengine uwekwe wazi. kama alihusika na masuala ya Karume basi that will be an "astreks" in his contribution to our country.

  ..sasa kama imefikia mpaka Col.Mahfudhi kuzikwa kwenye heroes cemetary za Mozambique halafu huku Tanzania hakuna anayejua habari zake nadhani siyo kitu kizuri hata kidogo.
   
 4. m

  mzanganyika JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 257
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Alichofanya Col. Mahfudh ni kuwazunguka Hizbu na yeye pia akazungukwa mbele ya safari yake ya kisiasa.


  Katika siasa, mtu anayesaliti wenzake hawezi kuaminiwa na wale walionufaika na usaliti wake hata akifanya nini. Watabaki kutumiana tu kwa muda.
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hata hivyo bado Col. Mahfoudh atabaki jina kubwa katia mapambano ya ukombozi zidi ya mabeberu wakoloni, aliamua kubaki Msumbiji baada ya SMZ kuisaka kwa udi na uvumba roho yake na Mungu tu ndo alikua mlinzi wake, aliyekuwa mkewe mama Naila M.Jidawi anahuisha harakati za siasa za iliyokuwa familia ya kimageuzi na mchango wake kwa maendeleo ya jamii ya watu wa kawaida wa zanzibar ni mkubwa bila ya kujali tafauti za kisiasa,kidini wala kikabila, cha kushangza bado kuna wanachama na viongozi wajinga wa CCM kule kusini Unguja wakimpiga vita huyu mama kwa chuki za kisiasa tu, ana waliwahi kuongoza harakati za kuhujumu vitega uchumi vyake, mama Naila kusimama kwake kaitka haki amefanikiwa kijasiri kulinda haki zake za wananchi wanyonge wanaotiwa umasikini na SMZ na CCM kule visiwani.
   
 6. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  <mtu anayesaliti wenzake hawezi kuaminiwa>

  Mzanganyika unaandika nini jamani? Col Mahfudhi kawasaliti wenzake kwa kujiunga na Umma Party na baadae kushirikiana na ASP kumpindua Sultani? Huku ni kusaliti?
  Ulikuwa unataka abakie Hizbu akiulinda utawala wa Sultan na hapo ndio ungelimuona hajasaliti? Ninahakika huijui Zanzibar kabla ya Mapinduzi, else usingeliandika maneno kama hayo. Sio peke yako, wengi hapa JF hawaijui Zanzibar na huwa wanaropokwa ovyo tu!
  Ungelikuwa unarejea shule na huku umechoka na unaambiwa na baba yako ukafukuze ng'ombe waliokatwa kamba kwasababu wamekula majani ya kwenye shamba la Sultani, basi hapo ungelijua nini kusaliti na nini kuwatakia kheri waliyowengi!!!
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,583
  Trophy Points: 280
  Asante kukumbushia Col. Mahafudh. Huyu ni miongoni mwa ma strategists wa Zanzibar Revolution, yeye, akina Abrahaman Mohamed Babu.Feild Marshal John Okello, Abdalah Said Natepe na wengine. Siku ya mapinduzi yenyewe, January 12, Karume aliikimbia Zanzibar na kujificha bara. Baada ya mapinduzi, ikaamuliwa Karume aliongoze Baraza la Mapinduzi kwa heshima tuu lakini power halisi zilikuwa zishikwe na Okello, Mnganda. Hili lilimuogopesha Karume, akamwambia Julius amuite Okello Dar, Tarehe 14 January 1964, baada ya ile picha ya pamoja ya Baraza la kwanza la Mapinduzi, John Okello alitwa Dar na masikini kumbe ndio ilikuwa safari yake ya mwisho.
  Taarifa za ujio wa Okello Dar zilizagaa ambapo wajeshi walimsubiri kama shujaa.
  Okelo alipofika tuu bara, badala ya mapokezi ya kishujaa, alipokelewa na detention kitu kilichowatia wazimu wajeshi ambao nao tarehe 18-20 Wakafanya Maasi na sasa ilikuwa ni zamu ya Julius kutoroshwa kwa boti kufichwa Zanzibar.Jaribio likazimwa, jeshi likavunjwa na kuundewa upiya chini ya Sarakikya.
  Upande wa Zanzibar, ikumbukwe Karume (Mmalawi) hakushiriki physically aliwekwa tuu sasa aliwageuka wenzake akajipa madaraka yote in full na akawa hasikilizi tena ushauri wala cha mtu, ni yeye na Julius tuu.
  Hata uamuzi wa kuungani aliufanya Karume sio kwa mapenzi na wabara, bali convenience ya usalama wa Zanzibar dhidi ya maadui nwa ndani, waliofanikisha mapinduzi na maadui wa nje, manowari ya Muingereza ulikuwa umeshatia nanga Lamu.

  Baada ya Karume kujitwalia madaraka yote, yako maovu aliyoyafanya ambayo hata Julius hakuyaunga mkono, alisitisha utawala wa sheria, aliyonga kila aina ya wahalifu. Aliruhusu weusi wajitwalie vibinti vya kiarabu kwa kuwabaka, ikumbukwe baba zao ndio waliochinjwa wakati wa mapinduzi, no wonder kwa nini Wazanzibari wana jazba sana.

  Ndipo mipango ya kumfix Karume ikafanywa ndani kwa ndani, azma iliyotimizwa 1972. Wako watu waliongamia akiwemo Shamte, baba wa Mwandishi/Mhariri wa Makala wa gazeti la Mwanachi na corespondent wa Sauti ya Ujerumani, Deustche Welle (Dochi Vella), Bi. Hawra Shamte.
  Abdulrahaman Mohamed Babu na Col. Mahafudh waliepuka kifo kwa kukingiwa kifua na Julius, walitiwa kizuizini na kusalimishwa roho zao kwa Babu kukimbizwa uhamishoni London na Mahafudha kuchukuliwa na Samora.
  Aliyekuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Makamo Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora, Mahafudha Hamid Alley maarufu kama Untie Ummie, ni binti wa Col. Mahafudh, na wanaomfahamu huyu mama kwa karibu, ni miongoni mwa wanawake wachache wa shoka toka visiwani Zanzibar wenye misimamo isiyotetereka kwa jambo wanaliamini.
   
 8. Amosam

  Amosam Senior Member

  #8
  Sep 13, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kumbe ndio maana kazaa kitoto cha kiarabu kinaitwa AHAAD MESKIR aliyekuwa anaishi Uiengereza na baadae kurudi TZ kuwa mkurugenzi wa KNIGHT FRANK(T)LTD.Mmambo hayo!
   
 9. m

  mzanganyika JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 257
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Regardless of what party you support or oppose, my argument is that as long as you betray those who are with you, you will never be trusted by initial beneficiaries of your disloyalty.

  So hata hama angesaliti ASP na kujiunga chama kingine hicho chama kingine kingekuwa na mashaka naye.

  Ndio maana karibu wote wa Umma Party hawakuaminiwa with very few exceptions kama Dr. Salim ambaye naye pia alipewa nafasi za kibalozi ili asiwepo nchini kwa muda.

  Hayo ndio yaliyomkuta.

  Hata Okello naye hakuaminiwa na ndio maana alifukuzwa.
   
 10. Kamanda

  Kamanda Senior Member

  #10
  Sep 13, 2009
  Joined: Dec 5, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Mengi yatasemwa na kuandikwa, lakini itoshe tu kusema kuwa Mahfoudh (Mahafudh) ni miongoni mwa mashijaa wa Zanzibar ambao hawakupaswa kupotea, tena baya zaidi kufia na kuzikwa uhamishoni. Tutafakari namna ya kurejesha baadhi ya mifupa yake (kama ipo) na izikwe kwa heshima zote. Kama Mocambique wanamkubali na kumpa heshima kubwa namna hiyo, iweje nyumbani hakubaliki? Au ndiyo nabii hakubaliki kwao?
   
 11. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Pasco, usizungumzie juu ya utawala wa sheria when you talk of Zanzibar. Hayo aliyokuwa akiyafanya Sultani kabla ya Mapinduzi yalikuwa ya sheria au tumeyasahau leo? Maovu ya Sultani yasingeliweza kuondoshwa kwa kutumia utawala wa sheria. Utawala wa sheria is a way to enslave the masses! Hilo unalijua, kwani kwetu Danganyika, with a rule of law ufisadi will always shine among our midst - wether we are under CCM, Chadema, CUF, etc!
  Kusema kwamba Karume hakushiriki Mapinduzi ya Zanzibar is to tarnish the history and the revolution of Zanzibar. Mapinduzi sio kurusha mawe au kufyatua risasi, else sote tungelikuwa wana-Mapinduzi. There was a lot behind organizing the revolution than what we saw on January 12th. Without Karume the Zanzibar revolution would have failed and I am damn serious about this!. Yule jamaa alikuwa kweli shujaa, bila ya yeye bado ndugu zetu Zanzibar mpaka leo wangekuwa wametawaliwa na Sultani. Kweli akina Natepe, Said Washoto, Bavuai, Mahfudhi walifyatua risasi za mwanzo, but the brain behind them was Karume and that is why he was whisked away to DSM for the sake of the success of the revolution. He never fled to DSM as you suggested. He was taken by the ZRC to DSM for the good sake of the revolution itself.
  So, what if Karume came from Malawi? Kafanya mengi kuliko wewe unaetoka Mbeya au hao mafisadi wetu wanaotoka Monduli au mimi ninaetoka Songea. Without Karume downtown Zanzibar would still have been a gutter till this date as left by the Sultan. Kaondoa vibanda mjini - nani mwengine kafanya hivyo???? He was also an economist japokuwa hakufika shule na pesa zake ndio tulizoshindia vita ya Kagera na kuweza kumuondoa yule Nduli (Iddi Amin).
  So, please, let's not besmirch the good name of Karume!
  Karume was a sacred person - hata Nyerere akijua hivyo. Please don't touch his name in unreliable stories. Mimi sio CCM, else nisingelikuwepo hapa, wala sio CUF. Mimi ni Mwana-Chadema halisi, but I know our past and I will never mingle it with any party feelings!
  Mchana mwema Bwana Pasco!
   
 12. N

  Nkazahau Member

  #12
  Sep 13, 2009
  Joined: Apr 26, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sijui source yako ya hii habari inatoka wapi lakini it's a well known fact kwamba hakushiriki na kwamba kuna strong evidence kuonyesha hivyo, kuna vitabu vimeandikwa na independent writers (sio wana mapinduzi au waliopinduliwa) kuhusu hili jambo visome halafu come to your own conclusion, kimojawapo kinaitwa "Zanzibar Revolution: An American Cold War Tale" by Don Peterson, huyu Don Peterson alikuwa ni Mmarekani pekee aliekuwepo ubalozi wa Marekani Zanzibar katika kipindi chote kabla na baada ya mapinduzi na alishiriki katika majadiliano baina ya Revolutionary Council na serikali za Marekani/UK, majadiliano yalihusu mambo mengi yakiwemo kuwaachia raia wa nchi hizi kupanda manuwari ya kimarekani iliyokuja kuwachukua na pia kuhusu Marekani/UK kuyatambua mapinduzi, nchi hizi hazikuyatambua mapinduzi na ilipita zaidi ya miezi miwili mpaka kuyatambua!!!!. Yeye kwa ufupi anasema kuwa hata katika majadiliano yao kiongozi alikuwa ni Okello na sio Karume, uamuzi wa mwisho ukitoka kwa Okello, sasa kama wewe ndio kiongozi wa Mapinduzi inakuwaje maamuzi ya mwisho anakuwa nayo Okello - inaeleweka hii?.

  Vile vile katika chama cha ASP kulikuwa kuna kundi ambalo lilitaka kufanya kila njia ili chama hicho kitwae madaraka na kundi ambalo lilitaka ASP iheshimu mfumo wa siasa uliokuwepo (akiwemo Sultani) na wafanye mgomo baridi ndani ya baraza la kutunga sheria (bunge) la Zanzibar, Karume alikuwa kwenye kundi hili la mgomo baridi na wala hakuwafiki mambo ya fujo pengine akiogopa yatakayomfika pindi wakishindwa.

  La mwisho na ombi kwa wale wanaoweza wamuulize Natepe ukweli ni upi, nasikia keshasema kuna kitabu kakiandika kuhusu mapinduzi na kitachapishwa akishafariki maana anaona wasaliti wa mapinduzi leo wanaitwa wana mapinduzi!!!!! - habari ndo hiyo.
   
 13. S

  Shwari Senior Member

  #13
  Sep 14, 2009
  Joined: Jan 12, 2008
  Messages: 189
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  True historical account.

  Thank you very much.

  Col. Mahfudh was also loved by junior officers and rank and file. I witnessed this at the officers' mess in Upanga when I was at Tambaza High School (1969 - 1970). I knew some army officers there.

  Idi Amin is reported to have said the only person he feared in Tanzania was Colonel Mahfudh.

  Great soldier and military strategist. Fearless. And a true African patriot not only in Tanzania but across the continent.

  Will always be proud of him.

  Asante sana kwa kumkumbuka shujaa wetu huyo.
   
 14. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  <Sijui source yako ya hii habari inatoka wapi lakini it's a well known fact kwamba hakushirik>

  Nkazahau, you don't need to be Che Guevara to understand that you don't send your marshalls, lieutenants and your top brass to the front line. What will happen to your mission if they are killed? How would you continue with the war? Because Nyerere was not seen in a helmet in Kampala when we took it over, this didn't mean that Nyerere did not take part in that war or that he played an insignificant role! It is absurd and sheer stupidity to expect Karume physically taking part in the street fights on January 12th.
  Msinichekeshe jamani. Mnajua nini kilitokea Zanzibar after the furore of 1961? Natepe mwenyewe anajua vizuri the part played by Karume in the emancipation of Zanzibar.
  Take it from me, without Karume there would not have been a revolution in Zanzibar. Nkazahau, it was necessary to create a fake division in the ASP at the last minute before the revolution. That was a millitary strategy to confuse the Sultan and his henchmen. Kweli Karume hakuwa anapenda fujo, but he did realize that, that was the only alternative in order to rid the Isles of an oligarchic regime.
  Hapa kwetu Danganyika pia hatupendi fujo, lakini bila ya kutokea fujo hapa hawa Mafisadi wataendelea kutuuma milele na kwahivyo kazi ni kwetu!!!
  Okello alitumiwa tu kama alivyotumiwa Nyerere kukubali Muungano haraka haraka. Karume hakuwa anautaka Muungano isipokuwa kwa faida yake tu. Amir Jamaal angelikuwa hai angetueleza mengi kuhusu Karume. How can you banish a Union Finance Minister from one part of the Union? Hayo yalimkuta Jamal na akaitwa CHORI na Karume pale alipotaka kuunganisha foreign reserves za Visiwani na za Bara. Nyerere hakujua amfanye nini the revolutinonery Karume. Zaidi aliambiwa Azimio lake la Arusha limalizikie Chumbe - a place about 5 miles from the Zanzibar harbour.
  Karume hakuwa shujaa tu bali he was also a very clever guy na kama wasingelimua ile 1972 basi Nyerere angelikuwa na kazi kubwa sana. Kama pale alipoachia Urais Nyerere angempa Karume kuwa Rais wa Tanzania, basi nasi Wadanganyika leo tungelikuwa huru kikweli - sio huu uhuru wa bandia tunaobandikwa na hawa MAFISADI. Tungelikuwa tunajivunia Udanganyika wetu leo kama wenzetu wanavyojivunia Uzanzibari wao!
  Japokuwa katika hio miaka 8 (yake) Karume kafanya mabaya mengi Visiwani, lakini hayakutimia hata one millionth part ya mabaya waliofanyiwa ndugu zetu Zanzibar chini ya utawala wa Sultani.
  Mungu amlaze Karume pema Peponi!
  AMIN!
   
 15. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  Duh!!!!! hii historia tunapelekwa to and fro,sasa which is which,tunashindwa kujua ukweli uko wapi,IT seems our history is littered with inaccuracies and needs to be rewritten.In the meantime we will continue feeding on crumbs and jump to our own conclusions.All in all many thanks to all contributers.
   
 16. N

  Nkazahau Member

  #16
  Sep 14, 2009
  Joined: Apr 26, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nafahamu kuwa hupeleki kiongozi vitani lakini baada ya mapinduzi kutokea kwenye vikao vya mwanzo vya majadiliano na mataifa makubwa (ambavyo wote walishiriki) Karume hakuwa na sauti mbele ya Okello, sasa wewe kama ndio amiri jeshi mkuu kwa nini unamwachia lieutenant wako atoe maamuzi yote?, hii ni sawa na kumuona Nyerere anamuachia Brigedia Peter Marwa atoe maamuzi yote kwenye vikao walivyoshiriki pamoja baada ya kuikomboa Uganda, sasa kama wewe ndio field marshal vita vishaisha kwa nini huonekani kuwa kiongozi mbele ya lieutenant wako?, jee unajua kwamba mwenyekiti wa kwanza wa baraza la mapinduzi ni Okello na sio Karume? duh. Jee unajua kuwa wiki kabla ya mapinduzi kulikuwa pia na mgawanyiko wa kiuongozi ndani ya ASP baina ya Karume na Othman Shariff na chama kilikuwa tayari kinasambaratika na hakikuwa na uwezo wa kukaa chini na kupanga hata kikao cha ndani mbali mapinduzi?, ok tuseme na mgawanyiko huu nao ulifanyiwa usanii tu ili umzibe macho sultani, sasa ilikuwaje basi baada ya Okello kuwaita na kuwapatanisha Karume na Othman Shariff ili wapate kuongoza nchi bado Karume alifanya kila njia kuona kuwa Othman Sharif anakuwa mbali na madaraka Zanzibar mpaka hata kufika Othman Shariff akauliwa. Kwa mtanganyika nadhani tayari unaanza kujiuliza ni nani Othman Shariff.

  Karume alikuwa na average intelligence, alikuwa ni layman with a good common sense - period. Angalia kila alichokifanya utakiona kuna common sense lakini hakuna deep understanding, nyumba alizojenga, na mengi aliyoyafanya ni mazuri lakini hakuwa anafahamu vipi ata sustain vitu hivyo au what is the long term implications of his ideas na ndio maana si miaka mingi baada ya uongozi wake vitu vingi alivyofanya vilianza ku collapse au kuleta matatizo (ukiwemo muungano).

  Tatizo la ndugu zetu watanganyika ni kuwa hamuielewi vizuri historia ya Zanzibar lakini nyinyi munajifanya ndio wataalamu na madaktari wa kila baya liliopo Zanzibar. Historia halisi ya Zanzibar imo kweye vichwa vya watu walioishuhudia haya mambo na sio hiyo ya kwenye vitabu vya ushabiki wa kisiasa. Cha kusikitisha ni kuwa kwa hapa Tanzania hakuna mtu hata mmoja alieishuhudia historia hii ambae yuko tayari kuielezea bila kuongeza chumvi za kisiasa, kila mmoja akiwemo Salim Ahmed Salim wanaogopa kumwaga unga wao, hii inanyima future generations haki yao ya kuujua ukweli.
   
 17. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ndugu Nkazahau, Kwa kweli mimi sina haja ya kuuendeleza huu mjadala. Karume ni wenu nyinyi na kama mnamuona hakufanya kitu hilo ni lenu nyinyi. Sisi katuletea balaa la milele. Kama unavyosikia kuwa Pemba jana vurugu zishaanza tena. Zanzibar to us is a thorn in our ass! Kama nyinyi hamuutaki Muungano sisi hatuutaki mara mia. Mnatutia aibu internationally na huo ugomvi wenu baina ya wapemba na wazanzibari usiokwisha maisha &#8211; katika kila uchaguzi!!!.
  Ø[FONT=&quot] [/FONT]chama kilikuwa tayari kinasambaratika na hakikuwa na uwezo wa kukaa chini na kupanga hata kikao cha ndani mbali mapinduzi?, Sasa unatueleza Mapinduzi yalikuwa organized na Hizbu wenyewe?
  Othman Sherrif, Moyo, Idiria, Hanga na mlevi Jumbe na wengine hawakujua mipango ya Mapinduzi. Karume alikuwa hawaamini wasomi tokea hapo mwanzo, kwani wangetoa siri. Karume aliwaamini akina Seif Bakar, Saidi Washoto, Bavuai, etc - watu ambao hawakupita shule kama yeye. In fact kama Karume angelijua kuwa atakufa siku ile, basi angelimuachia urais wa Zanzibar hayati Seif Bakar!

  Ø[FONT=&quot] [/FONT]Karume alikuwa na average intelligence, alikuwa ni layman with a good common sense - period. Angalia kila alichokifanya utakiona kuna common sense lakini hakuna deep understanding,
  Sasa tueleze ni kipi kilichofanyika tokea 1972 ambacho kina deep understanding na sustainability hata tunafika kusema kuwa Karume yeye alikosea? Ni hizo picha za video za porno za wasichana wa ki-zanzibari tunazoziona nje siku hizi? Kukosa Karume Michenzani ingelibakia bwawa la maji machafu mpaka leo. Kukosa Karume TV isingelifika Zanzibar milele. If you say that is an average intelligence, then it is better to have that. Common sense is indeed very uncommon with many people. Only intelligent people like Karume have common sense. Most of us don't have it though it is said to be common!.

  Ø[FONT=&quot] [/FONT]jee unajua kwamba mwenyekiti wa kwanza wa baraza la mapinduzi ni Okello na sio Karume?
  That makes sense. It took days to find out that the revolution succeeded. Sasa kama Karume angelirejea haraka haraka na siku yapili mngereza kaleta majeshi je ingelikuwa vipi? Nyerere hakutaka Karume arejee Zanzibar siku yapili baada ya Mapinduzi wakati Mapinduzi yalikuwa hayajatambulika na ndio maana akamueleza Karume angojee kwanza kule Bagamoyo mpaka mambo yakae sawa na hapo ndipo alipopata ukumbi Okello ili pasiwepo vacuum!

  Okello katokea Pemba alikokuwa akipiga matuta na alikuwa hana mtu Zanzibar anaemjua na kwahivyo asingeliweza ku-organize mapinduzi. Pia Okello asingeliweza kumjua yule ndugu yetu Mchaga Edington Kisasi (Police Officer in the Sultan's army) ambae ndie aliyetoa bunduki Bomani na zikafanikisha Mapinduzi. Hio kusema mmepindua kwa mapanga na mashoka ni nyimbo za watoto wa shule tu. Mapinduzi bila ya huyu Mchaga yangelikuwa magumu, kwani yasingelipata silaha ya kuenda kuiteka ile kambi nyengine.

  [FONT=&quot]Jambo alilokosea Nyerere ni kuwa pale Karume alipotaka Muungano ili asalimike na wamanga Nyerere angelimueleza kuwa achanganye nchi kabisa na sio kumkubalia nusu nusu kama walivyofanya. Karume was not interested in the Union, lakini Nyerere [/FONT]
   
 18. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Jambo alilokosea Nyerere ni kuwa pale Karume alipotaka Muungano ili asalimike na wamanga Nyerere angelimueleza kuwa achanganye nchi kabisa na sio kumkubalia nusu nusu kama walivyofanya. Karume was not interested in the Union, lakini Nyerere inaonesha hakujua hivyo. Nyerere kama angelimueleza Karume achanganye nchi yake na Tanganyika moja kwa moja na kuwa Zanzibar na Tanganyika zisiwepo tena, Karume ingelibidi akubali, kwani alikuwa hana njia nyengine ya kutawala. Without the Union Karume would not have survived even for a day. Karume knew that and now someone is saying that he was a person of an average intelligence!
  Nyerere aliharibu kuiua Tanganyika na kuibakisha Zanzibar, matokeo yake ni kuwa leo Zanzibar is a big problem to us!!!. Ilibidi amueleze Karume kuwa waziue nchi zote mbili. Kama ingelikuwa hivyo &#8211; that is, zote mbili Tanganyika na Zanzibar kufa, basi hili balaa la mafuta mnalolianzisha hivi sasa lingelikuwa halipo na hizi vurugu za Pemba pia zingelikuwa hazipo. Pinda mnamuona adui lakini kasema kweli. Ingelikuwa vizuri kama angelikuwepo Pinda serikalini wakati ule (in 1964) na akampa ushauri mzuri Nyerere, basi leo tungelikuwa tunazungumzia mambo mengine!
   
 19. r

  rahamajo Member

  #19
  Sep 14, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 25
  Hili ni funzo kuwa wale tunaowasifia kuwa watu wema si wema katu, wema ni akina Col Mahafudhi waliopinga uonevu wakati wote na wameishia kuenziwa ughaibuni. Na bado kuna viwete wa kufikiri wanawaita wasaliti!!! Kasaliti nini kupinga uonevu??? Col ni shujaa alimpinga Sultani na hata Karume muuza nchi na muuaji pia alimsaliti!!!
   
 20. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  sasa huyo polisi aliyetoa silaha,Edington kisasi aliishia wapi? NA je huyu somebody HANGA je did he play any part katika haya mapinduzi?
   
Loading...