Coastal Union yatoa tamko kuwa haina mkataba na Kocha Mgunda

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
FcI6pB5X0AMBB_W.jpg

Klabu ya Coastal Union imetangaza kutokuwa na mkataba na Kocha Juma Mgunda ambaye kwa sasa anaitumikia Simba akiwa kocha wa muda.

Coastal imeeleza mazungumzo ya kusaini mkataba mpya baina yao na Mgunda yalikuwa kwenye mchakato, hivyo suala la Mgunda kujiunga na Simba ni la kwake binafsi.

Kutokana na hali hiyo uongozi wa Coastal Union umemtangaza Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Joseph Lazaro kusimamia timu kwa muda.
 
Naona Karia na Kidau wanajaribu kuficha aibu. Baada ya mtoto wao pendwa kuwavua nguo!
 
Kwa hiyo makocha wengi wa NBC premier league ni madeiwaka, kwa hiyo TFF hausiki na makocha manake kama hivyo hata mtu yoyote anweza kupiga deiwaka kwenye timu zetu za NBC.Daah huu mpira wetu kivyetuvyetu, ila tuliosoma CUBA tushaelewa.

Simba na Coast mmetisha mpo vizuri.
 
Kocha asiyekuwa na mkataba, anakaa kwenye benchi la ufundi kwa kigezo kipi? Kumbe ligi yetu inaeuhusu ma day worker (madeiwaka)
 
Mbona barua imekiri ni suala lake binafsi kwenye paragraph ya pili mwishoni
 
Hakuna anayelazimisha ubaya ila bora wangekaa kimya tu maana ndio wamechafua kabisa hali ya hewa. Yaani kocha hana mkataba halafu anaiongoza timu, kituko hiki
Mi nasemea kwa simba kumchukua kumbe ni hiari yake binafsi hana deni na coastal
 
Hakuna anayelazimisha ubaya ila bora wangekaa kimya tu maana ndio wamechafua kabisa hali ya hewa. Yaani kocha hana mkataba halafu anaiongoza timu, kituko hiki
Wangekaa kimya uzushi wenu ungekuwa na nguvu. Sasa hiyo comeback walioifanya Coastal hamjaipenda maana imeonesha hoja zenu hazikuwa sahihi.

Kueleza kwao kuwa hawana mkataba naye ni jambo baya ukilinganisha na wao kukaa kimya?
 
Kocha wa timu za Coastal Union SC na Simba SC ameondoka leo nchini na Klabu ya Simba kuelekea Malawi kuiongoza timu ya Simba kwenye mechi yake ya awali kwenye mashindano ya CAF!

Kocha atakaporudi ataendelea kuziongoza timu zake za Coastal Union na Simba kwenye mashindano la ligi ya NBC na Mashindano ya CAF!

IMG-20220908-WA0019.jpg
 
Back
Top Bottom