Coco Beach: The project has consumed 260m/- from its concept design phase to completion of a Master

Coco Beach: The project has consumed 260m/- from its concept design phase to completion of a Master

Nimeipitia hii thesis na kujiuliza swali hivi Garduates wa kitanzania especially wale waliomaliza ARDHI University hawana uwezo wa kufanya utafiti wa aina hii?

Je Wataalamu wa manispaa ya Kinondoni wana uwezo wa kufanya assessment ya mradi kama huu?

Je manispaa hii ilishindwa au inashindwa kufanya study ya namna hii?

Majibu yangu ni confusion juu ya confusion inayosababishwa na pengine uwezo mdogo wa waajiriwa wa serikali au uzembe wa waajiriwa wa serikali au uvivu wa wasomi wa kitanzania au ni kukosekana kwa uzalendo kati ya jamii ya kitanzania au kuendekeza rushwa na ufisadi tu.

Kiufupi naweza kusema huwa napenda vitu vya hisani ya watanzania...
Ingawa pia siwezi kuignore ukweli kuwa at times we need to make decision basing on best available evidence iwe kutoka kwa mtanzania au mwengine yoyote yule.

Nikirudi kwenye thesis yenyewe naona kuna limitation moja kubwa ya kukosekana kwa maelezo ya gharama za kuujenga na kuusustain mradi ...hili ni jambo muhimu ambalo as a scientist au msomi huwezi ukaliacha kuliongelea kwani ni muhimu kupita maelezo especially katika nchi ambayo haina ukwasi wa kujitosheleza hata kwenye msosi.

Waandishi wa utafiti huu au mradi huu wamelitendea haki taifa katika eneo moja muhimu kwamba kwa vyovyote vile iwavyo eneo hili au mradi huu ni lazima ulenge kwa watumiaji wote yaani umma lakini kimsisitizo ni umma ambao ni wa walalahoi.

Hii ni fact au uzuri wa mradi huu basing on proposal ya wadada wa kisweeden.

Ni mtanzania fisadi tu ambaye hatakubaliana na hawa kina dada katika hilo.

Hapa kuna swali nyeti inabidi tujiulize kama GTs au wasomi au wazalendo....JE HIVI COCO BEACH KABLA HAIJAANZA KUTUMIWA KAMA ENEO LA WALALAHOI KUJIPUMZISHA ILIKUWAJE?

NI NANI ALIYEANZISHA IDEA YA KUFYEKA MSITU NA KUWEKA MANDHARI AMBAYO LEO HII WATWAJWA WA UFISADI WANATAKA KUWEKEZA NA KUBORESHA??

Ni nani hasa alikuwa akihudumia eneo hili kwa kipindi chote hiki?

Ni wapi alipokwamia na sababu za yeye kukwama ni zipi?

Haya ni maswali ambayo waandishi wa mradi na yoyote yule anayejidai anataka kupaboresha ajiulize na kuyapatia majibu.

Waandishi wamenigusa walipoongelea uchafuzi wa mazingira katika eneo hili pamoja na possible solutions za kukabiliana na tatizo hili.

Mimi sio mtaalamu wa miradi au michoro ya miradi lakini kwa perspective ya mlalahoi naona waandishi wamejaribu kukidhi mahitaji ya watumiaji tarajiwa wa eneo au mradi huu.

By the way watarajiwa walio wengi wa mradi huu hawana na wala hawahitaji makuu sana ...
Utamaduni wao hautakiwi kufananishwa na wa waarabu au wazungu bali watanzania.

Kuhusu KMC/TIB na Manji

Sitaongelea sana kwani sijaona version yao ya mradi ingawa kwa maelezo machache ya waandishi hapo juu na uzoefu mdogo wa mwenendo na tuhumu dhidi ya Manji napata wasiwasi mradi wake utawaondolea access walalahoi ambao kwa mujibu wa mh Rais COCO ni kati ya maeneo machache yaliyobakia kwa kuwaliwaza wapiga kura wake ambao wengi ni walalahoi.

Halmashauri ya Kinondoni

Nawaona watumishi wa manispaa ya Kinondoni hawajafanya kazi yao kama ilivyo hulka ya watumishi wengi wa halmashauri.

Wao ndio waliotakiwa kuwa watatuzi wa migongano hii badala yake wamekuwa chanzo.

Kwa vyovyote vile nitasimama na swahiba wangu Magufuli kuwa COCO lazima iwe eneo la wazi kwa ajili ya umma wa walalahoi....njia au proposal za kutekeleza hili lirudishwe kwa halmashuri na ikiwezekana kuwe na jopo la wataalamu wa kitanzania na wapewe hadidu za rejea za jinsi ya kuliboresha eneo hilo nq mengine yanayofanania nayo.

Nitaendelea ikinibidi.

HII MADA NI KUBWA KWA WAZUNGUSHA MIKONO KWA HIYO MKAE KANDO.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 
tatizo ni kuwa wabongo hawajazoea biashara za aina hizi,
tumezoe biashara za uchuuzi sana,hii kitu mbona ya kawaida sana na inaweza kuvuta watalii wakitoka zao kilimanjaro wanakuja cocobeach kujiachia kabla hawajakwea pipa kurudi makwao,thimk how much milions of dollars that project can generate.and create employment.


Mji kama Beirut,lebanon wanapata watalii kwa mamilion kwa ajili ya watalii wanaokuja kujigalagaza kwenye fukwe zao maridadi
Mkuu tuna mbuga za wanyama za kutosha ambapo watumiaji wakubwa ni wageni pengine ni kutokana na gharama za kutembekea huko ama kutokana na utamaduni wetu.

Hii ilikuwa ni sehemu ya wabongo kujivinjari sasa unataka igeuzwe kuwa ya wageni kisa uwekezaji au kukuza ajira...!


Leo hii jiulize kwanini mdundiko haupo ?ambapo ungelindwa ungeweza kuwa kivutio cha utalii na kuulinda utamaduni wa mzaramo.

Unajua ni kwa kiasi gani kutokuwepo kwa mdundiko kumewaathiri wazaramo kisaikolojia au hata kiuchumi na kimaadili ?

Leo hii wote tunaishia disko kupumuliana hewa zenye kifua kikuu na kuharibu usikivu wa masikio ya vijana wetu.
 
Mkuu jingalao huitendei haki Ardhi University kwa kuijudge kutokana na hii project.

1. Hakuna mtu aliyewafuata hao wazungu kuja kufanya masters thesis kuhusu Coco Beach wamefanya kwa mapenzi yao. Kuna master thesis nyingi zipo pale Ardhi kuhusu mambo ya kumanage open spaces sio beach pekee. Hivyo si kweli Watanzania wameshindwa kufanya hilo unalowaza.

2.pili masters thesis ya mtu ni suala la interest, hupangiwi kwamba fanya ya Coco Beach inawezekana kabisa hao waswidi interest yao ikawa ni beach na Watanzania wengine hasa hao wa Ardhi University wakawa na interest na mambo mengine kabisa wakayafanyia utafiti kutokana na umuhimu wa jambo.

3. Ardhi kama chuo kina consultancy unit ambapo mtu awaye yeyote akitaka ushauri wa kitaalamu kwenye jambo lolote kuhusu ardhi unakaribishwa na utapewa ushauri huo. (Kama umeobserve vizuri projects nyingi kubwa za ujenzi mathalani utaona either Architect au Quantity Surveyor ni Ardhi University). Kwa hiyo suala la uwekezaji wa beach ya manispaa ni nje ya scope ya madaraka ya chuo hata hivyo kama Manispaa ingeomba ushauri wa kitaalamu ingepewa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nashukuru umefunguka!

Umesema kuna utaalamu wa kutosha hapo ARDHI university juu ya kumanage open spaces ...je uko published??

Kwa nini hutaki kukubali kuwa wataalamu wetu wa hapo UCLAS achana na ARDHI kuwa walilala mpaka leo hii wakaibuka wadada wa sweeden?

Anyways tusibishanie kwenye hili bali tujikite kwenye thesisi yao na way foward.

wewe maoni yako ni yapi?

Mimi nimeanza kusoma juu ya uendelezwaji wa beach ya Copa cabana kule brazil ili nione wapi tulipokosea au ni wapi inatakiwa serikali iende....sio kwa COCO tu bali kwa beach nyinginezo pia.
Msimamo wangu though hautapingana na maono ya Rais kwamba fukwe hii lazima iwe ya public tena ile ya kipato duni kwani ndio sehemu yao ya kujivinjari.

your proposal should and must consider hii fact.
Funguka mkuu king kan
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nashukuru kwanza niseme wazi sijasomea mipango miji wala landscape architecture nimesoma course nyingine hapo hapo Ardhi.

Pili matazamo wangu nilikuwa nimeutoa kwenye thread iliyojadili hiyo thesis.

Sio mbaya nikirudia hata hapa;

Kuna mambo ambayo nadhani watu tunayakwepa. Kuna watu hawataki wawekezaji wawepo Coco Beach wanataka ibaki hivyo hivyo jambo ambalo napingana nalo.

1. Nataka uwekezaji ufanyike Coco Beach ili iendelezwe na hatimaye kukidhi viwango vya kimazingira na usafi. Hapa mjadala nadhani uwe unatakiwa uwekezaji wa aina ipi. Nani anaweka fedha kuwekeza, je ni mwekezaji kama TIB, serikali yenyewe au tutafute sponsors kama Voda etc.

2. Hoja ya pili ni kwa nini pawekezwe. Kwa hali ilivyo Coco inahatarisha usalama wa kiafya na amani. Hakuna huduma za kimsingi kama vyoo ukiacha kile cha ile Bar moja pale na kuna wahuni wengi kupita kiasi. Sasa ni lazima tuwekeze kuboresha mazingira yale na usalama wa raia na mali zao.

Na napingana kwamba muwekezaji awe serikali kwa sababu mamilioni ya kodi za Watanzania hayawezi kutumika kugharamia starehe ya watu wachache wakati maelfu bado hata darasa la kusomea hawana.

Kama wawekezaji wanadevelop ecofriendly structures sina tatizo nao kwa kuwa as long as entrance is free na kuoga ni free najiuliza watu wanaogopa nini kuwapo kwa baa tatu au nne pale kutoa huduma, vyoo vya kutosha vya kulipia na fresh water basin ya kujissuza baada ya kuoga chumvi.

Mwisho badala ya kuipinga proposal yote ya TIB na KMC kwa nini isiwekwe ijadiliwe na kufanyiwa marekebisho?? Naamini proposal yote haiwezi kuwa mbaya.

Kuhusu gharama watu wanazohofia, nashangaa tunahofia gharama tusizozijua. Leteni kwanza gharama ndio tujadiliane affordability. Hoja ya waswahili hawawezi kuafford ni uongo. Nilitoa mfano ukienda Mikadi utagundua kuna waswahili kibao ambao almost wanalingana na waliopo Coco Beach. Pale Mikadi wameingia kwa kulipa na wameacha kwenda Coco bure. Kujificha kwenye dhana ya watu flani hawataweza kuafford wakati Kigamboni wanaafford ni kutokuwa fair.

Mwisho kuna watu wanaendeshwa na chuki dhidi ya Manji kitu ambacho si sahihi hata kidogo. Huo ni ubaguzi wa wazi na pia kuna upotoshwaji mwingine kuwa amemilikishwa eneo nao sio sahihi inawezekana yeye amepewa development and management rights basi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom