Coco Beach: The project has consumed 260m/- from its concept design phase to completion of a Master

Coco Beach: The project has consumed 260m/- from its concept design phase to completion of a Master

hili ni tatizo,mtu kwenu mpwapwa ambako hata bwawa hakuna unajifanya kuongelea mambo ya beach...private beaches zinalipiwa,nenda beach kimba ya mikadi kigamboni huingii hadi utoe 2,000/=

Usie jua ni wewe. Hakuna private beach Tanzania. Beach zote ni Public kwa mujibu wa sheria. Hao wanaowatoza wanawaonea kwa kisingizio cha kuwa mnatumia huduma zao.

Amandla.....
 
Kwenye hili sakata ni Manji tu anaonekana na sio wengine kuna nini?

Huyo jamaa ni monster of corruption in current Tanzania. Anachagua ''windo'' tamu lenye faida ya kuafa mtu, ana-set plan, ana-attack kwa kutumia kiasi chochote cha fedha anachoona kitarudi huku yeye akijiweka mbali na haachi loopholes za kuweza kumshtaki hata siku moja. Lakini kwa Magufuli nadhani amefika kwani watu wa aina hii anawajua sana na hacheki nao!
 
Magufuli alikurupuka alivoshauriwa lakini ukweli ni kuwa hii project muhim sana na kwann hvi wabongo sisi ni watu wa mihemuko

Hii projekt haina umuhimu wowote. Kama ingekuwa na umuhimu wangeiweka wazi mapema ili wananchi waweze kutoa maoni yao. Wangetueleza Environmental and Social Impact Assessment imefanyika lini. Lengo la huu mradi ni kugawa viwanja kati ya Sea Cliff na Golden Tulip ili wajenge mahoteli na makasri. Eneo hilo halina beach ila ni nyeti kutokana na kuzuia mmonyoko wa ardhi. Ukitaka kujua athari ya kujenga hapo kawaulize Police Officers Mess, Sea Cliff n.k. Watu wamekuwa wakinyemelea eneo hilo kwa miaka mingi na leo hii wanatumia haya mashirika yetu ya umma yenye mawazo ya mafanikio ya haraka haraka ( NHC ni culprit mkubwa katika kuharibu heritage ya miji yetu) kufanikisha uovu wao. Wanajua sisi tunapenda mno majibu mepesi kwa maswali magumu. Huu mradi uzuiwe. Haufai na utaharibu huu mji beyond repair.

Amandla.......
 
Bado nawaza JE PUBLIC BEACH ZOTE NI ZA WAWEKEZAJI? DIAMOND KASEMA JE UTANIPENDA..MI NASEMA JE TUTABAKIWA NA NINI....KUSEMA HUNA HELA NA MWANAO ANATAKA KWENDA BEACH NA VIINGILIO JUU..ATAISHIA KUTAZAMA NJE NA KUFUKUZWA AKISIMAMA SANA....KAMA NAIONA TANZANIA YANGU WENYE ZAMANA NDO WENYE MAISHA AU.........BADO NAWAZA TUUU
 
Watu waache ushamba..ufukwe wa coco beach hauwezi kubaki hivyo hadi yesu arudi .....iwapo itaendelea kuwa open beach wacheni iendelezwe...

Kuna tatizo gani ukibaki hivyo? Copacabana wamejenga nini kwenye ufukwe wao? Bondi Beach wamejenga nini kwenye ufukwe wao?

Tusipende kudanganyana. Mvuto wa Coco Beach ni unspoilt nature. Kuanza kujenga ni kuiharibu.

Amandla.....
 
Mentality za Kiswahili ....Kama hawatatoza kiingilio hiyo mihogo ya buku ....kwanini isiwepo ...itakuwapo Tena kwenye mazingira safi ........pale coco beach kwa Sasa hakuna Choo wala Maji ya kunawa kabla ya kula na bado mnataka pabaki hivyo hivyo

Hiyo mnayoiita Coco Beach ilikuwa ndio changing room kwa ajili ya Oyster Beach. Ilikuwa na vyoo, showers na lockers kwa ajili ya waogeleaji. Akaingia mwekezaji, the rest is history. Vyoo havipo, watu wanajisaidia vichakani. Na ndio yatakayotokea tukisikiliza ngonjera za hawa wakina TIB, NHC, Quality na watu wa aina hiyo. Hatujifunzi.

Amanda.......
 
Fundi Mchundo aliyetoweka muda mrefu lakini busara zake zimeongezeka mara dufu! Hongera sana na asante. Project za aina hii ni lazima wakazi wangeshirikishwa kwa sababu ndio wadau wakuu. Tanzania tuna tatizo la viongozi kujiona wana mandate ya kuamua masuala makubwa kwa niaba ya wengi! Maslahi binafisi siku zote ndio huwapofusha kwani wanajua wakiwashirikisha wananchi wataambulia tupu!
 
Anahangaika na beach yetu.... Asia hamna beach? Analialia eti nchi yake Tz haimthamini.. sie tuna watu hivyo? hata Seith Harbinda naye alijifanya mhehe... sina imani na hawa watu... ofisi zao wamejaa wao tuu weusi tunabaki vibarua....
Usiombe kufanya kazi kwa hawa..
Sabani leta box ile,Sabani rudisha hii kule, Sabani namna gani Sabani, nakata mshahara yako...
 
Anahangaika na beach yetu.... Asia hamna beach? Analialia eti nchi yake Tz haimthamini.. sie tuna watu hivyo? hata Seith Harbinda naye alijifanya mhehe... sina imani na hawa watu... ofisi zao wamejaa wao tuu weusi tunabaki vibarua....
Usiombe kufanya kazi kwa hawa..
Sabani leta box ile,Sabani rudisha hii kule, Sabani namna gani Sabani, nakata mshahara yako...

Hahahahaha Mkuu kumbe tuko wengi, bora hiyo ya leta box... Ukikuta nyumbani kwao wanavyowapelekesha Dada zetu na kaka zetu na wadogo zetu hutatamani hata kuwasogelea. Utasikia Sabani Toto kunya.... Sabani vyombo chafu...hajamaliza utasikia wewe Fanya Kazi polepole bana kimbia kalete clips yenye pilipili mingi... sawa?
 
Watajiju,sisi walala hoi tunataka beach yetu ibaki hivo hivo,

mkuu ondoa mawazo yakujiita mlala hoi!, uboreshaji ni muhimu, tatizo zabuni ya kuwapa waboreshaji umepelekwa kimagumashi. inawezekana mwisho wa zabuni kutangazwa manji akamilikishwa eneo hilo. Kwenye maelezo hayo, ukiyasoma yote Manji ambaye kwa sasa anajulikana Mradi wote ni wa kwake, lakini hatajwi moja kwa moja kama ndiye mmiliki, inawezekana alikuwa kwenye category ya wafadhili wengine, lakini ujanja ujanja, ungepelekea eneo kumilikishwa kimagumashi kwa Manji.
 
Anahangaika na beach yetu.... Asia hamna beach? Analialia eti nchi yake Tz haimthamini.. sie tuna watu hivyo? hata Seith Harbinda naye alijifanya mhehe... sina imani na hawa watu... ofisi zao wamejaa wao tuu weusi tunabaki vibarua....
Usiombe kufanya kazi kwa hawa..
Sabani leta box ile,Sabani rudisha hii kule, Sabani namna gani Sabani, nakata mshahara yako...

Tehee!teeteeeehee!
 
Naona mmejipanga Leo kutumia Jamii Forum kumtukana Mhe. Rais kwenye hili sakata la Manji???? Mmeanzisha thread kabisa kwa kazi hiyo!!!!

Unapozungumzia mtu ata kodi kioski kwa $5,000. Je unategemea atauza mihogo ya Tshs. 1,000?? Na hiyo kodi atalipaje na bado apate faida???

Kusema akili ya mhindi inafanya kazi ni kuwatukana waswahili, kuchochea ugomvi kati ya wahindi na waswahili na baya kuliko yote ni kumtukana MHE. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR. JPM

Ili ukusanye Tshs. 17billion plus kwa mwezi unadhani market niche yako itakuwa watu wa chini???? Hivi hujui wenye pesa zao wanaenda Seacliff, slipway, Mediterranean, fish market, fukwe za Kigamboni nk

Akili ya viongozi wa Kinondoni imeishia hapo?? Hawana brain ya Kufikiri watatengenezaje miradi mingine?? Acheni unafiki kama mmechukua pesa za watu rudisheni.

Umemalizia kwa kusema "THE BEST BUSINESS MAN IS THE ONE WHO USES OTHER PEOPLE'S MONEY TO MAKE MONEY". Hapo umenikumbusha hotuba ya Mhe. Rais siku alipofanya mkutano na wafanya biashara aliposema Ma Benki Kama CRDB wanatumia pesa za Serikali kufanya biashara na Serikali. Halafu tunawapongeza!!!! Ndio maana nchi hii ni masikini kwasababu ya ubinafsi Kama huu.

HILI NI J?KWAA LA WASOMI, HIVYO BASI WEKENI HAPA BUSINESS PLAN YENU TUICHAMBUE. Mpaka sasa mnapiga tu porojo na kukaa vikao vya kumdhalilisha Mhe. Rais na kupanga mikakati ya ku counter attack maamuzi yake!!! Watch out!!!

Nawashauri muache kupambana na DOLA ya Magufuli........

Queen Esther



All commercial properties/ facilities I. E Restaurant, coffee shops etc public will have free access to all these facilities so they can spend monies, imagine you will have to rent kiosk for $5000/- per month while the high end facilities will be more than that. Parking fees on daily basis,This is where the 17B ++++ will be generated. Akili ya mhindi inafanya kazi. Kuna u semi " THE BEST BUSINESS MAN IS THE ONE WHO USES OTHER PEOPLE'S MONEY TO MAKE MONEY"
 
Paragraph ya mwisho ..." through various means including interested parties..." Ndio Manji anaingia hapo. Wake up!
Yaan mtu ambae hata hatajwi ndio anakuwa kinara Wa kuupigania mradi?! Hiyo open space ingeshavamiwa/kuuzwa isingekuwa magufuli, tuna bahati Sana!
 
ndo dunia ilivyo,bahati kumbe mradi una wawekezaji pamoja na mashirika ya umma,nchi zingine unakuta ni project ya mtu mmoja tu,

mi naamini kama watashusha kitu cha uhakika watalii lazima wamiminike hapo,we unafikiri moshi pangekuwa na beach si pangekua kama dubai kwa sasa:matokeo yake watu wanapanda mlima kilimanjaro then wanakwenda kujirusha fukwe za mombasa,TUNAPOTEZA mapato hapo

siamini kuwa mpk raisi kulizungumzia hili atakuwa hajui anachosema. yeye ana details zote zaidi ya hii article. tumwache afanye kazi . manji huyu huyu alinunua eneo la pale karibu na aluminium africa pale karibu na tazara sokota kwa ulaghai na kuwaacha mafundi kwenye mataa.
 
so what is the problem there.?

I mean kumbe mradi sio wa manji,yeye anawa miongoni mwa partiners katika mradi huo,

What is the problem there? Ikiwa huyo interested parties ndio kainvest hela nyingi kuliko wote, yeye ndiye atakayekuwa na say kubwa. Kwa nini wasiwataje hao interested parties ni kina nani? Ni technicality imetumika hapo, kuonesha kwamba offer ilikuwa open for any interested party.

The main point is watuwachie wanyonge tu enjoy Coco Cabana yetu in form of nature. Kama wana nia njema wafanye project ya kusambaza maji salama na tuko tayari kulipia, wasijifanye wajanja kutaka kuiba ardhi ya wanyonge. Mbona projects ziko nyingi tu za kimaendeleo. Hata kama ataamua kuingia kwenye kilimo na kulisha Tanzania nzima basi ni jambo jema na tutamuunga mkono. Bei ya chakula itashuka na faida atapata
 
hv jaman manji ni diwani wa wahindi au watz?
mbona huyu jamaa ni mfanyabiashara maarufu sana, Ina maana akipigiwa cm yamzigo wake umekatwa nje ya nchi na muda huo huo yupo kwenye kusuluhisha migogoro itakuwaje? mbona cpati picha vile.
 
Project mzima ni very potential... kwanza mimi ningekuwa ndo mfanya maamuzi, hiyo project ingekuwa ishakuwa implemented miaka kadhaa iliyopita. I usually don't give the goddamn sisi maskini stuff to be an obstacle for better utilization of our resources.

Wakati wa uchimbaji madini ulipokuwa unaanza watawala wenye akili kama zako walikuwa wanasema Ujinga kama huu lkn Leo wanaona Aibu wanasingizia hatukuwa na wataalamu wazuri wakusoma Mikataba Pumabafu......
 
Wakati wa uchimbaji madini ulipokuwa unaanza watawala wenye akili kama zako walikuwa wanasema Ujinga kama huu lkn Leo wanaona Aibu wanasingizia hatukuwa na wataalamu wazuri wakusoma Mikataba Pumabafu......
Na wewe endelea tu na hayo mawazo kale yako kama yale "tuna haraka gani ya kuchimba madini, kwani madini yanaoza....!" Yaani baada ya kuangalia ni namna gani jambo linaweza kufanyika kwa manufaa ya taifa karne ya 21 bado watu mna simulizi za madini hayaozi.... sisi maskini tutaishi wapi.... that's fantasy world!!

Kwanza hao maskini mnaojifanya kuwatetea ingekuwa busara kuwaambia waendelee kupiga kazi bila kuchoka ili waupukani na umaskini badala ya kutaka shughuli za kiuchumi zisifanyike ili eti maskini waendelee kuuza mihogo sehemu husika!!!
 
nishasemaga sijui ni nani anawapa nafasi hawa wahindi,waarabu na wachina kwenye mambo ambayo hayawahusu,hizi ten percent zinaumiza sisi wanyonge wa chini,kiwacha cha waislam akitake yeye,beach yeye,naomba JOHN POMBE magufuli aziue hili jambo,ikibidi ianzishwe petition ya sisi walalahoi tuzuie huyu jamaa.mimi ananiboa sana
 
Back
Top Bottom