ufisadi tz ni kila sehemu.
hebu fikiria eti coca-cola hawalipi kodi! wakati huo huo wamachinga wanakabwa kufa mtu
Posted Date::6/4/2008
TRA yaorodhesha makampuni yasiyolipa kodi
Na Tausi Mbowe
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imewasilisha serikalini orodha ya makampuni makubwa sugu, ambayo yanakwepa kulipa kodi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRA, Dk Moselina Chijolinga aliwaambia wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi jana kuwa, mamlaka yake imeamua kupeleka orodha hiyo kwa serikali ili kuomba kampuni hizo zichukuliwe hatua.
''Tumeshapeleka serikalini orodha ya makampuni ambayo hayalipi kodi kabisa na yale yanayolipa kwa kulegalega kwa kuwa yanajulikana,'' alisema Dk Chijolinga.
Hoja hiyo iliamsha ari ya wajumbe wa kamati hiyo ambao ni wabunge, chini ya uenyekiti wake Dk Abdallah Kigoda, ambao waliuliza ni makampuni gani hayo ambayo yanakwepa kulipa kodi.
''Sijui kama sheria inanilinda katika hili, lakini tumeshapeleka barua serikalini inayoonyesha orodha ya makampuni yote sugu kulipa kodi,'' alisema Dk Chijoliga.
Wabunge hao walimtoa shaka Mwenyekiti huyo wa TRA na kumtaka kutaja majina hayo kwa kuwa katika Kamati za Bunge sheria inasema kuwa ana haki ya kutaja chochote.
Baada ya kuambiwa hivyo Mwenyekiti huyo aliidai kuwa kampuni ya Coca-Cola imekuwa hailipi kabisa kodi na baadhi ya makampuni ya simu za mkononi yanalipa kodi kwa kusuasua.
Hata hivyo, Dk Chijoliga alishindwa kutaja idadi kamili ya makampuni hayo mbele ya wabunge hao ambao wengi walionekana wazi kutaka kuzifahamu kampuni hizo.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Omari Mzee aliahidi kuwa serikali italifanyia kazi suala hilo mapema iwezekanavyo.