Tangawizi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 5,171
- 3,893
Karume alirithi Zanzibar yenye Neema ....alikuta palace imejaa pesa na dhahabu baada ya kuwa Sultani kakimbia........pia wakati huo bei ya karafuuu ilikuwa mzuri na idadi ya watu haikuwa kubwa......haikuwa ajabu kumudu kufanya maendleo hayo.......lakini naamini kabisa Kama Karume angekuwa mtulivu na kuwatumia wasomi waliokuwa wamemzunguka ...Kama kina Abdulrahman Babu,Kassim Hanga ,Abdul Jumbe Mwinyi na wengine ......Zanzibar ingepiga hatua zaidi.....ya hayo magorofa ya wananchi na TV ambayo ndie imekuwa litania ya Kipimo cha maendleo
Ungeniambia ingekuwaje Karume angeendelea kuwepo miaka 5 tu mingine naona Angefika mahala angekwama kwa Aina ya uongozi wa mabavu na mauwaji.......pesa zilikuwa zinaelekea kwisha .......na kufikia Kati Kati ya 70s bei ya karafuuu ikaanza kushuka .....na Uchumi wa dunia uliyumba Sana ...na pia kulitokea njaaa na serikali za kiafrika ziliyumba kwa kutumia pesa nyingi kuagiza vyakula.....Sioni Kama Wazanzibar wangeweza kuendelea kuvumiliaaaa kuona Ndugu zao wakitoweka ....ingefikia mahala angebaki Hana pakukamata..........
When people run of ideas...wanatumia mabavu kuendelea kuwepo.