Ni kweli kuna wakati fulani tulikuwa tukijaribu kuwafuata wale wana-Mapinduzi (walipokuwa hai na wapo mapumzikoni -sio ulingoni) watueleze kilichojiri na walivyoshiriki siku ile- wapi hatukupata ukweli bali tulibabaishwa tu na ah. basi tukatangaza tu tena zile porojo.Tatizo la ndugu zetu watanganyika ni kuwa hamuielewi vizuri historia ya Zanzibar lakini nyinyi munajifanya ndio wataalamu na madaktari wa kila baya liliopo Zanzibar. Historia halisi ya Zanzibar imo kweye vichwa vya watu walioishuhudia haya mambo na sio hiyo ya kwenye vitabu vya ushabiki wa kisiasa. Cha kusikitisha ni kuwa kwa hapa Tanzania hakuna mtu hata mmoja alieishuhudia historia hii ambae yuko tayari kuielezea bila kuongeza chumvi za kisiasa, kila mmoja akiwemo Salim Ahmed Salim wanaogopa kumwaga unga wao, hii inanyima future generations haki yao ya kuujua ukweli.