DeepSeek imeendelea kunishangaza kwenye upande wa kuchakata IDEA, niliuliza swali moja la kutengeneza APP ili AI inisaidie kuchambua na kuchora UX/UI(Figma), kwa DeepSeek ilinisaidia kuchambua ila ikashindwa kuchora kozi hiyo feature bado haipo ili lifanya vzur sana na kwenda mbali zaidi kuliko Chatgpt. Kwenye upande wa idea DeepSeek ni zaidi na uwa napenda sana kuitumia kwenye brainstorm ideas iko vyema sana. Kwa upande wa Chatgpt inachambua idea ila hajiongez zaidi kwenye kuweka features mpya kwenye idea ambayo umempa achakate, ila kwenye upande wa UX/UI ni balaa zaidi, anachora na kuandika code zake kama image ilivyochora.
Chatgpt amenitisha zaidi kwenye upande wa UX/UI(Figma) ina madini makali sana, kuhusu UX ya app unayotaka kutengeneza Chatgpt ni njia bora ya kufanikisha ndoto yako.
Binafsi uwa nauliza DeepSeek then na copy response then na paste Chatgpt anakokotoa zaidi na hapo anakuwa hatari zaidi na uwa anakuja na idea ambayo ata wewe itakushangaza zaidi na mwisho anakuuliza nikuchore UX na database anakupa structure mzima. Hivi vitu kwa developers vilikuwa vigumu sana ila sasa ni very simple , unaweza kufanya project yoyote kama unajua ABC ya programming na kuunda APP kali zaidi na ya kisasa zaidi.
AI zilizo sasa ukiweza kuzitumia vizuri ni rahisi sana kutapa manufaa zaidi na kubadilisha maisha yako, kuna AI za kuchapa code kama Cursor , hii AI inakusaidia kuchapa code kwa kuweka UI/UX (Figma) au prompt ni kama github autopilot kwa watumia wa VS CODE, ukikosea ina correct kama kuna errors ina correct bila wewe kuchapa code. Ina rahisisha sana maisha ya programming, maana programming ni so kama unakuwa unachapa code from the scratch.
Nilijaribu Grok ila nimeona bado sana kwenye kuchambua idea nimeiteka, saiv ni DeepSeek na Chatgpt plus Cursor, kama ukilipia Chatgpt na Cursor utafurahia maisha ya coding na utafanikisha project zako kwa haraka zaidi.