Clouds yaipotezea UKAWA

Hivi nchi ina radio moja tu clouds? Mbona inawawasha sana wafuasi wa CDM? Kwanini msianzishe radio yenu na nyinyi? Kazi kuja kulialia kila siku hapa clouds clouds tumechoka

Hiyo radio UKAWA inawauma kwasababu inawachana ukweli na kibaya zaidi ndo redio inayosikilizwa na watu wengi sana hapa tanzania. Hivyo madhara yake wanayajua.

Waulize swali kidogo. Lile gazeti la udaku la tanzania daima mbona linaandika ugoro wa ufipa kila siku na wanalitetea kwa kile liandikacho? Iweje iwe nongwa kwa vyombo vingine vya habari viandike againsit na wanavyotaka iwe nongwa?
 

Pole sana kwakuchelewa kujuwa ndugu tulikwisha juwa sikaredio wanyonge bali ccm. Na ruge aliambiwa kama kunawatu kumi wa mwisho kuilaumu serikali basi yeye awe wa mwisho. Na kama hataki asubili rais ajae ataona kazi. Ilikuwa lov wapi usiniulize. Akili kichwani.
 
Je, kama ukawa nao wakiamua kupiga kampeni ya kusema wananchi wanaowaunga mkono waipotezee clouds kama wanavyotaka wao,watabaki salama?

Mi nadhan clouds wangeondoa msemo wao wa radio ya watu kwani kiuhalisia si radio ya watu tena.Ni redio ya ccm!

Mkuu kuna watu wanataka serokali 3, sasa wamechukia ukawa kutoka maana wametoa mwanya wa kupitishwa kwa 2! Ikumbukwe Kuwa bunge linaendelea, na hao siyo wajinga waendelee wakati wakijua ni ngumu kupitisha, wameshaona njia ya kupita, bora wangerudi wakabishana kwa hoja, wakishindwa ndiyo warudi kwa wananchi, wamegoma!! Kalagabaho!!!
 

Binadamu tunatofauriana sana!
Ukweli nikimuona mtu amebeba gazeti la Tanzania daima huwa namshangaa sana.
 
Naomaba Nikulize kwanza Mleta Mada Utaenda kujadili kitu Ambacho sicho kilicholetwa Mwezani? Ile rasimu ya Jaji warioba kwani Ukawa ndio wameikata kuijadili? 2 Clouds nafikiri inajulikana inamrengo gani kwahiyo siyojambo lakushanga sana kwa hilo

Kwani hiyo rasimu ya katiba imepelekwa bungeni kufanya nini? Kama ni kupitisha tu kwanini wasikae siku moja na kupitisha kisha iende kwa wananchi?
Imepelekwa bungeni kuichambua kurekebisha na kuiwasirisha kwa wananchi ili waipigie kura ipite.
Sasa hao ukawa wanataka ipitishwe kama ilivyo??? AkirI gani sasa hiyo?
Sasa waendelee kukaa nje huku mambo yanaenda kama kawaida, wakija kushtuka imeshafika kwa wananchi.
 
We hujui hako ka radio ka CCM?

Tena kanaendeshwa kwa mikono michafu ya 'wapiga minada ya sembe'? Hatuna la kushangaa hapo Clouds hawana lolote...maana hata kipindi cha uchaguzi 2010 hawa jamaa wakimtumia mchovu Kibonde ndio walikuwa wapiga debe wazuri wa Magamba, na pia waliongoza matamasha ya vijana kisanii kuipalilia ccm ndio MAANA akina kamanda Sugu, Selle, Prof J, na wengine walio ktk upande wa umma waliwapiga chini kwa sana kutokana na mwenendo wao wa 'uchumia tumbo'.
 
Hata watangazaji wake wote wana ngoma wanazotoa THT,her yangu mie masaa 24 siku 7 ni EA RADIO na RADIO ONE saaafi.
 

Rasimu ya warioba ni mawazo ya wananchi kama walivyosema japo si wananchi ni baadhi tu na asilimia kubwa ni maoni ya wana Kigoma, sasa kwanini mnang'ang'ania yapite kama yalivyo??? Acheni yachambuliwe, yalekebishwe kisha warudishiwe waTanzania wote wapige kura,kama hawayataki si watayakataa!!! Kwanini ukawa wanatumia nguvu kubwa hivi kama siyo uroho wa madaraka???.
 
Huyo jamaa wa Simiyu Yetu mbona kama babla, au ndo wale wachumia matumbo
 
Hayo si mawazo ya wanakigoma, ni ya watanzania kwa sababu tume ilipita kila kona ya nchi hii. Kila wilaya ilikuwa na takribani mikutano 12/bara na 22/Zanzibar. Hivyo ni maoni ya kutosha kutoka kwa watanzania. Hata kwenye kampeni za ccm hawawezi kufanya idadi kubwa ya mikutano kama iliyofanywa na tume. Hivyo tume inayjua matatizo ya watanzania zaidi kuliko ccm
 
Clouds kuna watangazaji au kuna kijiwe cha ghahawa! Mcdhalilishe taaluma ya uandishi,mtu ana dvs four 45 pts chuo magomeni mapipa,kazi clouds!
 
Tuache upofu wakisiasa. ITV na R.one wakiwa na ukawa(chadema) they are right and bright. Kituo kingine kikisapoti upande mwingine they are wrong. Jaman hata kula na kipofu hamuwezi? Mengi anaona interest zake znazuiwa na serikali so anaikomoa kwa kuwa opposit nao,kitu ambacho madhara yake ni madogo kuliko ambavyo serikali ikiamua kuitumia mawingu fm kwa sasa. Ndo station inayoskilizwa na vijana(wapenda mabadiliko) wengi zaidi tz. Mfano kile kipindi zito anamvutano mkubwa na chadema,kama alikuwa ana la maana sana lakusema anakwenda mawingu kwavile ndo inayoskilizwa sana na hasa vijana. Kwa mimi naona wala serikali haijaamua kuitumia vizuri mawingu fm kama Ukawa(chadema) inavoitumia IPP.
 
Ukweli unafiki kitu mbaya! Hivi inakuwa je mtu akikuunga mkono; kwako ni shujaa na unamuimbia sifa kibao! Mtu huyo huyo kesho akionyesha kuwa na msimamo ambao wewe huukubali, mara anakua adui, na unaanza kummwagia matusi kibao!
Kupo wapi uwezo wetu wa kuheshimu mawazo na uhuru wa mtu kuji-express? Kupo wapi uhuru wa kuchangia na kuweka hadharani mawazo yako, bila kuwa na hofu ya kupigwa mawe, kutukanwa na kubezwa?
TUnajenga nchi ya watu wa namna gani iwapo kila mwenye wazo au msimamo tofauti na wako ni adui?
watanzania ni LAZIMA tuamke, tuheshimu mawazo ya watu WOTE ikiwa ni pamoja na mawazo yanayokinzana na misimamo yetu!
Kubadilika na kuanza kumpiga mtu mawe na matusi - simply kwa kuwa ana mawazo tofauti na yako - HUO NI UNAFIKI wa kiwango cha juu kabisa! TUBADILIKE!
 

ukweli unabaki kwamba kama ccm watafanikiwa kuja na katiba inayojali maslahi ya taifa hilo litakua pigo kubwa la ukawa.
 
Kilichopaswa kujadiliwa ni RASIMU YA PILI YA KATIBA kama ilivyowasilishwa na TUME YA KATIBA MPYA.Na rasimu inapendekeza muundo wa serikali 3 ndani ya nchi iitwayo JMT.Kero inakuja pale CcM walipokuja na pendekezo la ajabu la SERIKALI 2 na kutaka hoja yao hiyo ijadiliwe badala ya kujadili jinsi ya kusanifisha mawazo ya wananchi juu ya muundo wa serikali 3.
Hapo ndipo wana falsafa wanasema,BMK LIMETEKWA NA WAPUMBAVU WENYE TABIA YA KUSHINIKIZA HOJA ZA NGUVU badala ya kuongozwa na WAJINGA wenye kusikiliza,kuuliza na kudodosa ambao wakishaelimishwa husema,"AHAA!!!!KUMBEEE!!!! Na kisha mambo yakaenda sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…